NAOMBA
SAMAHANI KWA WOTE MTAKAOITAZAMA HII PICHA. ISIPOKUWA IMENILAZIMU
KUWAWEKEA ILI KAMA KUNA NDUGU YAKE AWEZE KUJITOKEZA NA KUTAMBUA SEHEMU
MWILI WA NDUGU YAO UMELAZWA.
HUYU MTU INASADIKIWA KUFANYIWA
UKATILI WA KUMWAGIWA TINDI KALI MWILI MZIMA KISHA KUMTUPA KATIKA VICHAKA
VYA KIBAMBA HOSPITALI NA MAKONDEKO JIJINI DAR ES SALAAM, JE HUU NI
UNYAMA GANI HATA SASA TANZANIA TUMEKENGEUKA NA KUIGA MILA ZA MATAIFA YA
WENGINE AMBAO KUUWANA KWAO SI JAMBO GUMU, IVI TATIZO NI UONGOZI, AU
FEDHA ? LAKINI KUMBUKA KUWA ILI LEO LINATOKEA KWA HUYU LAKINI IPO SIKU
LAWEZA TOKEA HATA KWAKO AMA NDUGU YAKO, KWA HIYO KUNA KILA SABABU YA
TAADHALI KWA KILA MMOJA WETU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU UJAO, NA HAYA YOTE
YANATOKEA KWA AJILI YA BAADHI YA WATU KUJISAFISHIA NJIA ILI WAPATE
NAFASI YA MADARAKA, KWANI NANI KAKWAMBIA KWAMBA SISI TUNAHITAJI UONGOZI
WAKO USIOKUWA NA HEKIMA, UPENDO, AMANI, NA MSHIKAMANO? UNATUIJIA
HUKIONEKANA KAMA BINADAMU KUMBE MOYONI MWAKO KUNAWAKA TAMAA YA UUWAJI,
USHAWISHI UOVU, NA MWIVI, KINACHOKUFANYA UWEZE KUTENDA AMA KUAGIZA
MAUAJI YA KIKATILI KAMA HIVI NI NINI? JE NI KWA AJILI YA KUTAFUTA
UTUKUFU WA DUNIANI ? JE UNATAZAMIA KUINGIA PEPONI? MAANA UNASALI KILA
IJUMAA NA JUMAPILI, INAUMA SANA ILA KUMBUKA UKIUA KWA UPANDA UTAKUFA KWA
UPANGA, HATA KAMA KWA TINDI KALI NA WEWE SIKU ITAKUKUTA HIYO HIYO TINDI
KALI, FUNGUA HAPA KWA PICHA ZAIDI.
Baadhi ya wakazi wa jiji wakijaribu kutambua mwili wa marehemu
Askari Polisi wapelelezi wakiwa eneo la Tukio
Wakazi wa jiji wakitafakali jambo
mwili ukiwa eneo alikotupwa.
wakazi wakimiminika kutambua mwili
Eneo hili la Daraja la Kibamba na Makondeko, ambako ndiko tukio hili limefanwa
Poli ambalo ulitupwa mwili wa marehemu
No comments:
Post a Comment