Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) nchini Tanzania Dkt.Albina Chuwa
akifungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala la wataalam na Wakuu
wa Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na
Kifaransa leo jijini Dar es salaam. Kongamano hilo la siku 2 linajadili namna
Bora ya uendeshaji wa Taasisi za Takwimu na namna ya kukabiliana na changamoto
mbalimbali za masuala ya Takwimu Barani Afrika.
(Picha Zote na: Aron Msigwa
–MAELEZO
Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo
akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa
kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu
wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha
ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa
Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna
nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa
kutumia takwimu sahihi.
Bw. Andry
Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za
Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam.
Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.
Baadhi ya
watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la
Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu
Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.
Watalaam na
wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika
wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa la siku 2
linalojadili masuala ya Uongozi na utawala wa taasisi za takwimu Barani Afrika
linaloendelea jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment