TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Sunday, December 20, 2015
NAIBU WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MIWANI KUONA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO KITUONI HAPO.
Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Miwani, Wilaya ya Kati Unguja Fatma Keisi Ali akimtembeza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo sehemu mbali mbali za Kituo hicho kuona changamoto zinazowakabili ikiwemo tatizo la umeme, maji na upungufu wa wafanyakazi kituoni hapo.
Kituo cha Afya cha Miwani ambacho Naibu Waziri ameahidi kukiboresha ikiwa pamoja na kuondosha tatizo la umeme, maji na kujenga nyumba ya wafanyakazi.
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Miwani baada ya kusikiliza matatizo yanayokikabili kituo cha Afya cha Miwani.
Naibu Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo akiwasilikiza wananchi wa Miwani wakati alipofanya viara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho kujua matatizo yanayokikabili kituo hicho, (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mohammed Saleh Jidawi.
Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akitoa ufafanunuzi baadhi ya masuala yaliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Miwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo akiwasilikiza wananchi wa Miwani wakati alipofanya viara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho kujua matatizo yanayokikabili kituo hicho, (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mohammed Saleh Jidawi.
Mmoja ya wananchi wa kijiji cha Miwani akimueleza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) matatizo wanayoyapata kutokana na upungufu wa huduma muhimu katika kituo hicho .
Picha Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment