Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa mafunzo yanayotolewa na
Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kwa Menejimenti ya wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati walipotembelea mfumo wa
usimamizi wa nyaraka wa kidijiti.
Alisema pia kuwa mfumo huu una faida nyingi na ndio ambazo
zimeifanya wizara hii kutaka kujifunza ni pamoja na suala la gharama na
kwa kuwa serikali ya awamu ya tano iko katika jitihada kubwa za
kupunguza matumizi na kwa kuwa bajeti ya shajala ni kubwa katika taasisi
nyingi za serikali hivyo mfumo huu wa kidijiti utasaidia kupunguza
garama kwani hapatakuwa na haja ya kutumia karatasi na hivyo kupunguza
gharama kubwa.
Prof Elisante pia aliongeza kuwa mfumo huu utaongeza usiri wa
nyaraka hizi na kwa sasa zitakuwa zinasomwa na yule tu aliyekusudiwa na
kutoa pongezi kwa ofisi ya rais manejimenti ya umma kwa kuhamasisha
matumizi ya mfumo huu kwani ukitumiwa vyema utakuwa na manufaa sana.
Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora alisema kuwa mfumo huo ulijengwa miaka
mitatu iliyopita na unaweza kutumika katika wizara yeyote kwani una
ufanisi mkubwa sana kwani kwa sasa utaweza kuangalia mafaili gani
yameingia kwa mfumo wa kidijitali na kwa namna hii itapunguza garama
na muda kwani hatutakuwa tunatumia karatasi tena.
Prof.Kamuzora alizitaka Taasisi na Wizara mbalimbali kuwapa elimu
ya kutosha watunza kumbukumbu kwani wao ndio wahusika wakuu wa kwanza wa
mfumo huu na hivyo kuwataka wahusika kuwapa mafunzo ya kompyuta na
kuboresha vifaa kama scanner maofisini mwao.
Nae mmoja wa watunza kumbukumbu kutoka wizara
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Felomena Swai alisema amenufaika na
mafunzo hayo na yatawasaidia katika utunzaji wa kumbukumbu kwani sasa
watapeleka barua kwa wakati na kurahisisha utunzaji wa mafaili.
===========================================