TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, November 19, 2014

UZUNDUZI NA UHAMASISHAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII(CHF) WILAYANI KILINDI MKOANI TANGA

unnamedMeneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mkoa wa Tanga(NHIF)Ally Mwakababu kulia akimuelezea mikakati ya mfuko wa Afya
ya Jamii (CHF) Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa kulia kwake kabla ya kufanya uzinduzi wa Uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii wilayani humo (CHF) zoezi ambalo linaendeshwa na Meneja huyo na maafisa kutokana makao makuu na mkoani Tanga kwa muda wa siku kumi.
unnamed1Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) na watumishi wa Halmashauri hiyo Idara ya Afya ofisini kwake kabla ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).unnamed5Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi,Daudi Mayeji  akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake kabla
ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wilayani humo kulia kwake ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo kutoka makao makuu Isaya Shekifu.
unnamed6Afisa Uanachama wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga (NHIF) Miraji Swalehe akiwaelimisha waendesha pikipiki kwenye kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuweza kupata matibabu muda wote.unnamed7Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu akiwahimiza wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake uliofanywa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa.unnamed9Mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) tokea ulipoanzishwa wilayani humo akimuonyesha kadi zake Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu.unnamed10Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga,Suleimani Liwowa akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa  Tanga(NHIF)Ally Mwakababu  na maafisa wengine wa mfuko huo na
madereva wa pikipiki “Bodaboda”mara baada ya kuwakabidhi kadi zao za
uachama wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
unnamed12DC Liwowa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani humo wakati akiwahamasisha kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake.unnamed13Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 
(NHIF)kutoka Makao Makuu ,Isaya Shekifu akiwahamisha wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi mkoani Tanga juu ya umuhimu wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

No comments:

Post a Comment