TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, November 20, 2015

Stanslaus Mabula alitaka Tamasha la Kushukuru


Na Mwandishi Wetu
MBUNGE  wa Nyamagana Stanslaus Mabula ameiomba Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwewnye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, lihamie jijini Mwanza kwa lengo la kufikisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama wanayafanyia kazi mapendekezo ya Mabula ili kufanikisha tamasha hilo adhimu lenye nia ya kushukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu.


Msama alisema tamasha hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili ambao watawasilisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu.

Msama alisema Kamati yake inajipanga kufikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu kupitia viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali hapa nchini.

“Tamasha la Kushukuru Mungu lina mtazamo wa kufikisha asante kwa Mungu baada ya kuendelea kudumisha tunu ya amani ambayo ndio sifa ya Tanzania nje ya mipaka,” alisema Msama.

Aidha Msama alitoa wito kwa Wadhamini na wafadhili kujitokeza kwa lengo la kusaidia tamasha hilo.
Mwisho  

No comments:

Post a Comment