-DACICO
MWENDO MDUDO
-USTAWI
WA JAMII YATUMIA VYEMA UWANJA WA NYUMBANI.
Na:
Mwandishi Wetu,
Michuano ya NACTE INTER
COLLEGE CHAMPIONSHIPS TANZANIA-DAR ES SALAAM 2015, Leo imeendelea tena kwenye
Viwanja vya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambako Timu za kundi A zimecheza na
mchezo uliokuwa gumzo ni baina ya Chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere dhidi
ya Chuo cha Bandari, ambapo hadi Mwisho wa Mchezo Timu hizo zimeweza kufungana
3-3.
Timu ya Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ndiyo waliokuwa wa kwanza kupachika mabao 2
kipindi cha kwanza, ambapo hadi timu hizo zinakwenda Mapumziko Mwalimu Nyerere
ilikuwa mbele kwa 2-0.
kipindi cha pili
kilianza kwa kasi ambapo timu zote zilifanya mabadiliko ya hapa na pale lakini
ni ya Mwalimu nyerere tena iliyoweza kupata bao la tatu kabla ya Timu ya
Bandari Kusawazisha mbao yote kwenye dakika za Mwisho za mchezo huo ambao hakika ndiyo uliokuwa gumzo katika siku
ya leo.
Mchezo mwingine ilikuwa
ni kati ya IFM dhidi ya chuo cha Taasisi ya
Elimu ya Watu wazima, ambapo mchezo huo timu hizo zimekubali kugawana
pointi moja moja sambamba na wenzao wa chuo cha Kilimanjaro kwa mama ngoma
waliogawana pointi na chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT).
Matokeo ya kundi la
Uwanja wa Ustawi wa Jamii timu ya Chuo cha Biashara CBE, wamefanikiwa kujipatia
Pointi zao 3 na magoli mawili baada ya timu ya chuo cha Uhasibu kushindwa
kutokea Uwanjani katika kipindi kilichopangwa.
mchezo mwingine ilikuwa
ni baina ya timu ya Chuo cha kodi ambao wamecheza na timu ya kitivo cha
engeneering ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam zimeweza kugawana Pointi baada ya
timu zote kushindwa kufika Uwanjani.
wakati mchezo wa Mwisho
wenyeji timu ya chuo cha ustawi wa jamii imeweza kujipatia Ushindi mnono wa
Mabao mawili na hivyo kujizolea pointi zote tatu dhidi ya timu ya chuo cha
Wauguzi wa Muhimbili, ambapo michezo hiyo awali ilipangwa kufanyika kwenye
Viwanja vya chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini imelazimu kubadili Uwanja
kutokana na Viwanja vya Chuo Kikuu kuwa na ratiba katika kipindi hiki hivyo
michezo yote sasa itafanyika kwenye viwanja vya Ustawi wa jamii katika hatua
hii ya makundi.
Kundi B ambao michezo
yake inafanyika kwenye Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mchezo wa kwanza
ulizikutanisha timu za chuo cha St.Joseph, ambapo katika mchezo timu ya St.
JOSEPH ilifanikiwa kuibua na ushindi wa mabao mawili kwa bila (2-0) dhidi ya
timu ya chuo cha Njuweni Insititute.
mchezo mwingine Timu ya
chuo cha Wauguzi Tumbi ikafanikiwa kupata Point 3 baada ya kujipatia mabao
mawili dhidi ya kitivo cha UDBS ambao walishindwa kutokea uwanjani kabla ya
DACICO kidedea dhidi ya timu ya chuo cha taifa cha Teckinolojia (D.I.T) .
Washindi wawili katika
kila kundi ndiyo watakaoingia hatua ya Robo fainali itakayoshirikisha jumla ya
timu nane huku timu mbili zikipewa nafasi ya kuingia kwa njia ya upendeleo(Best
Looser).
Michezo hii inaratibiwa
na Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Enter tainment C.o Ltd, ya jijini
Dar es Salaam kwa Udhamini wa NACTE, SBC TANZANIA, Vodacom, CXC Tours, Zinduka,
Mlimani Radio & Mlimani Tv, Clouds Media, Michuzi Media, Tanzania Daima,
Free Media, Global Publishers, Gazeti la Champion, Njuweni Institute Kibaha na
Mpaluleblog:
Mawasiliano Tupigie:
+255-713-86-91-33 au +255-767-8691-33
No comments:
Post a Comment