TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, November 18, 2014

MSAKO WA POLISI MISIKITINI VIJANA MOMBASA WAFARIKI

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie habari Moja Kwa Moja

 KIJANA alipigwa risasi na kuuawa na wenzake zaidi ya 250 kukamatwa kwenye operesheni kali ya kusaka magaidi mjini Mombasa jana. BAADHI ya vijana waliokamatwa ndani ya misikiti ya Musa na Sakina, eneo la Majengo, Mombasa, wakati wa msako wa polisi usiku wa kuamkia jana ambapo kijana aliuawa na washukiwa zaidi ya 251 kukamatwa.Silaha mbalimbali zikiwemo gruneti, bastola, visu na mapanga zilipatikana ndani ya misikiti hiyo. Picha/LABAN WALLOGA

Akihutubia wanahabari katika kituo cha polisi cha Urban, mjini Mombasa, afisa mkuu wa polisi  (OCPD) Mahmoud Salim, alisema kijana aliyeuawa alijaribu kushamulia maafisa wa usalama kwa gruneti walipokuwa wakiingia msikitini. “Walimpiga risasi kabla ya hajatupa gruneti hiyo na kumwua papo hapo,” akasema Bw Salim na kuapa kuwa operesheni hiyo itaendelea hadi wahalifu wote wanaswe.  Vijana 16 walikamatwa ndani ya msikiti wa Masjid Musa na wengine wanane wakapatikana kwenye msikiti wa Sakina. 
Wakati huohuo, viongozi wa eneo la Mombasa wametaka vijana waliotiwa mbaroni waachiliwa mara moja kama hawatapatikana na hatia. 
Wakiongozwa na gavana Hassan Joho, viongozi hao walifika katika makao makuu ya polisi ya kaunti hiyo ambako walishauriana na maafisa wakuu wa polisi kwa karibu saa mbili. 
Walishutumu maafisa wa polisi kwa kuvamia msikiti wakisema ni mahali patakatifu pa ibada. 
Wengine walikuwa Seneta Hassan Omar, Mwakilishi wa Wanawake Mishi Juma Mboko na wabunge Abdulswamad Nassir (Mvita), Rashid Bedzimba (Kisauni) na Badi Twalib (Jomvu). 
- Taifa Leo

No comments:

Post a Comment