TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, April 7, 2016

MKUU WA WILAYA YA BABATI AIFUNGA SHULE KUFUATIA KUHARIBIKA KWA VYOO.

Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela
Na Woinde Shizza,Manyara Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela ameifunga shule ya msingi Matufa kwa muda usiojulikana baada ya kutitia kwa matundu ya vyoo vya wanafunzi na walimu kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazonyesha. Akizungumza baada ya kuitembelea shule hiyo, Meela alisema kutokana na matundu  24 ya vyoo vya shule hiyo kuharibika inabidi shule hiyo ifungwe kwani hakuna vyoo vingine vya kutumiwa kwa wanafunzi na walimu. Hata hivyo, kaya 64 zilizokuwa zinaishi kwenye shule hiyo ya Matufa kwa kukosa makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha siku mbili hivi sasa wamepatiwa hifadhi kwa kuwekwa kambini. Alisema kutokana na maafa hayo hana budi kuifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana na anatarajia watahakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa muda mfupi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wilaya na mkoa huo. “Namuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati vijijini Dominick Kweka, kuhakikisha shule hiyo inajengewa vyoo mara baada ya wiki moja kupita ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao,” alisema Meela. Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Babati vijijini Vrajlal Jitu Soni aliwapa pole wakazi wa vijiji vya Magugu na Matufa vilivyopo kwenye tarafa ya Mbugwe ambao wameathirika kutokana na mafuriko hayo. Jitu Soni alisema hivi sasa wanafanya tathmini ya mafuriko hayo ili kamati ya maafa kupitia ofisi ya Waziri Mkuu waweze kuwapatia msaada wananchi hao ambao nyumba na mazao yao yamechukuliwa na mafuriko hayo.

No comments:

Post a Comment