TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, April 12, 2014

MVUA JIJI DAR ZALETA MAFURIKO YAMAKUBWA

Hapa ni eneo la Jangwani Uwanja wa Club ya Yanga na nyumba zilizopo pembeni yake pakiwa pamejaa maji na barabara ya jangwani kutokea Kigogo haipitiki.
Huu ni uwanja wa Club ya Yanga ukiwa umejaa maji.
Hii ni Braking News ya Daraja la Matumbi kutoka Buguruni kuelekea Ubungo.....
Jangwani......
Nyumba za jiraji na Jengo la Yanga Jangwani......
Mito ni kama hivi hatari tupu.....
Hatari tupu eneo la Mbagala.....
Lori likiwa limetumbukia baada ya barabara kukatika kutokana na mvua kubwa iliyosababisha maji kukatiza barabara eneo la Mbagala. Dereva ameokolewa na wasamariawema.
Wananchi wakihama baada ya nyumba zao kujaa maji....
Wananchi wakiokoana kimtindo......
Nyumba za Dar Villa Msasani.....
Hapa ni Bunju, .......
 Sehemu ya maduka yaliyopo eneo la Kituo cha daladala cha ITV yakiwa yamezingirwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Kutokana na mvua hizo na maji kujaa kumesababisha msongamano mkubwa wa mago kuanzia jana jioni na leo.
 Barabara ya kuelekea Goba....
 Barabara ya Goba ikiwa imeharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
 Maji yakitiririka kwa kasi katika Mto Mbezi eneo la Bondeni...
 Vijana wakitumia fursa vizuri kwa kujipatia mchanga unaotiririshwa na maji ambapo huwauzia madereva wa maroli.
 Eneo la Mwenge karibu na kituo cha daladala.....
 Moja ya daladala lililokuwa gereji likiwa limezingirwa na maji eneo la Mwenge....
 Maduka ya Mwenge yakiwa yamezingrwa na maji.....
 Mdada huyu alikuwa akipiga hesabu na kujiuliza jinsi ya kuvuka maji yaliyojaa na kukatiza barabara eneo la ITV.
 Mwenge karibu na Zahanati......hakuna njia ya kuingilia Zahanati
 Maduka eneo la Mwenge yamejaa maji....
 Kazi haifanyiki leo katika maduka haya...
 Mwenge eneo la Nakiete......
 Maji yakikatiza barabara eneo la ITV.....
 Mitungi ya Ges ikielea....
Njia panda ya Kwa Nyerere.......

KAMPUNI ZA LUGUMI NA RAN IT ZATOA KOMPYUTA TANO NA FEDHA TASLIMU SHILINGI MILIONI 10 SHULE YA SEKONDARI PANGANI KIBAHA

Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akikabidhi kompyuta 5 kwa Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba kwa ajili ya shule ya sekondari ya Pangani wakati wa makabidhiano yaliyofanyika shuleni hapo leo mjini Kibaha ambapo pia mwakilishi huyo alikabidhi kiasi cha fedha Taslimu  shilingi milioni 10,000,000 kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabala katika shule hiyo.katikati ni Mkuu wa shule hiyo Inocencia Mfuru
Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akikabidhi fedha taslimu shilingi milioni 10,000,000 kwa Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara katika shule hiyo katikati ni Mkuu wa shule hiyo Inocencia Mfuru
Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya makabidhiano.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba wa tatu kutoka kushoto akiwa pamoja na wanafunzi wawakilishi wakati wa makabidhiano hayo, kutoka kulia ni Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises,Mkuu wa shule hiyo Inocencia Mfuru na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha Jenipher Omolo.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba pamoja na wawakilishi wa kampuni za RAN IT Solution na Lugumi Enterprises pamoja na wakuu wa shule ya Sekondari Pangani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano hayo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Pangani wilayani Kibaha wakibeba kompyuta kwa ajili ya kukamilisha kazi ya makabidhiano shuleni hapo leo.
Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprises za jijini Dar es salaam akipokea cheti cha kutambuliwa rasmi kwa mchango wa kampuni hizo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba.
 Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh. Halima Kihemba akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano.
 Baadhi ya wanafunzi wakihojiwa na mwandishi wa habari Faraja Kihongole kutoka kituo cha Televisheni cha Chanel Ten.
Fatma Mohamed Meneja msaidizi wa kampuni ya RAN IT Solution Limited na Lugumi Enterprisesna ,Ellygood Sangawe Meneja wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa wakitembelea maabara ya shule hiyo.
 Mkuu wa shule ya sekondari ya Pangani ya Kibaha  Inocencia Mfuru akitoa maelezo kwa wageni hao wakati walipokuwa wakitembelea maabara.
Baadhi ya majengo ya shule ya Sekondari Pangani. (FS)

Sunday, March 30, 2014

WADAU MBALI MBALI WAMEOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI MATANGAZO YA DACICO FM KUPITIA WWW.DACICOFM.COM

MDAU WA DACICO, HII NDIYO STUDIO YA RADIO YETU YA
www.dacicofm.com

Ukiwa kama mdau wetu tunaomba uweze kutusikiliza kila wakati na kila saa ususani wewe ambaye mdogo wako au mwanao pengine yawezekana anaitaji kujiunga na Chuo chetu, ni wakati wako kufuatilia kwa makini kuhusu chaguo la kumpeleka ili aweze kusoma na kupata Elimu ambayo ni kwa ajili yake. bofya tu hapa utasikia moja kwa moja. Radio na Chuo kinapatikana Kibamba CCM, Mita 100 kutoka barabarani. asante kwa ushirikiano wako.
Unlike ·  ·  · 11 · March 27 at 3:31am  
Yah ni kweli hata mimi nimeipenda sana Studio hii pamoja na kwamba ni ya chuo lakini inafanya vitu vikubwa.· 
habari hii kutoka Mtandao wa DACICO TANZANIA

Tuesday, March 25, 2014

OPARASHENI TAFUTA TAFUTA NDEGE YA MALAYSIA MH370 YAFIKIA KIKOMO

Jamaa za abiria wa ndege hiyo wamekumbwa na majonzi makubwa.

Mamlaka ya usalama wa safari za baharini nchini Australia imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya shirika la Malaysia iliyotoweka imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa na mawimbi makali baharini.
Taarifa zinasema kuwa upepo mkali pamoja na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo ina maana kuwa ndege hazitoweza kupaa kwa usalama. Mawimbi makali yameilazimisha meli ya jeshi la wanamaji wa Australia kuondoka katika eneo ambalo mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege hiyo yalionekana hapo jana Jumatatu.

Dr Erik van Sebille, ambaye ni mtaalam wa maswala ya Baharini katika chuo kikuu cha New South Wales mjini Sydney, amefanya utafiti katika eneo hilo la kusini mwa Bahari Hindi kutambua ni wapi na vipi vifusi vinasafirishwa na mawimbi ya bahari. Anasema itakuwa vigumu sana kupata mabaki ya ndege hiyo.

Shughuli ya kuitafuta MH370 imesitishwa
" Ni eneo lisiloweza kukalika duniani, acha niseme. Upepo unaovuma ni mkali sana, mawimbi ni makubwa, ni mojawepo wa mawimbi makubwa zaidi baharini. Unapofika katika eneo hili la kusini, unaanza kuhisi athari za eneo la Antactica kwenye bahari. Hapa tunazungumzia dhoruba kali kali sana hususan wakati huu tunapoingia majira ya kupukutika," anasema Dr. Erik van Sebille.
Kadhalika amesema kuwa vifusi vilivyoenekana hapo jana tayari vimekwishaondolewa katika eneo hilo na mawimbi makali.
"Haitakuwa rahisi kabisa kupata kijisanduku cha kunasa habari. Mawimbi ya eneo hili ni makali na kwa hiyo vifusi ambavyo wametambua kwa sasa huenda vimehamishwa katika kipindi cha majuma mawili au matatu tangu ndege hiyo ianguka-na huenda vimesafiri kilomita alfu moja tayari. Na hii inaifanya vigumu kurejelea utafutaji kwa sababu bahari inabadilika sana hapa-ina vurugu ukipenda."
Hapo awali naibu waziri wa mashauri ya nchi za Kigeni wa China Xie Hangsheng, aliitaka serikali ya Malaysia kutoka ushahidi unaoelezea kuwa ndege hiyo ilianguka katika eneo la Kusini mwa bahari Hindi. Ndege hiyo ilitoweka kwenye mtambo wa Radar zaidi ya majuma mawili yaliyopita

RAIS UHURU KENYATTA NDANI YA TANZANIA JANA