TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, September 19, 2013

SIMBA YAFANYA MAUAJI TAIFA , YANGA YABANWA MBAVU TENA



Na Elizabeth Mayemba

TIMU ya Simba, jana ilifanya mauaji baada ya kuwafunga Mgambo Shooting mabao 6-0 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Katika mechi hiyo, Simba ilianza kusherehekea bao lake la kwanza kwa dakika ya nne lililofungwa na Amis Tambwe kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi safi iliyochongwa na beki Idrisa Rashid ‘Baba Ubaya’.

Dakika ya 12 mshambuliaji wa Simba, Tambwe alikosabao baada ya kuubabatiza mpira uliokuwa unaokolewa na mabeki wa Mgambo Shooting, lakini shuti lake likatoka nje ya lango.Betram Mombeki wa Simba alikosa bao dakika ya 30 baada ya kuunasa mpira na kuachia shuti kali lililotoka nje ya lango.Simba ilipata bao la pili dakika ya 32 kupitia kwa Haroun Chanongo, ambaye alifunga bao hilo baada ya kipa kutoka ndani ya lango lake na kuupachika mpira kiulaini.

Tambwe aliendelea kuwaumiza Mgambo Shooting, baada ya kuifungia Simba bao la tatu dakika ya 41 baada ya kuunasa mpira uliotemwa na kipa wa Mgambo, Kulwa Manzi ambaye alitema shuti kali la Chanongo.Dakika ya 44 Tambwe aliipatia tena Simba bao la nne ikiwa ni bao lake la tatu katika mechi hiyo, baada ya kuunganisha krosi ya Amri Kiemba.

Simba ilitawala mpira kwa kiasi kikubwa huku kipa wa Simba, Abel Dhaira kuwa likizo Mgambo walizinduka dakika ya 45 na kufanya shambulizi la nguvu, ambapo nusura ingepata bao lakini Novat Lufunga akiwa nje ya 18 aliachia shuti kali lililopaa juu ya lango.Kipindi cha pili Mgambo waliingia kwa nguvu na kuliandama lango la Simba ambapo dakika ya 58, Salum Kipanga alikosa bao la wazi baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa Dhaira na mpira kuwahiwa na mabeki walioutoa nje ya uwanja.

Dakika ya 64, Simba ilipata bao la tano baada ya beki wa Mgambo Bakari Mtama kujifunga akimalizia shuti lililopigwa na Chonongo akiwa katika harakati za kuokoa mpira.Hamis Tambwe aliipatia Simba bao la sita dakika ya 18 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Mgambo kuunawa mpira akiwa katika eneo la hatari.

Naye Hamis Miraji anaripoti kutoka Mbeya kuwa, katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Sokoine Yanga ilibanwa mbavu na Prisons baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1Mechi hiyo ilianza kwa timu zote kukamiana ambapo dakika ya nane, Simon Msuva nusura aifungie Yanga bao baada ya kuachia shuti
kali lililotoka nje kidogo ya lango akiwa nje ya 18.
Dakika ya 19 Six Ally wa Prisons akiwa nje ya 18 naye aliachia shuti kali ambalo hata hivyo lilitoka nje ya lango.Jerry Tegete aliipatia Yanga bao dakika ya 41 kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Mbuyu Twite.Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kuingia na uchu wa mabao ambapo dakika ya 70, Didier Kavumbagu alipiga shuti lililotoka nje ya lango.Prisons ilisawazisha bao hilo dakika ya 78 kupitia kwa Ibrahim Isaka, baada ya kuunganisha kona iliyochongwa na Omega Seme.

Naye Speciroza Joseph anaripoti kuwa Azam FC imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Ashanti katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamanzi, Dar es Salaam. Kutoka Uwanja wa Mabatini, Chalinze Omari Mngindo anaripoti kuwa Ruvu Shooting imetoka kifua mbele kwa kuwafunga ndugu zao JKT Ruvu bao 1-0.Nako katika Uwanja wa Manungu, Morogoro wenyeji Mtibwa Sugar imelazimishwa suluhu na Mbeya City

MWEI: MIKOPO BILA RIBA


Meneja wa Vodacom Foundation Kitengo cha MWEI, Grace Lyon akimshuhudia mkazi wa Kunduchi, Beatrice Shayo (kushoto) wakati akisaini fomu kabla ya kupokea mkopo kupitia mradi huo. Shayo ni mmoja wa wanawake wajasiriamali zaidi ya 100 kutoka Kunduchi waliopokea jumla ya sh. milioni 18 kupitia mradi huo ili kuanzisha biashara. Zaidi ya wanawake 2,800 wameshapata mikopo hiyo isiyo na
riba

WATANZANIA KUANZA KUNUFAIKA NA MAKAA

picha_mchoro_wa_kiwanda_mchuchuma_8ab28.jpg
Mchoro wa kiwanda mchuchuma
DAR ES SALAAM: Tanzania inatarajia kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa chuma barani Afrika kwa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka mara uzalishaji wa madini hayo utakapoanza mwaka 2018/19 chini ya kampuni ya Tanzania China Mineral Resources Limited (TCIMRL), ambayo ni kampuni ya ubia kati ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Shirika la Sichuan Hongda Group (SHG) ya China.(P.T)
Ripoti ya utafiti wa TCIMRL ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kuanzishwa mgodi na kiwanda cha chuma katika eneo la Liganga wilayani Ludewa, iliyofanywa katika eneo la kilomita za mraba 10 pekee inabainisha kuwapo kwa tani milioni 219 za chuma ambazo zitadumu kwa zaidi ya miaka 70 kwa uchimbaji wa juu (open cast mining). Eneo lililobakia lina kilomita za mraba 156 na kukadiriwa kuwa na rasilimali kubwa zaidi.

Tanzania itashika nafasi ya nne ikizifuatia nchi za Afrika Kusini itakayozalisha bidhaa za chuma tani milioni 8.5 kwa mwaka, Misri tani milioni 8.0 na Libya tani milioni 2.0 kwa mwaka. Chuma kinachozalishwa duniani ni takribani tani bilioni 1.55 kwa mwaka, mzalishaji mkubwa ikiwa ni China inayotoa tani milioni 711 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 46 ya chuma chote kinachozalishwa duniani. Mbali na chuma, madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni Titanium tani 175,400 kwa mwaka na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka.

Mradi huu ni moja ya miradi miwili iliyopo katika mkataba kati ya NDC na SHG uliotiwa saini Septemba 21, 2011 ya uanzishwaji wa mgodi wa makaa ya mawe na ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa megawati 600 katika eneo la Mchuchuma pamoja na ujenzi wa msongo wa umeme wa kilovoti 220 kati ya Mchumchuma na Liganga; na uanzishwaji wa mgodi wa chuma na ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua chuma na kiwanda cha kuzalisha bidhaa za chuma, pamoja na ujenzi wa barabara kati ya Mchuchuma na Liganga.

Kiasi cha Makaa ya mawe kulingana na utafiti wa TCIMRL katika eneo la kilomita za mraba 30 ni tani milioni 370 ambazo zinaweza kuchimbwa kwa miaka zaidi ya 100. Kkuna eneo la ziada la kilomita za mraba 110 ambalo linakadiriwa kuwa na rasilimali zaidi ya makaa yam awe. Miradi hii miwili itakayogharimu Dola za Kimarekani bilioni tatu (USD 3.0bil) inatarajiwa kuliingizia taifa mapato ya Dola bilioni 1.7 kwa mwaka itakapoanza uzalishaji kamili mwaka 2018/19, mapato ambayo yatatokana na uuzaji wa umeme wa megawati 600, uuzaji wa makaa ya mawe kwa nishati ya viwandani, chuma, titanium, vanadium na itatoa ajira ya moja kwa moja watanzania 6,000 na 35,000 kwa zisizo za moja kwa moja.

Miradi hii hivi sasa ipo katika awamu ya kwanza ambayo ilikuwa inahusisha utafiti na maandalizi kabla ya Mei mwakani kuingia katika awamu ya ujenzi wa migodi na viwanda katika maeneo ya Mchuchuma na Liganga. Mradi huu wa ubia na mwekezaji wa kimataifa unakwenda sambamba na mradi mwingine katika eneo hilo la Ludewa uliotiwa saini Septemba 2, 2009 na kampuni ya wazawa ya M.M. Steel Resources Public Limited Company (MMSR PLC). 
Mradi huu unalenga kuzalisha chuma ghafi kwa kutumia chuma cha Liganga Matitu na makaa ya mawe ya Katewaka. Kampuni ya ubia iliyoanzishwa ni Maganga Matitu Resource Development Limited (MMRDL). Uwekezaji utakuwa ni dola za Kimarekani milioni 150 na unatazamiwa kuingiza mapato ya dola milioni 183.3 kwa mwaka. Chuma ghafi hiki kitatumika kuwa malighafi kwa viwanda vingine vilivyo ndani na nje ya nchi, hivyo kuwezesha uzalishaji wa chuma imara kulikoni hiki cha sasa kitokanacho na scrap ambacho ni hafifu. Lakini pia hujuma kwa miundombinu yetu kwa ajili ya scrap utakoma.

Imetolewa na: Abel Ngapemba
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika
angapemba@ndc.go.tz, 022 211 1490 0784 273 588/0715
18 Septemba 2013

AIRTEL Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wamezindua rasmi huduma ya kufanya malipo ya ada za leseni za magari

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money pichani kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs.Diana Masalla (wa pili kushoto) akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money wakishuhudia kulia ni meneja kitengo cha Airtel money John Ndunguru , mwisho kushoto ni mwakilishi wa max malipo Tumsifu Lema.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs.Diana Masalla (wa pili kushoto) akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money.

Airtel Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato  Tanzania TRA wamezindua rasmi huduma ya kufanya malipo ya ada za leseni za magari kupitia huduma ya Airtel money. Huduma hii inapatikana bure kwa wateja wote wa Airtel nchi nzima. Hii inawawezesha watumiaji wa huduma hii kulipia leseni ya magari yao wakiwa ofisini au majumbani mwao kwa urahisi zaidi ambapo kwa sasa ni BURE.

Adriana Lyamba, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel amesema " huduma ya kulipia leseni ya magari kupitia Airtel money imeleta unafuu kwa wateja watakaotaka kulipia leseni za magari. Huu ni mwendelezo wa mapinduzi ya huduma za kifedha kupitia huduma ya Airtel money inayomuhakikishia mteja uharaka, unafuu, usalama na urahisi zaidi katika kulipia huduma mbalimbali. Tunaamini huduma hii ya kulipia leseni za magari kupitia Airtel money kutaleta ufanisi na kuendeleza juhudi za serikali katika ukusanyaji wa kodi.

Tunaahidi kuendelea kuleta suluhisho katika huduma za malipo mbalimbali na kuwahakikishia wateja wetu urahisi, usalama na ufanisi zaidi kupitia Airtel Money."

Sasa tumewawezesha wateja wote wa Airtel kulipia leseni za magari bila kuwa na haja ya kutembelea ofisi za TRA kufanya malipo. Wateja watatakiwa kwenda kuchukua leseni/stika zao pale malipo yatakapofanyika na leseni/stika zao kuwa tayari.

Akiongea kuhusu huduma ya malipo ya ada za leseni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla alisema" huduma hii mpya inahusisha malipo ya ada za lesseni za magari, ada za uamisho wa magari pamoja na malipo mengine ya ada za usajili wa magari. Huduma hii itawezesha ukusanyaji wa malipo ya ada / kodi zifanyike kwa njia rahisi na nafuu. Unaweza kupata kiasi cha kulipia ada unayotakiwa kulipia kisha ukalipia hapohapo ndani ya sekunde chache kupitia huduma ya Airtel money.

Ulipaji huu unaenda sambamba na kauli mbiu ya TRA ya Urahisi, Uhiari na Uboreshaji Endelevu Akiongea juu ya namna ya ulipiaji ada Meneja wa kitengo cha Airtel money John Ndunguru alisema" huduma hii inapatikana kwa wateja wa malipo ya awali na ya mwenzi.

Aliongeza kwa kusema ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hii, Airtel imeweza kuiweka kwenye MENU ya Airtel Money "TRAMAGARI" ili kuweza kurahisisha ulipaji wa ada na kuiwezesa serikali kukusanya ada kwa gharama nafuu zaidi".

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga alisema "Ninawapongeza sana kampuni ya Airtel Kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kurahisisha ukusanyaji wa kodi hii ya Ada za magari maarufu kama Road License. Hi ni huduma nzuri inayosaidia watanzania kuokoa muda wao pale wanapoweza kutumia simu zao kupitia mtandao wa Airtel kulipia Ada ya magari yao kila mwaka bila usumbufu."

Kwa urahisi huu inatusaidia sana kuokoa muda ambao ungepotea kukaa kwenye foleni ya malipo na badala yake muda tunaookoa tutautumia katika shughuli nyingine za kiuchumi.

Naomba niwakumbushe kuwa wiki ya usalama barabarani itaanza wiki ijayo tarehe 23.9.2013 hivyo mambo yote ya ukaguzi wa stika za ada za magari yaani (Road Licence) pamoja na Stika za usalama barabarani na ukaguzi wa vyombo vyote vya moto utaenda sambamba, hivyo ninawakumbusha watumiaji wote wa vyombo vyote vya moto kufuata sheria zote zilizowekwa ili kuepuka adhabu ya kulipa faini.

Huduma ya Airtel money inawawezesha wateja kutumia simu zao za mkononi katika huduma za kifedha zikiwemo kulipa bill ya maji DAWASCO, kulipia Luku TANESCO malipo ya DSTV, kulipia visa ya USA na sasa ada za lesseni ya magari. Airtel money ni huduma rahisi na salama inayotoa huduma za mobile benki na za malipo mbalimbali.

KINANA AMPA RUNGU MPINA KUWABANA MAWAZIRI

 Na Mwandishi Wetu, Simiyu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amewataka wabunge wa chama hicho kuwahimiza mawaziri ili waweze kutimiza wajibu wao wa kutumikia wananchi tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wao wanafanya kazi kwa mazoea Kinana alisema kasi ya kufuatilia utendaji kazi wa mawaziri inayofanywa na Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina ni ya kuridhisha na kwamba chama hicho kinaheshimu msimamo wa mbunge huyo katika kuisimamia kikamilifu Serikali ili iweze kutimiza malengo ya kuwaletea maisha bora Watanzania. 

Alisema Mpina ni mbunge hodari na jasiri aliyemstari wa mbele kuwatetea wananchi na kuhoji uwajibikaji wa Serikali awapo bungeni, hivyo chama hicho kitaendelea kuthamini mchango wake kwani kwa kiasi kikubwa unasaidia kuharakisha utendaji wa Serikali. "Mbunge wenu ni hodari, sisi chama tunamheshimu, ni mchapakazi, mtetezi wenu na tunaamini mtaendelea kumchagua katika Uchaguzi Mkuu ujao,"alisema Kinana. Alisema matatizo mengi ya wananchi yanashindwa kutatuliwa kutokana na Mawaziri kukaa maofisini bila kufika katika maeneo husika na kwamba ufuatiliaji wa Mbunge huyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kuwaamsha ili waweze kuchapa kazi inayotegemewa na wananchi.

Pia alisifu uwajibikaji wa Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini katika kufuatilia kero za wananchi na kuwataka viongozi wengine kuacha kusubiri hadi madhara yatokee ndipo wakimbilie kwenye maeneo hayo kutafuta suluhu. Kwa upande wake Mpina alisema mapokezi makubwa aliyopata Katibu Mkuu huyo wa CCM ni ishara tosha kuwa Serikali imekuwa ikiwajibika kwa wananchi hasa katika jimbo hilo kwa kufanikisha kutelekezwa kwa ahadi za Rais Jakaya Kikwete alizotoa kwenye kampeni ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Mongo-obakima ambapo wananchi walipoteza maisha kwa kuliwa na mamba na viboko pamoja na kusombwa na maji. 

Katika mkutano huo wananchi hao walimuomba Katibu Mkuu huyo wa CCM kuwatafutia suluhu ya tatizo la malisho ya mifugo hususan kwa wananchi wanaoishi kando ya pori la akiba la Maswa kutokana na baadhi ya viongozi kuwabambikia kesi na kuwakamua fedha zao kupitia mgogoro huo wa malisho ya mifugo. Kufuatia ombi hilo Kinana aliwaagiza Mawaziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kufika katika eneo hilo na kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo.

JK APIGILIA MSUMARI WANASIASA



RAIS Jakaya Kikwete, ameshangazwa na kiwango cha uongo wa baadhi ya wanasiasa na hasa madai kwamba aliteua wajumbe wa Tume ya Katiba bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau mbalimbali waliopendekeza majina hayo.
 
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa bado anaendelea kuamini kuwa mchakato wa Katiba Mpya utafikia mwisho wake mwakani, 2014, na hivyo kuiwezesha Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 chini ya Katiba Mpya.

Rais Kikwete aliyasema hayo Jumatatu, wiki hii, mjini San Rafael, California wakati alipokutana na kuzungumza na Jumuiya ya Watanzania waishio Jimbo la California, nchini Marekani, wakati alipoanza ziara yake ya siku mbili katika Jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini Marekani.

Vilevile, Rais Kikwete alisema hana tatizo na watu wanaopinga sera za Serikali au hata kumpinga yeye binafsi bali tatizo lake ni wanasiasa na wanaharakati wanaochochea ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.  "Watu wote niliowateua walipendekezwa na wadau mbali mbali zikiwamo taasisi za dini. Yule Mama Maria Kashonda alipendekezwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mama Mwantumu Malale alipendekezwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA). Kila kundi ambalo lilipendekeza watu limepata mjumbe katika Tume hiyo wakiwemo walemavu ambao naambiwa nimewasahau," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Hivi nyinyi wanasiasa wenzangu mkikosa hoja mnaongopa hata kwa vitu ambavyo viko wazi kabisa. Tulikubaliana kuwa Rais angefanya uteuzi wa wajumbe wa Tume baada ya kupokea mapendekezo ya wadau mbali mbali na katika mchakato ulioendeshwa kwa uwazi kabisa. "Hivyo, ndiyo ilivyofanyika. Sasa uongo wa nini? Kama hakuna hoja ni kwamba hakuna tu na wala uongo hautasaidia." Kuhusu mjadala wa karibuni kuhusu kama Rais awe na madaraka ya kuteua wajumbe 166 wa nyongeza ili kuingia katika Bunge la Katiba kujadili Rasimu ya Katiba Mpya, Rais Kikwete amesema kuwa yeye hana tabu kama itabidi ateue basi atateua, lakini kama si lazima yeye hatafanya hivyo. "Mimi sina taabu, wakisema niteue basi nitateua. Wakisema nisiteue vilevile sina taabu, isitoshe hiyo itakuwa inanipunguzia mzigo na kazi. Ile kazi yenyewe ya kuteua Wajumbe wa Tume ya Katiba ilikuwa siyo rahisi

WABUNGE NIGERIA WATWANGANA MAKONDE, ABUJA, Nigeria



WABUNGE nchini Nigeria wamerushiana makonde baada ya kundi lililojitenga kutoka chama tawala cha PDP kujaribu kuhutubia  Bunge hilo la chini lilifanya vikao baada ya mapumziko ya wiki saba - ambapo kundi jipya la PDP liliundwa. Kwa mujibu wa BBC, Wabunge ambao ni watiifu kwa Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria walianza kupiga kelele na kuzomea, ambapo kitendo hicho kiliwaudhi wapinzani wao na ndipo mtafaruku ulipoanza.

Kundi hilo lililojitenga linapinga Rais Jonathan kuwania kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa 2015. Bw. Jonathan bado hajasema kama atagombea, lakini baadhi ya washirika wake, akiwemo mkewe, wameanza kumfanyia kampeni.Kulingana na BBC, Mbunge mmoja alionekana akimchania shati mwenzake katika hali ya vurugu ndani ya Bunge la Wawakilishi la Nigeria mjini Abuja.  Ugomvi huo ulidumu kwa dakika 10 huku Wabunge wakitwangana makonde.Picha za televisheni z i l i o n e s h a Mb u n g e mwanamke akimtia kidole mwenzake usoni. Mbunge mwingine alionekana akichukua kiti katika kujaribu kumpiga mtungasheria mwenzake, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Ufaransa, AFP.

C h a m a c h a P D P kimekuwa kikishinda chaguzi tangu kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999, kwa maana hiyo mgombea urais wa chama hicho atakuwa katika nafasi nzuri kuwa kiongozi atakayefuata wa Nigeria.Bw. Jonathan amekuwa rais tangu 2010, wakati mtangulizi wake alipokufa na akapandishwa kutoka makamu wa rais hadi kuwa rais.

SHAHIDI KESI YA MRAMBA AMTWISHA ZIGO BALALI

 Na Rehema Mohamed

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Masoko na Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kesisia Mbatia, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa benki hiyo ilihusika katika mchakato mzima wa kumtafuta mzabuni wa ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini ambaye ni Kampuni ya M/S Alex Stewart ya nchini Uingereza. Mbatia alieleza hayo jana mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jopo la Mahakimu wawili wakiongozwa na Jaji John Utamwa, waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba na wenzake.


Mbatia alisema kuwa katika mchakato wa kumtafuta mzabuni huyo, aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Daud Balali, alimteua yeye kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wajumbe watano wa kutafuta mzabuni huyo. Alidai kuwa, awali jumla ya wazabuni 21 walijitokeza kutaka kufanya kazi ya ukaguzi huo na baadaye walifanya mchujo na kubaki na wazabuni watano, ambapo kati ya hao ni Kampuni ya M/S Alex Stewart ndiyo ilishinda. 

Alisema kampuni hiyo ilishinda zabuni hiyo kwa makubaliano ya kulipwa asilimia 1.9 ya dhahabu atakayokagua na kwamba asingehusika na malipo yoyote ya kodi za hapa nchini. Alidai kuwa baada ya kushinda dhabuni hiyo,BoT iliandaa rasimu ya mkataba kati ya Serikali na M/S Alex Stewart ambapo Balali alimwalika kuja nchini kwa ajili ya kusaini mkataba huo ambapo kwa upande wa Tanzania Balali ndiye aliyesaini. Aliongeza kuwa mkataba huo ulikuwa wa kufanya kazi miaka miwili na baada ya muda huo kumalizika, Balali ilimwandikia barua M/S Alex Stewart kuongeza muda wa miaka miwili mingine ya kufanya kazi hiyo. 

"Kampuni ya M/S Alex Stewart iliongezewa mkataba Machi 2005, kipindi hicho Kamishna wa Madini ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati na hatukuwa na kazi kubwa kama awali kwani barua aliyoandikiwa na Balali ilimaliza kila kitu," alidai Mbatia. Alidai kuwa walichojadili wao katika mkataba wa pili ni kuitaka kampuni hiyo kupanua zaidi kazi yake na kwamba hakumbuki kitu ambacho kiliongezwa na kama Mramba alihusika kwa namna yoyote katika kamati ya kutafuta mzabuni huyo. 

Mbali na Mramba wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja. Katika kesi hiyo ambayo itaendelea kusikilizwa leo, Mramba na wenzake wanashtakiwa, wakidaiwa kwamba kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14, 2004, jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya Sh.bilioni 11.7.

MSWADA WA KATIBA SASA KAA LA MOTO

Na Goodluck Hongo


MSWADA wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba umezidi kugeuka kaa la moto kutokana na kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali wanaomtaka Rais Jakaya Kikwete, asisaini mswada huo ili kuwa sheria kwa kile kinachodaiwa kuwa ulipitishwa kiujanjaujanja.   Ili kuhakikisha muswada huo hausainiwi, vyama vitatu vilivyoungana kupinga mchakato wa Katiba Mpya vya CHADEMA, NCCR-Mageuzi na CUF vimezidi kutafuta nguvu ya kuungwa mkono kwa kukutana na makundi mbalimbali ndani ya jamii kwa lengo la kuunganisha sauti ili kukwamisha mswada huo. 

Jana, viongozi wa vyama hivyo, Freeman Mbowe (CHADEMA), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi) walikutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVIWATA) na kuwaeleza kasoro zilizoko kwenye mswada huo kwa lengo la kutaka kuungwa mkono.

Mazungumzo ya viongozi hao na SHIVIWATA yalifanyika jana asubuhi na baada ya kumalizika wanasiasa hao waliendelea na ratiba yao ya kukutana na vyama vingine vya walemavu vidogo vidogo Makao Makuu ya CUF, Buguruni, jijini Dar es Salaam. Mikutano hiyo ya vyama hivyo vitatu vya siasa ni mwendelezo wa mikutano mingine ambayo tayari imeishafanyika tangu wabunge wake wasusie mjadala wa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba Mpya.

Tangu kumalizika kwa Bunge, vyama hivyo vimeshafanya mikutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania, Jukwaa la Katiba na SHIVIWATA; na Jumamosi vitafanya mkutano mkubwa viwanja vya Jangwani ili kueleza jinsi mswada huo ulivyopitishwa kiujanja ujanja. Wakati hayo yakiendelea wadau mbalimbali wameshauri mswada huo usithubutu kupelekwa Ikulu kwa Rais Kikwete ili ukasainiwe na kuwa sheria.Wakizungumza Dar es Salaam  wakati wa mjadala wa wazi wa nini kifanyike hadi sasa mchakato wa mabadiliko ya katiba ulipofikia, wadau hao walisema yanatakiwa yafanyike maombi ya kukwamisha mswada huo. 

Mjadala huo ulioandaliwa na mtandao wa jinsia (TGNP). Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba, Deus Kibamba, alisema mchakato wa mabadiliko ya Katiba haukuanza kwa huruma ya Rais Kikwete, bali watu waliudai kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, hivyo inabidi ufanyike kwa uwazi. Alisema huo ni mchakato wa kwanza kufanyika kwa wananchi kutoa maoni yao, lakini umeanza kutushinda kutokana na wananchi kukosa elimu ya katiba.  Aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Xavery Rweitama, alisema mjadala wa mswada huo umetekwa na wanasiasa jambo ambalo limekuwa mwiba mkali kwao. 

Alisema kuna wanasiasa wa ajira na wale ambao wanataka masilahi ya wananchi. Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetokana na shinikizo la nje ya bunge ndiyo maana imeweza kufanya mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kupendekeza Serikali tatu.Alisema suala la Serikali tatu limekuwa mwiba mkubwa kwa CCM kutokana na chama hicho kuamini kuwa kinaweza kutawala milele. 

Naye Mwakilishi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga, alisema kwa sasa kuna hali ya wanasiasa kuteka mchakato wa katiba kwani wananchi wamebaki kuzungumzia Serikali tatu tu.  Alisema ni lazima wananchi wajue kutenganisha siasa na Katiba Mpya, kwani walio wengi wanaamini kuwa wahusika wakuu ni wanasiasa na si wananchi.

SAKATA LA WAHAMIAJI HARAMU: SITTA AWATETEA



Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana kuhusu kutengwa kwa Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki pamoja na ‘Operesheni Kimbunga’ inayoendelea hapa nchini. Kulia ni Katibu mkuu wa wizara hiyo Joyce Mapunjo. 


  • APINGA VIKALI UTARATIBU UNAOTUMIKA KUWAONDOA
  • ASEMA UNAKIUKA HAKI ZA BINADAMU, UTAWALA BORA
  • AHOJI KWA MIAKA YOTE SERIKALI ILIKUWA WAPI

 Salim Nyomolelo na Anneth Kagenda

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amekosoa utaratibu unaotumika kuwaondoa wahamiaji haramu nchini kupitia Operesheni Kimbunga, akisema ni kinyume cha haki za binadamu.Waziri Sitta amekuwa kiongozi wa kwanza nchini kukosoa utaratibu unaotumika kuondoa wahamiaji hao tangu Rais Jakaya Kikwete, aagize wawe wameondoka nchini ndani ya siku 14, vinginevyo wataondolewa kwa nguvu. Rais Kikwete alitoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Akizungumza , Sitta aliwataka wakuu wa mikoa, wilaya, jeshi la polisi na uhamiaji kuwapa muda wa kutosha wahamiaji hao ili waweze kujiandaa kuondoka na mali zao ambazo walichuma kwa muda mrefu walioishi nchini kuliko kuwaswagaswaga.

"Haifai kwa hawa ndugu zetu ambao tumeishi nao kwa muda mrefu leo hii wanaswagwaswagwa jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu pamoja na utawala bora," alisema na kuongeza;"Je, Watanzania waliopo nje ya nchi wakiondolewa kwa nguvu kama hawa wenzetu wanavyofanyiwa tutafurahi?" Alisema kwa jambo hili Tanzania isionekane ina nongwa na nchi fulani kwani hata Rais Kikwete, wakati anatoa agizo hilo hakusema utaratibu huo utumike.

Alitoa mfano kuwa kuna mwanamke ambaye amefukuzwa nchini ambaye ni raia wa Rwanda akisema aliishi kwa zaidi ya miaka 30 nchini Tanzania na mtoto wake amesomea nchini na kuajiriwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)."Mtu kama huyu hakutendewa haki...mtu unamfukuza anaondoka na begi lake moja wakati ana mali zake nyingi...huyo ni lazima arudishwe ili ahakiki mali zake," alisema.

Alisema walioondolewa na kuacha mali zao nyingi pamoja na watoto watarudishwa nchini kufanyiwa uhakiki kama inavyofanyika kwa raia wa Malawi. Alishauri wahamiaji hao watakaorudi kufuata mali zao wapewe makazi ya muda na mali zao zisiporwe kwani watu hao hawakuwa majambazi.

"Kama umemuacha mtu ameishi nchini kwako kwa muda wa miaka 30 halafu leo unamfukuza kwa kumswagaswaga nani mwenye kosa? Na muda wote ulikuwa wapi?" Alihoji Sitta na kusisitiza kuwa; "Ndiyo maana tunasema aondolewe kwa utaratibu."Aliongeza kuwa miongoni mwa wahamiaji haramu waliofukuzwa baadhi yao waliwahi kuwa viongozi wa Serikali za vijiji na mitaa katika maeneo waliyokutwa wakiishi.

Waziri Sitta alisema tayari amepokea barua kutoka nchi za Burundi na Rwanda zikilalamikia utaratibu unaotumika kuwaondoa wahamiaji haramu hao."Oktoba 1 mimi na Waziri wa Mambo ya Ndani tutakuwa mpakani mwa Burundi na Rwanda ili kuangalia jinsi operesheni hiyo inavyotekelezwa na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hizo ili Tanzania isionekane ina malengo mabaya," alisema Sitta.

Alisema endapo utaratibu unaotumika wa kuwaondoa ukiendelea maadui wa Tanzania wataona njia hiyo inalenga kuwakomoa, jambo ambalo si la kweli.

UJASILIA MALI NI PAMOJA NA MICHEZO


KONGAMANO KUBWA LA WIKI YA NEEMA LIMEENDELEA KATIKA VIWANJA VYA KIBAMBA HOSPITALI KWA AJILI YA KUOMBEA NCHI NA KUWAOMBEA WATU MBALIMBALI WENYE MAHITAJI

Wakazi wa Maeneo ya Mbezi, Makondeko, Kiluvya na Kibamba wameendelea na Huduma ya Wiki ya Kongamano kubwa la Wiki ya Neema katika Viwanja vya Kibamba HOSPITALI, lilianza tarehe 13  /9/2013 mpaka 22/9/2013. Huduma mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwamo kuombea wagonjwa, kuwapa na kuwatia Moyo wote wenye shida na matatizo mbali mbali.

ITV Tanzania Gari la mizigo lasababisha kifo cha mtu 1 Buswelo Mkoani Mwanza.:http://bit.ly/1aNVhX0


Gari la mizigo lasababisha kifo cha mtu 1 Buswelo Mkoani Mwanza.:http://bit.ly/1aNVhX0

TANZANIA KINARA KUVUTIA MITAJI YA UWEKEZAJI


Na Rehema Maigala

TANZANIA imeendelea kufanya vizuri katika kuvutia mitaji na kuongoza katika nchi za Afrika ya Mashariki.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya uwekezaji ya Rand Merchant Bank (RMB) ya mwaka 2013 inayotoa mwongozo wa mahali pa kuwekeza kwa kampuni Ripoti hiyo inaonesha kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania imeishinda Kenya katika kuvutia mitaji ya wawekezaji wa kampuni.Akizungumzia ripoti mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Juliet Kairuki, alisema kuwa Tanzania imeshikilia nafasi yake katika kundi la nchi 10 bora zinazovutia uwekezaji wa mitaji ya kampuni kubwa. 

Kufanya vizuri kwa Tanzania kunatokana na kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji ikiwemo jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.“Ripoti hii ni uthibitisho tosha wa jitihada zinazofanywa na Serikali kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuvutia mitaji kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema Kairuki. Tanzania, Kenya na Ethiopia ni nchi pekee zilizo katika kundi la nchi 10 zinazofanya vizuri katika eneo hili la Afrika.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imepanda nafasi moja na kuwa ya tisa wakati Kenya imeshuka nafasi na kuwa ya kumi.

Pamoja na kwamba Rwanda haikuwa katika nchi 10 bora, bado imeendelea kuwa kivutio na kushika nafasi ya 14. Nchi ya Uganda ni ya 15, Mauritius 16, Angola 20, na Burundi imeshika nafasi ya 41.Nchi ya Afrika Kusini ndiyo inayoongoza kwa kuvutia uwekezaji ikifuatiwa na Nigeria katika nafasi ya pili. RMB inatumia vigezo vikuu vitatu kuangalia suala zima la kuvutia uwekezaji katika kila nchi kama ifuatavyo: Ukubwa wa soko; ukuaji wa uchumi kwa miaka mitano ijayo na mazingira ya kazi katika nchi husika.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi za Afrika bado zina kazi kubwa ya kufanya kuvutia uwekezaji duniani kulinganisha na nchi nyingine.

Kairuki alisema ripoti hiyo inataka ushirikishwaji zaidi wa sekta binafsi ili kuvutia zaidi mitaji kutoka kampuni na benki kubwa."Kwa mara nyingine tena tunahamasisha ushiriki zaidi wa sekta binafsi katika ujenzi wa nchi yetu," alisema. Alisema kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo kuifanya Tanzania kufanya vizuri zaidi, TIC imefurahia ripoti hiyo na kusema kuwa inaonesha juhudi za Serikali katika kujenga mazingira bora ya uwekezaji na biashara.

INUKA YAKOPESHA WAJASIRIAMALI 29,000

Na: anaripoti Re hemaM aigala.

