Bendi pendwa Tanzania, Twanga Pepeta Internatinali, inatarajiwa
kuporomosha bonge la shoo ndani ya Jiji la Mwanza na Mji wa Nansio Ukerewe
katika viwanja vya CCM Kirumba na Nansio Ukerewe katika tamasha la kihistoria
la utamaduni wa msukuma na mkerewe linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi
Tarehe 27-04-2013 na Jumapili tarehe 28-04-2013 kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka
usiku.
Akiongea jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
Msaidizi wa Kampuni ya MyWay
Entertainment Rose Mwita Marwa, alisema bendi ya Twanga Pepeta imekuwa
mstari wa mbele kusaidia jamii na maendeleo ya vijana kupitia Muziki. Hivyo, burudani
ya bendi hii na burudani nyinginezo zitakazokuwepo ili kuhamasisha wakazi wa
Mwanza na Ukerewe kuhudhuria kwa wingi.
Rose alisema, “Tamasha hili linalenga kuhamasisha jamii ya msukuma, mkerewe na
makabila mengine kuenzi mila na tamaduni. Vilevile, jamii na falimia zilizopo
ndani na nje ya mikoa yao zikumbuke nyumbani na kutembelea wazee mara kwa mara”.
Aliendelea kueleza kwamba, zaidi ya
watu 3,000 na familia zao, watahudhuria kwa wingi tamasha hili la kihistoria
huku wakipata fursa ya;-
·
Kusikia historia ya msukuma na mkerewe kwa kina toka kwa wazee wanaotoka sehemu
mbalimbali hasa kwenye familia za watemi wa Kisukuma na Wakerewe.
·
Kuona maonyesho ya zana za kale za jadi zilizotumiwa na makabila haya
mawili.
·
Kuona na kucheza ngoma zote za asili ya msukuma na mkerewe pamoja na
vikundi tofauti tofauti vya ngoma za asili na sanaa za makabila mengine.
·
Kula aina zote za vyakula vya asili ya msukuma na mkerewe.
·
Kunywa vinywaji vyote vya asili ya msukuma na mkerewe.
·
Kupata burudani toka kwa wasanii wa kizazi kipya kutoka Dar es Salaam.
Vilevile alisema, wamewaalika
viongozi wa serikali yetu, viongozi wa dini zote, wawekezaji na wafanyabiashara
wakubwa ndani na nje ya mkoa wa Mwanza, viongozi wa asasi zisizo za kiserikali za
serikali na wanafunzi kutoka vyuo na shule mbalimbali katika mkoa wa Mwanza.
Tumejipanga vizuri katika kufanikisha siku za historia za
makabila yote Tanzania kila mwaka tukianza na makabila ya ukanda wa kaskazini, likifuata
Tamasha la Wahaya June 29, tukiwa na lengo la kuhamasisha jamii kuenzi mila na
na kukumbuka na kuzipeleka familia nyumbani.
Tamasha hili limedhaminiwa na;-
Balimi Extra
Lager, Safari Lager, Pepsi, Star TV, Radio Free Africa, JB Belmont Hotel,
Mwanza Institute, Toyo na La Kairo Investiment.
No comments:
Post a Comment