TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 25, 2012

Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wakutana nchini Afrika Kusini kwa siku tatu.

Pichani shoto ni   Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,mapema jana jioni,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini.Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na mwisho ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo.
Pichani kulia ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo akifafanua jambo kwa makini wakati wa mchakato wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ulipokuwa umepamba moto jioni ya jana,katika mkutano uliofanyika kweny moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo mchana,Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na   Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
Pichani juu na chini Mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ukiendelea ndani ya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema jana mchana.
Baadhi ya Marais Wastaafu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa kwenye mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,ambaye pia ni Mratibu mkuu wa mkutano akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Mkutano huo mapema jana mchana.
Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin,Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar,Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Rais Thambo Mbeki wa Afrika Kusini,Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria,Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Rais Rupiah Banda wa Zambia wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana mchana kabla ya kuanza mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akijadiliana jambo na Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin walipokuwa wakiwasili kwenye viunga vya vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema jana kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
Pichani  mbele ni Marais Wastaafu wa Tanzania,Ally Hassan Mwinyi na  Benjamin Mkapa sambamba  na  Marais wengine wakiwasili katika viwanja vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema jana kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka nchini Tanzania,wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema jana kwa ajili ya kuripoti mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.Shoto ni Yvonne Msemembo (ITV) ,Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper),Nestor Mapund,Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications), Muondosha Mfanga (The Guardian) pamoja na Deus Mjatta (ITV).
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakijadiliana jambo nje ya ukumbi,kabla ya kuanza kwa Mkutano huo,Shoto ni Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications),Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper), Muondosha Mfanga (The Guardian).
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mapema janakabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,ambao umewashirikisha Marais Wastaafu nane wa Afrika. 

Rais wa Zanzibar azungumza na uongozi wa Wiazra ya uwezeshaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi na Ushirika,chini wa Wazri wake Haroun Ali
Suleiman,(wa tatu kulia) katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Ofisi
za Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar leo,(kushoto) Makamo wa
Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.       [ Picha  na Ramadhan
Othman,IKULU.]
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi na Ushirika, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa
Wizara hiyo katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Ofisi za Wizara
hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar leo.         [ Picha  na Ramadhan
Othman,IKULU.]

Salim Said Salim:Zanzibar kuna habari nyingi sana

Na Miza Chande-Maelezo Zanzibar 

WAANDISHI wa habari Zanzibar wametakiwa kubadilika katika uandishi wao kwa kuandika habari zinazogusa zaidi maslahi ya jamii badala ya kuandika habari za kupamba viongozi na watu maarufu nchini.

Imefahamika kuwa kuna habari nyingi za kuziandikia zenye maslahi na jamii ya Zanzibar ambazo zitakapojulikana kunaweza kupelekea mabadiliko makubwa katika jamii jambo ambalo litachochea maendeleo na kasi ya uwajibikaji.

Wito huo umetolewa na Mshauri wa Wanahabari Zanzibar Salim Said Salim wakati wa mafunzo ya siku nne iliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, juu ya uandishi bora na namna ya kuzingatia maadili.

Salim amesema miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakigusa hisia za wazanzibar ni pamoja na uingizwaji wa bidhaa mbovu ambazo zinapelekea wananchi kuwa na shaka katika matumizi na hata kupata maradhi mbalimbali.

Amesema kama waandishi watakuwa wakitekeleza kazi zao vizuri na kuweza kufichua masuala kama hayo Zanzibar haitaweza kuingizwa bidhaa hizo mbovu na wale ambao watafanya hivyo wataweza kufichuliwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za Nchi.

Hivyo waandishi wa habari ni watu muhimu katika jamii kwani kalamu yao wakiitumia vizuri kwa maslahi ya nchi basin nchi inaweza kupiga hatua za haraka sana na mambo maovu kama hayo na mengineyo hayataweza kutendeka.

Amewasisitiza waandishi kujiamini katika kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao ambayo ndio muongozo katika kutekeleza kazi zao vizuri bila ya kujali habari hizo imemgusa nani.

Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda amewataka waandishi hao kutekeleza yale yote waliyoyapata katika mafunzo hayo ili kutoa habari zenye kuvutia.

Amesema kuwa anaamini kuwa Taaluma waliyoipata itasaidia Taifa na kuwajengea hadhi waandishi na taasisi zao ili ziwe zinakubalika na jamii.

Chunda amesema kuwa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar itaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini viwe vya Serikali au binafsi kwani vyombo hivyo vyote ni vya Zanzibar na vinahudumia Wazanzibari hivyo  niwajibu wote kupata elimu ya habari ya kisasa

Mafunzo hayo ni ya pili kutayarishwa na Idara ya habari Maelezo Zanzíbar na yakwanza yalifanyika Jijini Dar es Salaam mwezi wa Machi mwaka huu ambayo yalikuwa yamejikita katika uandishi wa habari za kibiashara na uchumi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uingereza nchini

Mchakato wa Mapitio ya Ripoti ya Mfumo wa Haki za Mdai waendelea DSM na Mbeya

Jaji Mstaafu Buxton Chipeta akizungumza na Mahakimu, Wenyeviti wa Mabaraza ya Wilaya ya Ardhi na Nyumba pamoja na Madalali wakati wa warsha ya Mapitio ya Ripoti ya Mfumo wa Haki za Madai, katikati ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Agnes Mgeyekwa na kulia ni Mratibu wa mradi wa BEST Athasia Soka.
Munir Shemweta
Ofisa Habari
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Ofisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Anjela Shila (Katikati) akisisitiza jambo wakati wa majadiliano
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria (Mapitio) Angela Bahati (katikati) akiwa katika majadiliano wakati wa kupitia ripoti ya mfumo wa Haki za Madai.
Washiriki wa warsha ya kupitia ripoti ya Mfumo wa Haki za Madai wakimsikiliza Jaji mstaafu Chipeta

Ziara ya Naibu Waziri January Makamba Airtel

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  January
Makamba (kushoto) akipokewa na Mkurugenzi Mtendai wa Airtel Tanzania,
Sam Elangallor,  alipofanya ziara kukagua shughuli mbalimbali za
kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa
Mawasilino\ wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  January
Makamba (kushoto) akipokewa na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel
Tanzania, Chiruwi Walingo  alipokwenda kufanya  ziara ili kukagua
shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano
Mallya.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano
Mallya akiongozana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba (kushoto) katika ofisi za makamo makuu ya
Airtel  wakati wa ziara yake kukagua shughuli mbalimbali za kampuni
hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor (katikati)
akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
 January Makamba (kulia) na ujumbe wake wakati wa ziara ya naibu
waziri huyo kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es
Salaam jana.

CHAMA CHA RIADHA (RT) WAPATA UONGOZI MPYA


CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pongezi kwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Tanzania Daima, Tullo Chambo kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania (RT).

Chambo alitwaa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa RT uliofanyika Jumapili mjini Morogoro, ambapo ni miongoni mwa wajumbe wapya walioingia kwenye chama hicho.
Wengine walioshinda ni Anthony Mtaka ambaye anakuwa Rais mpya wa RT, wakati Makamu wa Rais Utawala ni William Kallaghe, Makamu wa Rais Ufundi, Dk. Ahmed Ndee, Katibu Mkuu, Suleiman Nyambui, Katibu Msaidizi, Ombeni Zavalla, Mhazini, Is-Haq Suleiman.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mwinga Mwanjala, Meta Petro, Peter Mwita, Rehema Killo, Lwiza John, Zakaria Barrie, Zakaria Gwanda, Robert Kalyahe na Christian Matembo.

TASWA inatambua Chambo ni mwanahabari mzoefu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mhariri wa habari za michezo na ni mtu mwenye kujua mambo mengi yanayohusu riadha, hivyo atakuwa kiungo muhimu kwa watu wa riadha, pia atakuwa kiongo kizuri kwa waandishi wa habari za michezo kuhusiana na mambo ya riadha.

TASWA inaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kadri itakavyoweza na inamtakia kila la heri, huku ikiamini hatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa RT waliomuamini wakamchagua kushika wadhifa huo.

Pia Taswa inawapongeza viongozi wote wa RT walioingia madarakani Jumapili, ikiamini watakuwa chachu ya mafanikio ya riadha hapa nchini.

VODACOM YAZINDUA PROMOSHENI YA WIKIENDI YA WAJANJA


Wateja wa Vodacom kupata nyongeza ya  asilimia 50 kila wanapoongeza muda wa maongezi kuanzia  Tsh 1000
·        Nyongeza hii inaweza kutumika kwa ajili ya  a kutuma ujumbe mfupi SMS, kupiga simu au kuperuzi internet.
·        Kujua Salio la nyongeza mteja anaweza kubonyeza *102*02#

 Kampuni ya mawasiliano inayoongoza Tanzania, Vodacom leo imezindua promosheni kwa ajili ya wateja wake ambapo kuanzia leo hadi mwisho wa wikiendi watapata nyongeza ya asilimia hamsini kila mara wanapoongeza muda wa maongezi wa kuanzia Tsh1000.
Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema promosheni hii imetokana na kuguswa kwa wateja na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya WAJANJA ambayo imeonyesha kupendwa na kutumiwa sana na wateja wao kwenye matumizi ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi SMS na kuperuzi kwenye internet.
“Tunajivunia tunapowaona wateja wetu wakifurahi na kuendelea kutumia huduma zetu na hii promosheni inanuia kuwapa thamani zaidi yapesa zao wakati huu wa wikiendi ikiwa ni fursa kubwa kwa familia kufanya shughuli kadha wa kadha,” alisema Bwana Meza.
Nyongeza hii ya salio ya asilimia 50 inaweza kutumika kwa kutuma ujumbe mfupi, kupiga simu na kuperuzi internet kupitia simu za mkononi na pia promosheni hii ni kwa ajili ya  wateja wanaotumia Mpesa kununua muda wa maongezi.
Wateja pia wanaweza kuangalia salio la nyongeza hii kwa kubonyeza *102*02#

TAIFA STARS, MALAWI KUMENYANA KESHO UWANJANI WA TAIFA DAR ES SALAAM

Timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) zinapambana kesho (Mei 26 mwaka huu) katika mechi ya kirafiki itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
Makocha wa timu zote mbili, Kim Poulsen wa Taifa Stars na Kinnah Phiri wa The Flames wamezungumzia umuhimu wa mechi hiyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo (Mei 25 mwaka huu) ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 
Kim ambaye hiyo itakuwa mechi yake ya kwanza tangu asaini mkataba wa kuinoa Stars, amesema baada ya mazoezi ya siku kumi hicho ndicho kipimo chake cha kwanza na cha mwisho kabla ya kucheza na Ivory Coast kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayofanyika ugenini Juni 2 mwaka huu.
 
“Wachezaji wangu wamekuwa wakipokea mafunzo vizuri ingawa Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu hatakuwepo kwa vile ni majeruhi. Bila shaka baada ya mazoezi ni lazima ujipime, hivyo mechi hii ni muhimu kwangu ukizingatia kuwa kwenye ubora wa viwango vya FIFA, Malawi wako juu yetu,” amesema Kim.
 
Naye Phiri ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Malawi amesema awali aliombwa mechi na Misri, lakini akaamua kucheza na Taifa Stars kwa vile anaamini kitakuwa kipimo kizuri kwake kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Kenya itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Nairobi.
 
“Nimekuja na wachezaji 20 ambapo nusu yao wanacheza mpira wa kulipwa nje ya Malawi, wengi wakiwa Afrika Kusini lakini wapo pia kutoka Msumbiji na mmoja anacheza Hispania katika timu ya vijana ya Atletico Madrid. Tumejianda si kwa mechi hii tu, bali pia dhidi ya Kenya na baadaye Nigeria ambao tutacheza nao numbani Juni 9 mwaka huu,” amesema Phiri ambaye kwenye benchi lake la ufundi anasaidiwa na Young Chimodzi.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A inayochukua watazamaji 748 tu itakuwa sh. 20,000.

