Huku ulimwengu
ukiadhimisha miaka 70 tangu ndege za kijeshi za Marekani ilipodondosha
bomu la kinyuklia juu ya Nagasaki tazama picha za janga hilo.
Ibada maalumu za ukumbusho zinaendelea kufanywa
katika mji wa Nagasaki, nchini Japan, kuadhimisha miaka 70 tangu
kulipuliwa kwa bomu ya atomiki jijini humo.
Tarehe 9 Agosti mwaka wa 1945, ndege ya Marekani
ikiwa imejihami kwa silaha zenye nguvu za kitonaradi ilidondosha bomu la
pili kuwahi kutupwa katika uwanja wa kivita katika mji wa , Nagasaki
ambao ulikuwa ndio kitovu cha uzalishaji wa viwanda nchini Japan.
Siku 6 tu baadaye Japan ilitangaza kuwa imejisalimisha katika vita hivyo vya dunia.
Takwimu zinasema kuwa takriban watu 74,000 waliangamia.
Hii ilikuwa ni idadi kubwa zaidi ya watu hususan ikitokea siku tatu tu
baada ya bomu la kwanza la kinyuklia kuua zaidi ya watu 140,000 mjini Hiroshima.
Bomu hiyo iliyotikisa na kuangamiza kabisa mji wa Nagasaki ilijulikana kwa jina la utani kama ''Fat Man''.
Ndege iliyotumika kutupa bomu hilo ilijulikana kama Bockscar, ilipaa kutoka kisiwa cha Mariana.
Rubani wake alikuwa Meja jenerali Charles Sweeney.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000 waliuawa katika milipuko hiyo miwili,
Wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi.
Katika ibada ya ukumbusho iliyoandaliwa leo mjini Nagasaki,
wahasiriwa walimzomea waziri mkuu wa bwana Shinzo
Abe kwa kutaka kubadilisha katiba ya taifa hilo ilikuwaruhusu wanajeshi
wa Japan kuhusika na mapigano.
Meya wa mji wa Nagasaki naye alivutia waya huohuo
akimkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa jitihada za kubadilisha
katiba ya nchi.
No comments:
Post a Comment