TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, June 19, 2016

MAKAMU WA RAIS ASISITIZA KUSHIRIKISHA WANAUME KATIKA AJENDA YA MTOTO WA KIKE



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo aliahidi kuwasomesha watoto 100 na aliwasihi Wanawake wanapoweka mipango ya kimaendeleo kuwashirikisha pia wanaume.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa pamoja na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Binti Clubs jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu cha Binti Foundation wakati wa Tamasha Fadhili Mtoto Asome.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akitazama jambo liliokuwa linaendelea (halionekani pichani) pamoja na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Binti Foundation Johari Sadiq .
Sehemu ya watoto walioshiriki kuonyesha mitindo mbali mbali ya Mavazi pamoja na Wabunifu wao.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yanayoshughulikia masuala ya wanawake na watoto kujenga utamaduni wa kushirikisha wanaume katika kampeni za kumwinua mtoto wa kike kwa lengo la kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.

Mheshimiwa Samia ametoa kauli hiyo jana kwenye hafla ya uzinduzi wa Binti club iliyofanyika sambamba na harambee ya fadhili mtoto asome ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto 500 wa wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na Shirika lisislo la Kiserikali la Binti Foundation katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es salaam

Alisema wanaume kama wakala wa mabadiliko wanapaswa kushirikishwa na wajue ajenda ili wawe mabalozi wazuri katika kuzungumzia umuhimu wa kumwinua mtoto wa kike kielimu, kiafya na kwenye masuala ya ujasiriamali.

"Tuwaingize wanaume kama wakala wa mabadiliko, tuwashirikishe, wajue ajenda zetu katika mapambano hayo. wanaume wanashikilia sehemu nyingi, watumie nafasi hizo tulete mabadiliko," alisema Makamu wa Rais na kuongeza."Penye mkusanyiko wa watu 100, ukiingiza wanaume 20, na wakajua madhumuni ya mkusanyiko wetu, wataenda kushawishi wenzao 20,000 huko nje."

Aliipongeza Taasisi hiyo ya Binti Foundation kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika suala la elimu kwani safari ya mtoto wa kike ya kupata elimu inakuwa na ugumu zaidi kuliko wanaume kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mila potofu, hali ya uchumi katika familia na jinsi jamii inavyomwangalia kutokana na ujanajike wake.

"Tuna kazi kubwa ya kumtayarisha mtoto wa kike aweze kupambana na changamoto zinazomzunguka," alidokeza.

Mheshimiwa Samia alitumia fursa hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na changamoto za elimu ikiwa ni pamoja na kuondoa ada katika shule za msingi na sekondari, kuboresha ajira za walimu pamoja na maslahi yao, kujenga mabweni kwa wasichana na kuondoa tatizo la madawati ambapo amewashukuru Watanzania kwa kuchangia madawati.Aliwataka wazazi kuwatunza watoto wao kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu na kuhakikisha wanapata elimu zote ya dini na ya dunia ili kuwajenga kimaadili waweze kuwa raia wema.

Mtendaji Mkuu wa Binti Foundation Johari Sadik alimweleza Makamu wa Rais kuwa shirika hilo liliamua kuunga mkono jitihada za serikali ili kuwawezesha watoto kumudu masomo yao na hatimaye kufikia malengo yao."Kwa hiyo ukiwa na fedha taslimu, ama vifaa kama vile kalamu, madaftari, pedi, vyote tunapokea kwa ajili ya kusaidia watoto ambao malengo yao yanaweza yasitimie kutokana na changamoto hizo,"

Kampeni hiyo ya fadhili mtoto asome imeanzia kwa watoto 500 wanaoishi kwenye mazingira magumu wa shule za msingi Mwananyamala, Hananasif, Kumbukumbu na Msasani zilizoko katika wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam.Katika hafla hiyo iliyopambwa na onesho la mavazi la watoto Makamu wa Rais ambaye alikubali kuwa mlezi wa Binti Foundation aliahidi kusomesha watoto 100 wakati mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa alitoa ahadi pia ya kusomesha watoto 50.

==========================================

irtel yafuturu na Bloggers


Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Airtel, bwana Patrick Foya akiitambulisha kwa blogger VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel. 
Mmimiliki wa 80/20 blog Shamimu akiuliza swali mara baada ya kupata ufafanuzi juu ya mpango wa VSOMO ushirikiano kati Airtel na VETA kwenye mkutano ulifatiwa na Futari.
Baadhi ya Bloggers wakijaribu kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu zao na ipad zao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa kwenye Futari baada ya mkutano wa VSOMO.

Mzee John kitime (katikati) wakijadili jambo pamoja na shamimu mmiliki wa blog ya 80/20 na Josephat Lukaza mmlimiki wa lukaza blog, wakati wa mkutano wa kuitambulisha VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel


Baadhi ya bloggers wakipata futari

Airtel yafuturu na Bloggers 

Katika mpango wake wa kukutana na kuendelea na mfungo wa mwezi Ramadhani leo Airtel kupitia Airtel FURSA imekutana bloggers na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi na kupata cheti kupitia simu yake ya Airtel. 

