TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Sunday, December 20, 2015
WAFANYABIASHARA KIGOMA WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF).
Mkuu wa Mkoa wa kigoma akiwaeleza wafanyabiashara(ambai hawapo pichani) wa Kigoma umuhimu wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya(NHIF)
Ofisa matekelezo kutoka mfuko wa bima ya afya Kigoma Evance Ndyamkama akiongea na wafanyabiashara wa Kigoma jinsi ya kujiunga na mfuko huo
Makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Mkoa wa Kigima(TCCIA) Sethi Naftari akisona hotuba ya wafanyabiashara kwa Mgeni rasmi Issa Machibya na maofisa mfuko wa bima ya afya
Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigima wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo
===== ==== ==== =======
Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,KigomaWAFANYABIASHARA Mkoani hapa wametakiwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya(NHIF) ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya wakati akifungua mkutano wa wafanyabiashara na maofisa wa NHIF wa Mkoa wa Kigoma.Machibya alisema kuwa suala la kuugua ni la kila mtu na ugonjwa huwa unakuja bila ua taarifa,na magonjwa menfine gharama za matibabu zipo juu lakini kama mtu ana kadi ya bima atakuwa na uhakika wa matibabu."Nina waomba wafanyabiashara mjiunge na mfuko huu wa bima ya afya kwani mtakuwa na uhakika wa matibabu kipindi cha mwaka mzima"alisema MachibyaAliwautaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na bima ya afya ili kuongeza wigo mpana wa wananchi wanaonufaika na huduma zao.Naye ofisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya Mkoani Kigoma Evance Ndyamukama alisema kuwa kila mfanyabiashara anatakiwa kulipia shilingili elf 76000 itakayomwezesha kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mzima.Naye Makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara mkoa wa Kigoma(TCCIA)Sethi Naftari aliuomba mfuko huo uwape kipaumbe cha kuweka na wategemezi wao wanne katika hiyo shilingi elf 76000 kama wafanyavyo watumishi na watu wa makundi mbali mbali."Kama kweli NHIF mmelenga kutusaidia sisi wananchi wa kawaida tunaomba tuwaingize na sisi wategemezi wetu kwenye hayo malipo na yasiwe malipo ya mtu mmoja kwani sisi tumejiajiri"alisemaNaftari
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment