TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, April 4, 2016

Rais Magufuli , Raila Odinga Kila Mtu Kivyake

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuashiria kuagana na wageni wake, Raila Odinga pamoja na Mkewe Ida Odinga waliofika Chato juzi kwa ajili ya mapumziko na kumpongeza Mhe. Rais.
 Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita. Odinga alifika Chato juzi akiwa na familia yake kwa ajili ya kumpongeza Mhe. Rais pamoja na kushiriki pamoja Ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Bi. Ida Odinga.
 Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga, Bi Ida Odinga katika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Bi Ida Odinga, huku Raila Odinga akiagana na Mama Janeth Magufuli katika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Raila Odiga, Ida Odinga pamoja na Mkewe mama Janeth Magufuli katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia watoto aliwakuta kwenye uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment