TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, April 4, 2016

Mhe. Mhagama aagiza wamiliki wa vyombo vya usafiri kuzingatia mikataba ya kazi na ajira kwa madereva



Mhe mhagama alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wake na Kamati hiyo uliofanyika Aprili 1, 2016 katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya usafirishaji. 

Katika kikao cha Kamati hiyo inayoundwa na Wamiliki wa malori, daladala, mabasi, vyama vya abiria, Idara ya Usafirishaji, Shirika la viwango, Wakala wa Vipimo, Jeshi la polisi, watu wa usalama barabarani, TANROADS  na Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (UWADAR) mhe. Mhagama alisisitiza kuwa Serikali haitawafumbia macho wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawazingatii mikataba ya kazi kwa madereva. 
“Ninaagiza mikataba ya maderva iangaliwe upya na ikiwezekana yaainishwe majina ya wamiliki wa magari wanaokiuka haki na sheria zilizopo za kuwapa madereva mikataba na stahiki zao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,”alisema Mhagama 

Kutokana na changamoto mbalimbali za madereva zilizobainishwa wakati wa mkutano huo  Mhe.Waziri aliwataka wajumbe wote kuangalia namna nzuri ya kukabili changamoto hizo ili kuhakikisha malalamiko ya madeva yanaisha na kufanya sekta hiyo kuwa na  amani na utulivu. 

“Lengo kuu ni kuona sekta ya usafirishaji inakuwa salama na yenye amani kwani ikumbukwe sekta hii ni nyeti, inabeba roho za watu wengi kila iitwapo leo kwa kuwasafirisha mikoani na nje ya mikoa.” Alisisitiza Mhagama. 

Nae mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Leonard Chamuliho aliomba kamati kuyafikia maazimio ya muhimu yaliyojadiliwa na huku akisisitiza agizo la mhe. Mhagama la kuwataka wamiliki na waajiri wote kuzifuata na kuzitekeleza sheria za mikataba kwa waajiriwa wote. 

No comments:

Post a Comment