TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, April 4, 2016

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM WAKAMATA VITENGE NA PAMPERS ZISIZOLIPIWA USHURU

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii. JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata Marobota 10 ya vitenge na Katoni 17 za Pampers  pamoja na Gari lililotumika kubebea hitu hivyo katika eneo ya Gezaulole lililopo pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa kukamatwa kwa gari lenye vitu hivyo ni mara baada ya kupewa taarifa na Raia wema kwa kuwa katika eneo hilo kunapitishiwa mali zisizotolewa ushuru.

Siro amesema kuwa Gari lililo kamatwa na Vitenge na Pampers ni aina ya Suzuki Carry lenye namba za usajili T490 CQB ambalo nalo linashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam.

Pia Sirro amesema kuwa mwananchi anaeona kuwa alitelekeza gari hilo lililo na vitu hivyo ajisalimishe Polisi ili apelekwe Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) akalipie ushuru wa vitu hivyo.

Katika Operesheni nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilifanikiwa kukamata gari moja la wizi aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 314 DFH  ambapo kabla ya kuibwa lilikuwa na namba za usajili T 622 DDR  ikiwa gari hilo ni Mali ya Hellen Michael liliibwa maeneo ya Kitunda Kivule ambapo lililuwa limeegeshwa nyumbani kwake. Pia Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limkamata watu wawili wakiwa na Pikipiki mbili zenye namba za usajili MC343 ASL aina ya Boxer na MC 606 ex aina ya Fercon ambazo ni za wizi na watuhumiwa hao kukuli kuwa wameziiba Pikipiki hizo.

No comments:

Post a Comment