TFF NA HALI YA MAMBO NDANI KLABU YA YANGA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Bw. Loyd Nchunga.
 
Kwa vile wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji ya Yanga akiwemo Mwenyekiti wa kamati hiyo Lloyd Nchunga wamejiuzulu, Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka mwongozo juu ya hilo.
 
Kwa kuzingatia hilo, TFF imepeleka suala hilo kwa kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ili itoe maoni yake kisheria ya nini kinafanyike kuhakikisha Yanga inaendelea na shughuli zake kama kawaida.
 
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana leo jioni kushughulikia suala hilo na baadaye Kamati ya Uchaguzi ya Yanga pamoja na Kamati ya Uchaguzi ya TFF zitapewa maelekezo ya kufanya kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

Rais Kikwete apokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe uliowasilishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Bwana Sidney Sekeremayi ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Bwana Sidney Sekeremayi ambaye ni mjumbe maalumu wa Rais Robert Mugabe ikulu mjini Dodoma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MJINI BOTSWANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib
Bilal na Mama Asha Bilal, wakiingi kwenye ukumbi wa tafrija ya chakula
cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana Lt General Seretse Khama
kwa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa siku
mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika Nchini Gaborone
Botswana.
(PICHA NA VPO)
Makamu wa Raisa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal kushoto, Rais wa Liberia Mhe. Ellen Jonson na Rais wa Botswana
Mhe. Lt General Seretse Khama wakiwa kwenye tafrija ya chakula cha
jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana kwa Viongozi wakuu wa Afrika
waliohudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara
la Afrika jana jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na mkewe Mama Asha Bilal wakiwa kwenye tafrija iliyoandaliwa na
Rais wa Botswana Lt. General Seretse Khama kwa ajili ya viongozi wakuu
wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano kuhusu maendeleo endelevu kwa
Bara la Afrika
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akizungumza na baadhi ya
wajumbe waliohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu
maendeleo endelevu kwa bara la Afrika unaoendelea mjini Gaborone
Botswana
Wasanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni nchini Botswana wakitumbuiza
kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo endelevu ya
Bara la Afrika unaoendelea leo mjini Gaborone Botswana.

TANZANIA BEGA KWA BEGA NA UNDP KUJENGA AFRIKA YENYE UHAKIKA WA CHAKULA.


Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou akizungumza kwa niaba ya UNDP kuhusiana na kuzinduliwa kwa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 ambapo amesema huu sasa ni wakati kwa nchi za Afrika haswa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kujenga mazingira ya kuelekea mustakabali wenye uhakika wa chakula.

Mgeni rasmi Mh. Janet Mbene na Dk. Alberic Kacou wakionyesha Ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi leo.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou (kulia) wakifuatilia maoni ya Uchambuzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kutoka kwa Maprofesa wa Vyuo vikuu nchini.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakipitia Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kuelekea kwenye Mustakabali wenye uhakika wa Chakula kwa nchi za Afrika iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Na.Mwandishi wetu.

Bara la Afrika ikiwemo Tanzania limeshakumbwa na matukio kadhaa ya kukabiliwa na uhaba wa chakula, uliokwenda sambamba na matukio ya watu wengi kupoteza maisha haswa Kusini mwa jangwa la Sahara na Ukanda wa Sahel eneo la Afrika Magharibi.

Hali hiyo imekuwa moja ya changamoto kubwa inazozikabili serikali za mataifa hayo ambapo yanapambana ili kuitatua ili kila mwananchi barani Afrika aweze kufurahia kukua kwa uchumi.

Akitoa hotuba wakati akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) amesema kwa muda mrefu sura ya eneo la nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara imekuwa ni ya njaa ya kukithiri, ambapo zaidi ya mtu mmoja katika kila waafrika wane wana tatizo la upungufu wa lishe.

Amesema Ripoti hiyo inaonyesha kuwa pamoja na ukweli kwamba baadhi ya nchi zinazokuwa kwa kasi kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ziko Afrika, lakini bado hali ya maisha ya waafrika ni duni.

Awali Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou alisema bara la Afrika limejaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa kwa kukuzia mazao, lakini swali la kujiuliza ni kwanini bado kuna uhaba wa chakula.

Hata hivyo Dk. Kacou ametoa matumaini kuwa bara la Afrika bado lina uwezo wa kujijengea mazingira ya kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa kipindi kijacho.

Ripoti hii ya Kwanza ya Maendeleo ya Afrika inasema kwamba ongezeko endelevu katika uzalishaji kwenye kilimo kunalinda haki ya chakula na uwezo wa watu kupata chakula.

SIMBA ITAKAVYOSHEREHEKEA USHINDI DAR LIVE JUMAPILI

Makamu Mwenyekiti wa Simba SC Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, akizungumzia maandalizi ya sherehe hiyo.
 
KLABU ya mpira wa miguu ya Simba leo imezungumzia juu ya sherehe ya ubingwa wa kombe la Tanzania bara 2012 walilolitwaa hivikaribuni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema maandalizi ya sherehe hiyo tayari yameshakamilika na kinachosubiriwa hadi sasa ni siku husika ambayo ni Jumapili ya wiki hii, tarehe 27.
Alisema wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo watatakiwa siku ya Jumapili hii kukusanyika makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi, asubuhi tayari kwa safari ya kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam, ambapo sherehe hizo zitafanyika.
Mmoja wa waratibu wa sherehe hiyo wa Dar Live, Luqman Maloto (kulia), akielezea jinsi walivyojiandaa kufanikisha sherehe hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Nyange katika ukumbi wa klabu hiyo uliopo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar.

Redds Miss IFM kulindima CINE Club jumamosi

Mkurugenzi wa kampuni ya LINO Agency ambao ni waandaaji wa Shindano la Redds Miss Tz Hashimu Lundenga katikati akizungungumza na warembo wanashiriki shindano la Redds Miss IFM juu ya vigezo na taratibu za kumpata mshindi kwenye fainali zinazotarajia kufanyika SINE Club jumamosi ya juma hili,Kulia ni Mwandaaji wa Redds Miss Dar Inter College na kushoto Ni afisa toka kamati ya Redds Miss Tanzania.
Msanii wa musiki wa Kizazi kipya Diyamondi akielezea namna alivyojiandaa kufanya unyesho kubwa kwenye fainali ya Redds Miss IFM jumamosi ya juma hili kwenye Ufukwe wa CINE CLUB kulia ni warembo wa shindano hilo Rosa Damazo ,Waliosimama ni Teressia Issaya kulia na Caroline Dandu kushoto na Mwalimu wao Estar Wilsoni
 

Thursday, May 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AMWAKILISHA RAIS KATIKA MKUTANO WA MAENDELEO ENDELEVU AFRIKA JIJINI GABOFRONE, BOTSWANA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dkt. Mohammed Gharib Bilal amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Maendeleo Endelevu Afrika unaolenga katika kujumuisha thamani ya Rasilimali Asilia katika kupima maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Afrika.
Katika mkutano huo, Tanzania imeunga mkono kuanzishwa kwa mfumo wa kujumuisha thamani ya raslimali asilia ambao utahusishwa kwenye tathmini ya pato la taifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na  vijavyo.
Makamu wa Rais alisema wakati akihutubia mkutano huo leo Alhamis Mei 24, 2012 kuwa, mchango wa rasilimali asilia zina nafasi kubwa katika kuchangia katika pato la taifa lakini ili mchango wake utambulike, nchi zinahitajika kuwa na utaratibu wa kuzifanyia tathmini hasa kuhusu matumizi yake na faida zake katika uchumi huku pia athari zake zikitazamwa hasa zile zinazotokana na kupoteza uhalisia wa mazingira ama kuharibu mazingira ya nchi.
“Ni imani ya serikali ya Tanzania kuwa mpango huu utasaidia kutoa nafasi ya nchi kujikagua hasa kwa kuzingatia rasilimali zinazotumika na faida inayopatikana. Tena mpango huu utatoa nafasi kwa nchi kujiuliza kama matumizi ya rasilimali zake yanalenga kutambua faida ya sasa na siku zijazo ili kuhakikisha kuwa mazingira yanabakia kuwa salama kwa ajili ya vizazi vijavyo,” anasema Mheshimiwa Makamu wa Rais Katika hotuba yake.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU MAENDELEO NDANI YA BARA LA AFRIKA GABORONE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi pamoja na wawakilishi  kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa Maendeleo Endelevu katika Bara la Afrika.(PICHA NA VPO)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais wa Liberia Bibi Ellen Johnson Sirleaf kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo Endelevu Barani Afrika leo mjini Gaborone
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akihutubia kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo Endelevu katika Bara la Afrika leo mjini Gaborone.

WASHINDI WENGINE WASHINDA ZAWADI NONO ZA SBL, MMOJA ACHOMOKA NA GARI MPYA, WA PILI PIKIPIKI MPYA,HUKU WA TATU AKIIBUKA NA JENERETA MPYA KABISA

 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumpata mshindi wa gari aina ya Ford Figo, Pikipiki na Genereta katika droo ya mwezi ya "Vumbua Dhahabu chini ya Kizibo" inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti, kwenye makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbaym kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Diageo kanda ya Afrika Bi. Cristina Diezhandino na kushoto ni aBakari Maggid Afisa msimamizi wa michezo ya Kubahatisha.
 Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Diageo kanda ya Afrika Bi. Cristina Diezhandino akibonyeza kitufe kwenye kompyua ili kuchezesha bahati nasibu kwa ajili ya kupata mshindi wa gari aina ya Ford Figo leo.
Kampuni ya bia ya Serengeti imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali hapa nchini kukabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali wa promosheni  kubwa na ya kipekee kabisa kutokea hapa nchini Tanzania  ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ambayo ama kwa hakika inashuhudia watanzania wengi wakinufaika na kupiga hatua mbele kimaisha.
Asubuhi ya leo droo ya nne katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ambapo kwa mara ya kwanza wadau,washiriki na watanzania wote wameshuhudia mmoja wa washindi wa droo ya nne akiibuka na gari mpya aina FORD FIGO huku mwenzake akichomoka na Jenereta mpya.
 Bi. Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti ( SBL) alikuwa na haya ya kusema“  najisikia furaha sana kuona kila tunapochezesha droo yetu tunapata washindi ambao mpaka sasa tumeshawapata washindi watatu wa jenereta,mshindi mmoja wa pikipiki na washindi wawili wa Bajaj ambapo tayari tumewakabidhi zawadi zao,”alisema Mapunda
“ Bado tunaendelea kuwahamasisha wateja wetu na watanzania wote wenye umri unaruhusu kshiriki katika promosheni hii waendelee kushiriki bila kukata tamaa kwani bado kuna zawadi nyingi sana hadi zifikie milioni 780 kwa zawadi pekeyake  na milioni 380 pesa taslim zinaendelea kushindaniwa.
Washindi wetu katika droo ya nne ni Rogers Kavishe kutoka mkoa wa Kilimanjaro ambaye amejishindia jenereta  kupitia bia ya Serengeti Lager, wa pili ni bw. Oktavian Changula kutoka mkoani Iringa ambaye  amejinyakulia pikipiki mpya kupitia bia ya Tusker lager  wa tatu ni  bw.Isack Juvenari kutoka mkoa wa Morogoro  ambaye amejishindia gari mpya kabisa aina ya FORD FIGO
Kwa upande wake meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Peter Chonjo aliwapongeza washindi wote katika droo hiyo na kuwataka watanzania waendelee kunywa bia za Serengeti ambazo zimeainishwa katika promosheni hiyo ili kuendelea kushinda na hatimaye kupiga hatua katika maisha yao.
Kupitia mawasiliano kwa simu ya mezani mshindi huyo wa gari mpya hakuweza kujieleza kwa mara moja kutoka na hali halisi alioonekana nayo baada ya kupata taarifa ya kushinda gari alipagawa na kupelekea mawasiliano hayo kuyumba kwa muda lakini baadaye aliweza kutulia na kujieleza vizuri.Gari hilo litakabidhiwa kwa mshindi huyo siku chache zijazo.