Meneja
Rasilimali watu wa Airtel, Bi, Gabriella Kaisi (kulia) akiwapongeza
James Kwayu (katikati) na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo
waliofaidika na aiira katika kampuni ya Airtel kupitia ushirikiano kati
ya Airtel na chama cha wanafunzi vyuoni Tanzania AIESEC wenye lengo la
kuwawezesha vijana walioko vyuoni kupata ajira katika makampuni
mbalimbali kila mwaka.

Mwenyekiti
wa taasisi ya Muzdalifa Shekh Abdalla Hadhar Abdalla akimkabidhi Mchele
Afisa msaidizi wa kambi ya wahanga wa mafuriko Makame Khatibu Makame
iliopo Skuli ya Mwanakwerekwe C Mjini Zanzibar.
Afisa
msaidizi wa Kambi ya Mafuriko iliyopo Skuli ya Mwanakwerekwe C Makame
Khatib Makame, akitoa shukrani kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Muzidalifa
Shekh Abdalla Hadhar Abdalla kwa msaada waliowatia.
Baadhi ya Misaada mbalimbali iliyotolewa na Taasisi ya Muzdalifa.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Muzdalifa Shekh Abdalla Hadhar Abdalla akimkabidhi Box la
dawa Daktari dhamana kanda ya Unguja Fadhili Moh’d, katika Kambi ya
kipindupindu iliopo Mtaa wa Chumbuni Zanzibar.
Daktari dhamana kanda ya Unguja Fadhil Moh’d, akitoa shukurani kwa msaada waliopatiwa na Taasisi ya Muzdalifa
Baadhi ya Madawa mbalimbali iliyotolewa.Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika
wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya
Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa
Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo
uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni
mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe
huo kwa wabunge wa Afrika. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Seneta la
Lesotho Mhe Seeiso Berenge Seeiso na kushoto ni senate kutoka Bunge la
Afrika Mhe. Bennette hayatoe
Wabunge
wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Tanzania wakila kiapa cha uaminifu.
Kutoka kushoto ni Mhe. Asha Abdalah Juma, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile,
Mhe. David Silinde na Mhe. Mboni Mhita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza
kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa
TAMISEMI mjini Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kutoka
kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa
TAMISEMI mjini Dodoma.PICHA NA IKULU
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila
akiongoza mazungumzo na Viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na SUMA –
JKT(hawapo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja(wa kwanza kushoto)
akiwa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo wakifuatilia kwa
makini mazungumzo na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Thomas Kashilila(hayupo pichani).
Mtendaji
Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri akifuatilia mazungumzo
hayo na Maofisa Watendaji wa Shirika hilo la SUMA – JKT.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja akiteta jambo na
Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri walipokutana
leo Mei 3, 2016 katika Ofisi za Bunge, Jijini Dar es Salaam(Picha zote
na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).









Mtendaji
Mkuu wa Temesa Mhandisi Manase Ole-Kujan akitoa taarifa juu ya
kusimamia kwa huduma za Mv Magogoni inayofanyiwa Matengenzo makubwa.
Wananchi
wakipita katika daraja la Nyerere lilopo Kigamboani Jijini Dar es
Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Kivuko cha Mv Magogoni kikiwa katika shughuli zake za kila siku za kutoa huduma kwa wananchi. (Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)


Mwenyekiti
wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Bw. John Mponda (kulia)
akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya
Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
Afisa
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.
Fransis Songoro (aliyesimama) akiwasilisha mchango ulitolewa katika
kamati ndogo ndogo zilizoundwa wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi
ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei
mwaka huu.
Mkurugenzi
Msaidizi Sanaa Hajjat Shani Kitogo (aliyesimama) akiongoza majadiliano
jana Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya
siku ya Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe ya 21 Mei.
Afisa
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.
Sefania Motela (aliyesimama) akichangia wakati wa kikao cha kamati ya
maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe
21 Mei mwaka huu.
Baadhi
ya Maafisa Utamaduni na Wadau wa Utamaduni wakifuatilia kwa makini
majadiliano yaliyokua yakiendelea wakati wa kikao cha kamati ya
maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe
21 Mei mwaka huu.Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
No comments:
Post a Comment