TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 21, 2015

SIKU YA WATOTO NJITI


 Mwanzilishi wa Mfuko wa Doris Mollel, Doris Mollel akizungumza katika kilele cha maazimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya siku (njiti) katika mkutano ambao umefanyika leo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akizungumza kwenye maadhimisho hayo leo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha akifuatilia mkutano huo leo pamoja na wauguzi waandamizi wa hospitali hiyo.
 Mmoja wa kinamama akiwa na mtoto wake ambaye alizaliwa kabla ya kutimiza siku akishiriki maadhimisho hay oleo katika hospitali hiyo.
 Mashine iliyotolewa kwa ajili ya kuwatunza watoto wanaozaliwa kabla ya muda. Mashine hiyo imetolewa leo na mfuko wa Doris Mollel kwa ajili ya kutunza watoto hao.
 Mmoja wa kinamama, Lipina Lyimo akizungumza katika kilele cha maazimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya siku (njiti). Katika mkutano na waandishi wa habari Mama Lyimo amesema alijifungua mtoto kabla ya kutimiza muda na kwamba madaktari na wauguzi walimwelekeza jinsi ya kumtunza mtoto wake, Emmanuel Mgumba hadi amekuwa mkubwa na kuwa na afya bora.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akiwa amembeba mtoto, Emmanuel Mgumba  ambaye alizaliwa kabla siku. Mama wa mtoto huyo Lipina Lyimo ameleza jinsi alivyopewa huduma nzuri na wauguzi na madaktari wa ‘Huduma ya Mama Kangaroo’ baada ya kujifungua mtoto kabla ya muda (njiti).

No comments:

Post a Comment