TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, May 28, 2012

ZIARA YA WAZIRI KIGODA KATIKA KIWANDA CHA URAFIKI

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mh, Abdala kigoda akiongea na wajumbe pamoja na Viongozi wa kiwanda cha Urafiki jijini Dar es Salaam alipotembelea kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam ambapo aliziona changamoto nyingi zinazozikabili kiwanda hicho ikiwemo mishahara miidogo ya wafanyakazi na akaahidi kuzifanyia kazi.
Diwani wa kata ya Ubungo  jijini  Dr es Salaam Mh, Bonifas Jacob  akieleza changamoto zinazo wakabili wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na usimamiaji mbovu wa Kiwanda hicho mbele ya Waziri.
Baadhi ya wafanyakazi, Viongozi pamoja na wajumbe mbalimbali waliohudhuria kwenye ziara hiyo wakimsikiliza Mh, Waziri kwa umakini.
Naibu Meneja uchapishaji na utiaji rangi kwenye kanga Bw, Solomon Laban(kulia) akimuelekeza waziri namana mtambo huo wa utiaji Rangi unavyofanya kazi  akikagua baadhi ya Mitambo ndani ya kiwanda hicho.
Waziri akikagua uzalishaji wa kanga kiwandani hapo.
Mh. Waziri wa viwanda na Biashara akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya kumaliza matembezi.

Uzinduzi rasmi wa tawi la Chadema Washington Dc wafanyika

Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc  kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mhe. Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi,  Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, Dogo Janja, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania
Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
Mwanachama wa chadema kutoka Boston kamanda Doto akiuliza masuali tofauti  katika mpango mzima wa uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc uliofanyika jana Mei 27, kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University  Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
Mhe. Leticia Nyererewenye uzinduzi wa watawi la Chadema Washington Dc
Mhe. Peter Msigwa akiandika masuali yaliokuwa yakiulizwa na baadhi ya wakireketwa
Mhe. Maryam Msabaha kwenye uzinduzi wa tawi la Chadema Washington Dc
Baadhi ya wakereketwa wachukua kadi baada ya uzinduzi wa tawi la chadema Washington
 Mhe. Nassari Joshua (Dogo Janja) Akishanga mamia ya wana DMV waliofurika katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc

REDD'S MISS TABORA HUYU HAPA

 Mshindi wa taji la Redds Miss Tabora 2012 Sarah Paul katikakati akiwa na washindi wengine wawili Glory Mongi kulia na Alice Amour kushoto mara baada ya kufanikiwa kutawaza washindi wa taji hilo na kufanikiwa kuingia katika kinyanganyiro cha kanda kuelekea kwenye fainali ya Redds Miss Tanzania 2012 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Toleo la Leo.
BIA YA CASTLE LITE SASA KUPATIKANA KATIKA KOPO
Dar es Salaam, May 28. 2012:
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi muonekano wa kopo lililojazwa kinywaji hicho ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia walaji upatikanaji wa Bia hiyo iliyotokea kupendwa na watumiaji wa vileo na kuifanya iwe bia inayokua kwa kasi hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; Leo tunazindua ujazo mpya wa bia ya Castle lite, bia yenu muipendayo kwa sasa inapatikana katika kopo lenye ujazo wa mililita 330. Uamuzi huu unatokana na mahitaji makubwa toka kwa watumiaji na wapenzi wa bia hii ambayo imekuwa ikipatikana katika chupa yenye ujazo wa mililita 375. Wateja wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale walipo au kuwa nayo popote waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa peke yake kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji kurudisha chupa kila waitumiapo.
Uzinduzi wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza upatikanaji wa kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k kote nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao waipendayo na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni shilingi 1700/- na bei ya reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile 1700/-.
Kwa upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Tbl Edith Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini, “ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia Castle Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote. Alisema Edith.
-MWISHO-



 Meneja wa kinywaji cha Castle Lite Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa castle lite ya Kopo, kulia ni meneja habari na mawasiliano ya Umma wa Tbl Edith Mushi.
 
 

Sunday, May 27, 2012

MBUNGE WA JIMBO LA KILOLO PROF PETER MSOLLA AKIMBIA KUWEKWA KITIMOTO NA WAPIGA KURA WAKE

Mwakilishi wa mkurugenzi wa Kilolo John Kiteve akijibu maswali katika mdahalo huo ambao ulipaswa pia kuhudhuria na mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla
Na Francis Godwin,Blog

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla amekwepa kushiriki mdahalo wa kimaendeleo katika Kati yake na wananchi wa jimbo hilo leo .

Katika mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Upendo Ruaha mbuyuni mbunge Profesa Msolla ambaye pia amepata kuwa waziri wa mawasiliano sayansi na Teknolojia mbali ya kupewa taarifa na waandaaji wa midahalo hiyo ambao ni azaki za kiraia Tanzania ,mbunge huyo alipaswa kufika katika ukumbi huo kuanzia majira ya saa tatu asubuhi ila hadi saa Saba mchana mbunge huyo wala katibu wake hawakuweza kutokea ukumbini na kupelekea mdahalo huo kuchelewa kuanza .

Mratibu wa midahalo hiyo mkoa wa Iringa Raphael Mtitu alisema kuwa mbunge huyo alipewa taarifa kwa wakati juu ya uwepo wa midahalo hiyo japo alisema kuwa anasikitishwa na hatua ya mbunge kutofika na kuwa ni mbunge wa kwanza toka kuanza kwa midahalo hiyo kushindwa kufika huku akidai kuwa kutofika kwake bado hakujazuia mdahalo huo kuendelea

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA YAFANA, LONDON-UINGEREZA

Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika hapa nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London.
Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika.
Kutoka kulia, Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George,
Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika
Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika hapa London
 
Siku ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini Uingereza. Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika, kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na mbaye ni Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Warren Blackbeard.

Aidha Mheshimiwa Balozi Roy Blackbeard, alitoa salamu maalum kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, ambaye pia ni Raisi wa Benin.

Balozi Roy, alielezea changamoto nyingi zinazo tokea Barani Afrika na kwingineko na juhudi maalum zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Afrika kutatua migogoro na matatizo ya mara kwa mara yanayolikumba Bara letu la Afrika.

kabla ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Uganda Mheshimiwa Mama Joan Rwabyomere, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki wa Afrika na Wageni mbalimbali waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao na kujumuika pamoja na waafrika wote duniani kuadhimisha siku hiyo hapa nchini Uingereza. Amani, Upendo, Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika vilihimizwa katika maadhimisho hayo.

Airtel yafanya promosheni ya huduma ya ‘Jiunge na Supa 5’ kwa kishindo Mkoani Dodoma.

Wasanii wa kikundi cha Kinoko kutoka Dar es Salaam wakilishambulia
jukwaa wakati wa promosheni ya Airtel Jiunge na Supa 5 katika viwanja
vya Jamhuri, Mkoani Dodoma jana. Uzinduzi rasmi ulifanyika jijini Dar
es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakihamia Airtel wakati wa promosheni
ya Airtel Jiunge na Supa 5 mkoani humo jana.
Mkazi wa Dodoma, Queen Jackson akishindana kucheza taarab wakati
wa promosheni ya Airtel Jiunge na Supa 5 mkoani humo jana.
Zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mkononi zilitolewa ili kufanya
promosheni hiyo iwe ya aina yake.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria promosheni ya Airtel Jiunge
na Supa 5 Mkoani Dodoma jana.

Idadi ya abiria ATCL yazidi kupaa

Na Mwandishi Wetu.
IDADI ya abiria wa Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) imezidi kuongezeka kila kukicha kutokana na wananchi kuonyesha uzalendo na imani kwa kampuni hiyo , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Paul Chizi amesema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari jana Chizi alisema kutokana na imani hiyo, kampuni yake imejizatiti kuleta mabadiriko makubwa katika sekta ya usafiri wa anga kupitia mpango  wa maendeleo wa miaka mitano wa shirika hilo.
Chizi alisema tangu uzinduzi wa safari za Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza wiki moja iliyopita kwa kutumia ndege ya aina ya Boeing 737-500,kampuni yake imekuwa ikijaza abiria takribani 106 katika kila safari kwa siku tatu mfulilizo ikiwemo na siku ya jana hali ambayo inaashiria kuwa wananchi wameanza kuwa na imani na huduma zinazotolewa na shirika lake.
 “Ndege yetu kwa takribani siku tatu zilizopita imekuwa ikija katika safari zote za Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza . Sikujua kuwa tutakuwa na uwezo wa kurejea na kupata mapokezi ya namna hii kwa haraka kutokana na kuwa kuna watoa huduma wengine katika njia hii .
 “Baada ya wananchi kuonyesha imani na uzalendo,tutaendelea na kuongeza nguvu zetu katika kutoa huduma zetu kwa wakati na kwa bei nafuu. Nawaomba wananchi kuendelea na uzalendo wanaouonyesha kwa faida ya kampuni yetu na nchi nzima kwa ujumla,” alisema.
Chizi alisema kuwa mipango ya kampuni hiyo ya kupata ndege nyingine ambayo itatumika katika safari za kimataifa katika miezi mitatu mpaka sita ijayo inaenda vizuri na kuongeza kuwa kampuni itatoa taarifa kamili wakati muafaka utakapofika.
“Kutokana ukweli kuwa tunatarajia kuanza safari za kimataifa, ni dhahiri kuwa ndege ambayo  tunategemea kuleta lazima iwe kubwa,” aliongeza.
Alisema kuwa kampuni yake kwa sasa imejikita katika utekelezaji wa mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano utakaosaidia kuongeza ubora katika kampuni hiyo na kuboresha utoaji huduma kwa ujumla.
“Tutajikita katika kuongeza ubora wa huduma tunazozitoa na vilevile kuchukua nafasi ile tuliyoipoteza hapo nyuma. Tunamatarajio ya kupata ndege nyingine ya Boeing na mazungumzo yameshaanza na tumefikia pazuri,” alisema.
Kurudi kwa huduma za ndege ya ATCL kumeanzisha  vita ya viwango vya bei za usafiri wa anga bada ya ATCL kutoza bei ya shilingi 199,00 kwa safari zake kwenda na kurudi (return ticket) na kusababisha watoa huduma wengine wakiwemo Precision Air nao kupunguza gharama zao ile ilikukabiriana na ATCL.

KWA MUJIBU WA TFF KAMATI ILIYOUNDWA YANGA NI BATILI, KLABU ITAENDELEA KUWA CHINI YA KATIBU MKUU NA SEKRETARIETI YAKE

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Mei 26 mwaka huu ili kutoa mwongozo wa nini kifanyike ndani ya Yanga baada ya wajumbe wake kudhaa kujiuzulu. Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ilikuwa imeomba mwongozo huo TFF.
 
Baada ya kupata taarifa rasmi kutoka Yanga, Kamati imebaini kuwa Kamati ya Utendaji ya Yanga imekosa akidi baada ya wajumbe wake wengi kujiuzulu hivyo kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kwa mujibu wa Ibara ya 32(1) ya Katiba ya klabu hiyo.
 
Hivyo, Kamati imetoa mwongozo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambayo ndiyo msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuwa ili Kamati ya Utendaji ya Yanga iwe na nguvu za kikatiba kufanya shughuli zake ikiwemo uamuzi wa masuala mbalimbali ndani ya klabu hiyo ni lazima iwe na akidi.
Kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) ya Katiba ya Yanga nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zinatakiwa kujazwa katika Mkutano Mkuu wa Kawaida ujao.
Pia Kamati imebaini uteuzi wa kujaza nafasi zilizo wazi za wajumbe uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mei 21 mwaka huu ni batili kwa vile Kamati ya Utendaji iliyofanya uteuzi huo haikuwa na akidi.
Ili kupata akidi na kufanya uamuzi Kamati ya Utendaji ya Yanga yenye wajumbe 13 inatakiwa kuwa na asilimia 50 ya wajumbe wote, hivyo ili wafanye uamuzi halali hawatakiwi kupungua saba.
Kwa wajumbe ambao hawajajiuzulu; Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia kwa sasa hawawezi kufanya shughuli zozote za Yanga hadi nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zitakapojazwa.
Kama inavyoelekeza Katiba ya Yanga, shughuli za kila siku za klabu hiyo zitaendelea kufanywa na Sekretarieti ya Yanga ambayo kiongozi wake ni Katibu Mkuu.
 
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji

TAIFA STARS, MALAWI ZAINGIZA MIL 40/-

Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 40,980,000.
 
Mapato hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 51,000 na sh. 20,000. Washabiki 9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.
 
Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 4,714,803, asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh. 10,608,306).
 

TWIGA STARS UWANJANI ETHIOPIA LEO

Twiga Stars inacheza leo (Mei 27 mwaka huu) na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) kuwania tiketi ya kucheza fainali zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa saa za nyumbani itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa ulioko jijini Addis Ababa na timu hizo zitarudiana Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Addis Ababa, wachezaji wa Twiga Stars ambayo imefikia hoteli ya Churchil, leo saa 4 asubuhi wamefanya mkutano wa mwisho wa maandalizi ya mechi hiyo na kocha wao Charles Boniface Mkwasa na baadaye kupata chakula cha mchana kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
 
Twiga Stars; Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Evelyn Sekikubo, Mwapewa Mtumwa, Etoe Mlenzi, Mwanahamisi Omari, Ester Chabruma, Fatuma Mustafa na Asha Rashid.
Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said, Semeni Abeid, Zena Khamis, Amina Ally, Rukia Hamis na Fadhila Hamad.
 
Mchezo huo unachezeshwa na Angelique Tuyishime akisaidiwa na Sandrine Murangwa, Speciose Nyinawabari na Salma Mukansanga wote kutoka Rwanda. Kamishna ni Catherine Adipo kutoka Uganda.
 

MASHINDANO YA JUDO YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Judo Tanzania Bw, Khalifa Kiumbemoto katikati akifuatila kwa makini Mashindano ya Mchezo huo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Landmark  jijini Dar es Salaam wa kwanza kushoto kwake ni Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Habari na Michezo Bw. Charles Mattoke  na wapili kushoto kwake ni Mdhamini wa Mashindano hayo kutoka Germin Copperation LTD Bw. Yulliy Tarverdyan. Katika Mashindano hayo Watanzania walionekana kushindwa na wachezaji kutoka Zanzibar.
Mchezaji wa Judo kutoka CCP Polisi Moshi (wa juu) Bw. Kisamerwa Magangwa akiwa amemgeuza mshindani wake Bw,.Mohammed Juma kutoka Magereza  Ukonga jijini Dar es Salaam katika mchezo huo.
Baadhi ya mashabiki walioudhuria katika
mpambano wa mchezo huo wakifuatilia kwa makini.
Wataalamu wa kufuatilia muda katika mashindano ya mchezo huo wakifuatilia kwa umakini mchezo huo.

Msama Promotions yadaka mtambo wa CD feki

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa wamefanikiwa kukamata mashine za kudurufu kazi za wasanii wa nyimbo ambazo tathmini yake katika utendaji kazi ni mkubwa ukilinganishwa na mashine nyingine alizowahi kuzikamata.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Msama alisema utaratibu wa kuwasaka wezi wa kazi za wasanii wa nyimbo za injili unaendelea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mashine hizo zilikamatwa mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Alisema mbali ya kukamata mashine hizo, pia walifanikiwa kumkamata mhusika anayefanya kazi hiyo, Anord Chrispian ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma hizo.

Msama alisema wamefanikiwa kukamata mitambo hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kusisitiza kuwa msako wa kuwabaini watu wanaojihusisha na kazi hiyo ya wizi unaendelea kwa ari na kasi aliyoanza nayo.

Akizungumzia tukio hilo Ofisa Upelelezi wa Jeshi la Polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa sababu za kiintelijensia, alisema mtambo huo wa kudurufu kazi za wasanii ulikamatwa katika nyumba ya mtu anayefahamika kwa jina maarufu 'Msukuma' katika eneo la Kimara Bonyokwa.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa akifanya kazi hiyo mchana na baada ya upekuzi wa zaidi ya saa mbili ndani ya nyumba hiyo walikuta mikasi na sindano za kufanya kazi ya kuandaa vifungashi vya CD, VCD, DVD na kaseti zinazozalishwa ndani ya chumba hicho.

Ofisa huyo wa upelelezi alisema kitu kingine kilichokutwa ndani ya chumba hicho ni wino wa kuchanganya katika kuandaa kava za bidhaa zinazozalishwa.

Alisema mitambo iliyokamatwa ni mitatu ya kudurufu CD na DVD, mitambo sita ya kudurufu kaseti na mitambo mitatu ya kuandaa kava za CD, DVD na kaseti.

Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mitambo hiyo ina uwezo wa kudurufu DVD 10,000 na VCD 30,000 kwa wiki na kwamba mmiliki wa mtambo huo ni miongoni mwa wasambazaji wakubwa wa kazi bandia za sanaa ya muziki.

Alisema kati ya maeneo ya Dar es Salaam yanayoongoza kwa kuwa na wazalishaji wa kazi bandia za wasanii Ubungo ndio eneo mama ikifuatiwa na Kimara na viunga vyake.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, mitambo na vifaa vyote vilivyokamatwa vimehifadhiwa katika kituo cha Polisi Kimara Mbezi kwa Yusufu na mtuhumiwa anashikiliwa kwa tuhuma hizo huku uchunguzi ukiendelea dhidi ya tukio hilo.

Kipindi kilichopita Kampuni ya Msama iliwahi kumkamata kiongozi wa mtandao wa kundi la wanyonyaji wa kazi za wasanii wa muziki wa injili, Francis Kamalamu, aliyekuwa akifanya biashara hiyo katika eneo la Ubungo Maziwa, Dar es Salaam.

Maofisa usambazaji wa kampuni hiyo, wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwabaini wezi wa kazi za wasanii na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wasambazaji na wazalishaji wa kazi hizo zimenaswa na zinatumiwa kuwatia nguvuni na taratibu za kisheria kuchukua mkondo wake.

Meneja Twanga Pepeta afukuzwa


Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka amesema kuwa wamemfukuza kazi Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Asha alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa Sospeter anaihujumu bendi kwa kuwashawishi wasanii kuihama bendi hiyo ili watue bendi ya Mashujaa ambayo naye ana mipango ya kutua huko.
"Tumeamua kumfukuza kazi Meneja wa Twanga Pepeta, Sospeter kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ubadhirifu na kutowajibika ipasavyo... anasuka mipango ya kwenda bendi ya Mashujaa, hivyo tumeamua kumuondoa mapema ili aende akiwa huru.
"Tumemwandikia barua ya kumfukuza kazi na pia anapaswa kulipa fedha za matamasha alizokwapua... nimeamini kumbe kikulacho kinguoni mwako," alisema Asha.
Pia alisema sababu nyingine ya kumtimua ni kukosa uaminifu baada ya kupokea fedha za matamasha mbalimbali takriban sh. milioni 6, lakini hajaziwasilisha ofisini kama ilivyo utaratibu wa kazi.
Asha alisema uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu kumhusu Sospeter umebainika kuwa ndiye amekuwa mstari wa mbele kuwashawishi baadhi ya wasanii wa Twanga Pepeta waliohamia Mashujaa na yeye ana mpango wa kuhamia katika bendi hiyo, hivyo anawatanguliza wasanii ili iwe rahisi yeye kujiunga nao atakapokamilisha dhamira yake.
"Mashujaa wenyewe wanadai eti Sospeter anajua siri nyingi za mafanikio ya Twanga Pepeta, hivyo atawasaidia kuimarisha bendi yao, tumeamua kumfukuza ili akawape vyema hizo siri," alisema Asha.
Mkurugenzi huyo alisema imebidi wamfukuze akajiunge na bendi hiyo anayoona anataka kuitumikia na kwamba safari aliyokwenda  Nyanda za Juu na bendi hiyo ndiyo ya mwisho katika utumishi wake akiwa na Twanga Pepeta.
Mbali ya hujuma za fedha na wasanii walioikimbia Twanga Pepeta kuhamia Mashujaa, Asha alisema kuwa imegundulika kuwa, Sospeter hivi sasa anamshawishi mpiga gita la besi wa bendi hiyo, Jumanne Said 'Jojo Jumanne' ili ahamie Mashujaa, hali aliyosema kuwa haiwezi kuvumiliwa kuendelea kuitafuna bendi hiyo.
"Tumemchunguza na kujiridhisha kumhusu huyu meneja Sospeter, ni mtu asiyeitakia uhai Twanga Pepeta... kama hilo ndilo lengo lake akafanye kazi na hao wanaomhitaji na mimi niendelee na mipango yangu na watu ninaoamini kuwa watanisaidia kuikuza tasnia ya muziki wa Twanga Pepeta," alisema Asha

TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI MAGUNIA 50 NA WATUHUMIWA WANNE MKOANI ARUSHA

Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya mifuko 50 ya bangi iliyokuwa kwenye gari baada ya kukamatwa tarehe 23/05/2012 wilayani Longido (PICHA NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA)
Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akihoji jambo kwa watuhumiwa hao.
MNAMO TAREHE 23/05/2012 MUDA WA SAA 9:00 ALASIRI HUKO SINYA VILIMA SABA MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA KATIKA WILAYA YA LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA WANYAMA PORI WALIFANIKIWA KUKAMATA WATU WANNE WAKIWA NA MIFUKO 50 YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI KWENYE GARI AINA YA CANTER DCM LENYE NAMBA ZA USAJILI T.922 AFJ MALI YA ZEPHANIA S/O KAMBEI MKAZI WA NGARAMTONI.
MADAWA HAYO YALIKUWA YANASAFIRISHWA KUTOKA KATIKA VIJIJI VILIVYOPO KANDO YA KANDO YA MLIMA MERU KUELEKEA NAIROBI NCHINI KENYA KUPITIA NJIA ISIYO RASMI (MAARUFU KAMA NJIA YA PANYA) ILIYOPO HUKO SINYA VILIMA SABA, NA BAADA YA KUONA HIVYO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA KWA ASKARI HAO NA HATIMAYE KUFANIKIWA KUWAKAMATA.
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA KATIKA TUKIO HILO NI BABUU S/O LAIZER (34) MKULIMA, MKAZI WA OLDONYOSAMBU,LOMNYAKI S/O LEKIBENGI (30) MKULIMA , MKAZI WA OLDONYOSAMBU, JOHN S/O JOSHUA AMBAYE NI UTINGO NA NI MKAZI WA OLDONYOSAMBU NA EDWARD S/O MOLLEL (27) DEREVA NA NI MKAZI  WA OLDONYOSAMBU.
BADO JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUWAHOJI WATUHUMIWA HAO ILI KUBAINI WAHUSIKA WENGINE NA PINDI UPELELEZI UTAKAPOKAMILIKA  WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI
(SACP) THOBIAS ANDENGENYE
TAREHE 25/05/2012.

ZANZIBAR HALI SI SHWARI

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto jana usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana.
(Picha/Zanzibar Yetu)
Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickoson Maganga lililochomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa jana katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu shilingi millioni 120.

KUFUATIA MACHAFUKO ZANZIBAR LEO

Askari wakiwa katika hali kutuliza vurugu, na hapa mkazi mmoja ambaye jina lake halikutambulika, akipewa kibano baada ya kuhusika na Ghasia hizo.
Askari wakiranda kutuliza Ghasia, ambazo watu wameandamana kupinga Muungano
Gari likiwa limeteketea kwa moto kufuatia ghasia hizo
Mmoja wa Waislam akionyesha kitu ambacho kinasadikiwa kuwa Damu wakati vurugu zikiendelea muda huu
Wakazi wa Zanzibar, wakiwa katika maandamano