ZAIDI ya sh.milioni35 zimetumika kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali wadogo na wakubwa kwa ajili ya kuendeleza biashara zao, Akizungumza katika mafunzo ya ujasiriamali juzi jijini Dar es Salaam,Ofisa Mikopo wa Taasisi ya Inuka Wanawake na Maendeleo, David Msuya alisema tayari wameshakopesha pesa hizo kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kuwa,katika Mkoa wa Dar es Salaam tayari wanachama 29,000 ambao wengi wao wamesha kopeshwa mkopo mdogo ambao hauna riba unaoanzia sh. 30,000.
Hata hivyo, alisema hivi karibuni wamepata wajasiriamali wapya 30 wanaotoka Mbezi Mpigi Magoe, Wilaya ya Kinondoni ambapo tayari wameshawakopesha sh. milioni 1.8.
Vile vile, Msuya alisema hivi sasa wana vituo 16 ambavyo vipo Dar es Salaam, Shinyanga, Tanga, Tunduru, Lindi na Mtwara.Hata hivyo, ofisa mikopo huyo aliwataka wajasilimari kuwa wa kweli katika biashara zao na kuwa wabunifu.  

“Mjasiriamali yeyote anatakiwa kuwa mbunifu wa kujua leo atengeneze nini ili aweze kupata wateja wengi kushinda mwenzake na si kuigizana bidhaa,” alisema Msuya.Hata hivyo, taasisi hiyo ilisema lengo lake ni kuinua wajasiriamali wa chini ili waweze kuwa wakubwa 
Alisema kuwa,katika Mkoa wa Dar es Salaam tayari wanachama 29,000 ambao wengi wao wamesha kopeshwa mkopo mdogo ambao hauna riba unaoanzia sh. 30,000. 

Hata hivyo, alisema hivi karibuni wamepata wajasiriamali wapya 30 wanaotoka Mbezi Mpigi Magoe, Wilaya ya Kinondoni ambapo tayari wameshawakopesha sh. milioni 1.8.Vile vile, Msuya alisema hivi sasa wana vituo 16 ambavyo vipo Dar es Salaam, Shinyanga, Tanga, Tunduru, Lindi na Mtwara.Hata hivyo, ofisa mikopo huyo aliwataka wajasilimari kuwa wa kweli katika biashara zao na kuwa wabunifu.

“Mjasiriamali yeyote anatakiwa kuwa mbunifu wa kujua leo atengeneze nini ili aweze kupata wateja wengi kushinda mwenzake na si kuigizana bidhaa,” alisema Msuya.Hata hivyo, taasisi hiyo ilisema lengo lake ni kuinua wajasiriamali wa chini ili waweze kuwa wakubwa

TBS YAFUNGA KIWANDA CHA UZALISHAJI NONDO

NaMwandishi Wetu, Kib aha

SHIRIKA la ViwangoTanzania (TBS) limesitisha shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha nondo cha Hong Yu Steels COT LTD kilichopo Visiga wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani hadi pale kitakapo kamilisha taratibu za kuwa na leseni za ubora wa viwango .Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusitisha shughuli za kiwanda hicho,mkaguzi wa viwango vya vyuma wa TBS,Yona Afrika ,alisema kuwa baada ya kufanya ukaguzi waligundua kwamba nondo zinazozalishwa katika kiwanda hicho hazina viwango upande wa ukubwa. 

Alisema kuwa nondo hizo zina viashiria vya upungufu wa ubora ndiyo maana wameamua kusitisha shughu li za uzalishaji hadi pale watakaporidhika baada ya kiwanda hicho kuthibitisha ubora wa nondo hizo kwa shirika hilo. Alisema pia wamesitisha nondo zilizokwisha tengenezwa zisitoke nje ya kiwanda hicho hadi pale zitaka pothibitika kwamba ubora wake unaridhisha. Nondo hizo ni zile zenye uzito wa tani255 zenye unene wa mita 12 na tani 14 zenye ujazo wa mita14.Alisema kuwa pia TBS itatoa muda kwa uongozi wa kiwanda hicho kurudisha nondo zilizokwishapelekwa kwa wateja .

Alisema ni rahisi nondo hizo kurudishwa kwa kuwa zina jina la kiwanda hicho. Naye,Mwanasheria waTBS, Baptista Bitaho,alisema shirika hilo linafanya kazi kupitia sheria namba mbili y aviwango ya mwaka 2009 na kwa kupitia sheria hiyo linafuatilia wadau wake ili kuhakikisha wazalishaji wanakuwa na leseni za ubora. Alisema kuwa pale wanapoona mzalishaji anakwenda kinyume na kukiuka sheria za viwango TBS inachuk ua hatua kw akusimamisha uzalishaji kwa muda hadi pale mzalishaji huyo atakapofuata sheria za uzalishaji.
Alisema katika kutekeleza azma ya shirika hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi kub wa ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kupokea rushwa.

Mkalimani wa wamiliki wa kiwanda hicho ambao ni raia wa nchini ,Ernest Sinje,alisema TBS kusitisha uzalishaji wa kiwanda hicho ni hujuma kutoka kwa viwanda vingine vinavyotengeneza nondo nchini. Alisema kiwanda hicho ndicho kinazalisha nondo zenye ubora kwa Tanzania