Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd kwa kushirikiana na kituo bora cha Matangazo TIMES FM 100.5 kwa pamoja wanakuletea bonanza la vyuo SEASON TWO itakayofantika katika viwanja vya ustawi wa jamii kijitonyama siku ya jumamosi wiki hii tarehe 29/11/2014. Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa dar es salaam, vinatarajia kuchuana katika bonanza la hilo litakalokuwa na michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball, ikiwa ni sehemu ya pili ya mchujo wa kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015,baada ya sehemu ya kwanza kumalizika kwenye chuo cha DIT Mwishoni mwa juma na kuhusisha vyuo mbali mbali vya Dar es salaam.
Sehemu ya pili ambayo imepangwa kufanyika katika uwanja wa ustawi wa jamii kijitonyama jumamosi ya tarehe 29 mwezi huu inatarajia kuwa ya kusisimua kutokana na Michuano hii ya Mtoano kuwa kivutio kwa Wachezaji na Mashabiki ambao wengi wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wanaofika kushuhudia michuano hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu. Timu zinazochuana juma hili ni pamoja na Institute of Adult Education, Institute of Social Work (ISW) – DSM, Lugalo Military Medical School – Dsm, St. Joseph College (University), Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ) – DSM, National Institute of Transport (NIT) – DSM, Bandari College – DSM,huku timu mwalikwa ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.
Timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya pili wiki iliyopita kwa upande wa soka ni Chuo cha IFM waliofanikiwa kuwafunga DIT katika fainali kwa njia ya penalt baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 bika kufungana, kabla ya kutinga hatua hiyo ya fainali kikosi cha IFM kilifanikiwa kuwafunga CBE katika mchezo wa kwanza kwa 2-1 wafungaji wa magoli wakiwa ni Godlisten Kessy aliyepachika mabao yote mawili dakika ya 15 kipindi cha kwanza na dakika 51 kipindi cha pili huku bao la CBE likiwekwa wavuni na Mwendo Sitena mchezo uliochezeshwa na mwamuzi Mussa Charles. Wakati DIT wakafanikwa kutinga fainali baada ya kuwafunga Muhimbili kwa bao 1-0, TRA ikaambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Times, wakati Voleyball wanaume CBE waliibuka kidedea dhidi ya wenyeji DIT, huku David Davic akiibuka (Best Spiker), Dickison Benjamini wa DTI, aliibuka (Best Broker), Gideon Joseph wa IFM aliibuka (Best Recever), Joseph Mafuru wa CBE aliibuka (Best Seter), Daniel Msambusi wa DIT aliibuka (Best Rebelo), na MVP katika ufunguzi huo akiwa ni nyota wa CBE Samweli Kitime. Kwa upande wa mpira wa mikono netball pia IFM ilijidhiilisha kuwa kijoo cha mjini baada ya kufuata nyayo za kaka zao kwa kuwafunga chuo cha DIT kwa 19 dhidi ya 14 huku wafungaji katika mchezo huo wakiwa ni Sarah Shaaban aliyefunga magoli 12(GS) na Teckila teas akifunga 7 (GA) katika mchezo wa Fainali pia uliofanyika kwenye viwanja vya DIT. CBE pia ilimg’ara katika mchezo wa Kikapu (Basketball) kwa upande wa wanaume baada ya kuwafunga DIT katika mchezo wa Fainali kwa vikapu 51-37 ambapo wahezaji waliong’ara ni Sarehe Ramadhani, Evance David, Edger Mwakase huku kwa DIT waking’ara wachezaji Evance Kamola na Charles Poul. Michuano hiyo ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA imeanza siku ya jumamosi tarehe 22/11/2014 ikiwa ni ufunguzi ambapo vyuo vilivyohusika katika ufunguzi huo ni pamoja na IFM, DIT, TRA, MUHIMBILI, CBE, ROYAL, MLIMANI Profesianal na timu Mwalikwa Times Fm 100.5. Aidha vyuo vyote vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa kuwahi Viwanjani ili kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano hiyo ya mtoano kuanza na ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa Bonanza na inafanyika kila siku za jumamosi kutokana na wanafunzi kuwa masomoni katika siku za kawaida. kila mwaka michuano hii itakuwa ikifanyika kwa kushirikisha vyuo mbali mbali vya elimu ya kati hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM. Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha, na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Wadhamini aliojitokeza mpaka sasa na kuonyesha nia ya kusaidia mashindano hayo ni pamoja na Coca Cola, Vodacom, MLONGE BY MAKAI, CXC –Tours, na 100.5 Times Fm. lakini hata hivyo dirisha la wadhamini bado liko wazi kwa maana bado gharama ni kubwa za uendeshaji ambapo wajitokeze waweze kusaidia michezo hii iliyoanza kwa shamrashamra nyingi na kuwa na mvuto kwa watazamaji ususani wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza.
No comments:
Post a Comment