Akielezea VSOMO Mkurugenzi wa rasilimali watu bwana Patrick Foya alisema, ana anamatumaini kuwa VSOMO masomo ya Ufundi yanayotolewa na VETA kupitia simu za mkononi za Airtel, yatakua suluhisho kwa vijana wengi wenye ujuzi na ari ya kujifunza kufanya shughuli kwa uhakika kwani watakua wamejifunza mbinu zitakazowawezesha kuto bahatisha na kuongeza ufanisi katika kazi zao. 

Nao bloggers walio hudhuria walikua na haya ya kusema, mfumo huu utaleta tija sana kwa vijana wengi ambao wako katika shughuli mbalimbali kupata muda wa kujifunza na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri, tunawapongeza Airtel kwa kuanzia mfumo huu wa masomo kupitia simu. 

Aidha waliongeza kwa kusema wao watakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Airtel kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya vijana katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii katika kujiendeleza kitaaluma.
=======================================

Serikali kuaandaa mashindano ya upandaji miti na ufufuaji wa visiki hai.

Na Daudi Manongi-Dodoma
Waziri wa nchi na Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba amesema kuwa wameandaa mashindano ya upandaji wa miti na ufufuaji visiki hai katika ngazi zote nchini ili kufanikisha mapinduzi ya kijani na kutoa kiasi cha pesa cha shilingi milioni 100 kwa halmshauri itakayofanya vizuri.

Waziri makamba ameyasema hayo alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kwa wabunge kuhusu kukabiliana na tishio la jangwa na kuboresha ardhi iliyochakaa ili izalishe zaidi katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Aidha amesema kuwa atashirikiana na Tamisemi na Wizara ya elimu kuhakikisha elimu ya upandaji miti na ufufuaji wa visiki hai inatolewa kuanzia ngazi ya elimu ya Awali ili wanafunzi waanze kupata elimu hii kuanzia katika ngazi ya chini.

Mhe.Mkamba alisema kuwa upandaji wa miti ndio utaleta manufaa makubwa nchini mwetu kwani hakuna sekta isiyotegemea miti toka uumbwaji wa dunia hii kwani Nyanja za Afya,ufugaji,misitu,utalii na maji zote zinategemea uhifadhi wa Mazingira yetu.

Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya mazingira alisema kuwa kama jamii yetu haitahifadhi mazingira basi hakuna sekta itakayofaidika na kuongeza kwamba atasimama kidete kutengeneza mikakati ya maendeleo juu ya mazingira.Pia amehaidi Serikali kutenga fedha za kutosha,kutengeneza Sera nzuri,sheria na miongozo yenye tija katika mipango ya maendeleo.

Katika upande mwingine amesema kuwa kwa sasa utaratibu wa kufufua visiki hai ni jambo ambalo litawekwa katika mpango wa maendeleo ya Taifa na kuzitaka wizara zinazohusiana na mazingira kushirikisha watu wote ikiwemo kuwapa elimu kuhusu ufufuaji wa visiki hai.

Aidha Waziri Makamba amesema kuwa serikali ina mkakati mkubwa wa uboreshaji wa Sera za Mazingira uku mkakati wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021 ukiwa bado katika mipango mahususi ya kuifanya Tanzania kuwa ya Kijani.
==========================================

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAANDAA FUTARI KWA WAFANYAZI WAKE, DAR


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, kuchukua Futari wakati wa hafla Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo katika Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 18, 2016. Kushoto ni mgeni rasmi, Sheikh Ali Hamis.
Mgeni rasmi Sheikh Ali Hamis, akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF,(hawapo pichani) wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 17, 2016. Katikati ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo, William Erio.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto) akiongozana na mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakati alipofika kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016 kwa ajili ya kumwakilisha Mufti Mkuu wa Tanzania katika Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo. Picha na Mafoto Blog

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI ZA UCHANGIAJI WA UJENZI BWENI LA MWANACHUO WA KIKE KATIKA CHUO KIKUU CHA MZUMBE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi kampeni za uchangiaji wa ujenzi wa bweni la wanachuo wa Kike.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike ambapo aliwashi mabinti kuzingatia masomo kwanza kabla ya kuingia kwenye mambo mengi.

Wanafunzi wa Chuo Cha Mzumbe wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuuu cha Mzumbe na uzinduzi wa kampeni za uchangiaji wa ujenzi wa bweni la wanachuo wa kike.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bernadetha Msigwa mwanafunzi wa chuo cha Mzumbe ambaye amepoteza uwezo wake wa kuona na anasubiri kwenda nje kwa matibabu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu chenye orodha ya majina ya wanachuo waliohitimu katika chuo cha Mzumbe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii maarufu wa kuigiza sauti za Viongozi anayejulikana kwa jina la JK Komedian

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wakati wa sherehe ya Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike Kampasi Kuu mjini Morogoro, Waliokaa kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Chuo cha Mzumbe,Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Barnabas Samatta, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Moro Mhe. Steven Kebwe na Rais wa Baraza la la Masajili,chuo kikuuu Mzumbe Bw. Ludovick Utouh
=================================================

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AKABIDHI VYAKULA VYA FUTARI KWA VITUO VINNE VYA KULEA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

JAM7






========================================

MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI

No comments:

Post a Comment