TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, June 20, 2016

WABUNGE WA KAMBI YA UPINZANI WAIBUKA NA MPYA,WAINGIA NA KUTOKA BUNGENI WAKIWA WAMEZIBA MIDOMO YAO KWA PLASTA NA KARATASI

RASIMU YA MWISHO YA MICHORO YA MPANGO MJI KABAMBE WA ARUSHA 2035 KUIDHINISHWA NA WADAU












===================================================

MTUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI ARINDIMA KATIKA MKUTANO WA OYES 2016 JIJINI MWANZA.


Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mkutano huo ulianza June 12,2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne, Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo. Na George Binagi-GB Pazzo
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (Kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola (Kulia) katika Mkutano wa OYES 2016

Mama Mchungaji, Mercy Kulola (kushoto) akiwa katika Mkutano wa OYES 2016

MAOFISA 27 WA NGAZI ZA JUU KATIKA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) WAMALIZA MAFUNZO YA KIJESHI KATIKA KAMBI YA MLELE MKOANI KATAVI.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akipokea salamu wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa maofisa 27 wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikagua gwaride la maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakati wa kufunga mafunzo yao katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) wakila kiapo cha utii wakati wa kumaliza mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani Katavi.

TANZANIA KUSHIRIKI MIAKA 65 YA JUNDOKAN KARATE 2018, NAHA CITY, OKINAWA, JAPAN.

===================================================

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA WATOTO KUPEWA ELIMU KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwasili kwenye ukmbi wa Diamond Jubilee ambapo kulikuwa na mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Aisha Sururu Bi. Aisha Sururu (kushoto) na Katibu wa Taasisi hiyo Bi. Joha Lemky wakati wa mashishindano ya kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Sehemu ya Viongozi waliohidhuria mashindano hayo ya kuhifadhi Quran
Majaji wa Mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu kwenye ukumbi wa Diamond.
Sheikh Muharami Mziwanda akitoa elimu juu ya umuhimu wa kuijua Quran kwenye mashindano ya Kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kijana mwenye ulemavu wa macho Ali Hamisi Mpemba akisoma Juzuu 30 wakati wa mashindano hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa nasaha zake mara baada ya shindano la kuhifadhi Quran lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidi mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake na mshindi wa jumla wa kuhifadhi quran juzuu 30 ,Ashura Amani (16) mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kike walioshiriki mashindano ya kuhifadhi quran kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mhagama; Tumieni nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima kukabiliana na njaa


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly kukagua shamba la mihogo la mkulima wa kijiji cha Nga’mbi wilayani humo Bahati Mtonyi (kushoto), aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa, Bahati Mtonyi, aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa (kulia kwake) Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje, (kushoto) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly na Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Brig.Jen, Mbazi Msuya, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje kukagua mashamba ya muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, jinsi gereza hilo lilivyo panda mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo wilayani Mpwapwa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akifurahia mihogo iliyovunwa katika mashamba ya wakulima kijijini Mazae wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, mara baada ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akinawishwa mikono na Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, mara baada ya kuonja chakula cha wafungwa wa gereza hilo, wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Katikati) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akishiriki kuonja chakula cha wafungwa wa Gereza la Mpwapwa wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Kulia kwake), Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje na (kushoto) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MUU)

Watanzania waaswa kujifunza mchezo wa YOGA.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika katika viwanja vya Coco kushiriki Siku ya kimataifa ya Yoga leo June 19, 2016 katikati ni Balozi wa  nchini Mhe. Sandip Aryan na kulia ni Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda. Picha na raymond Mushumbusi WHUSM

Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Watanzania wameaswa kujifunza mchezo wa Yoga ili kuimarisha miili yao na kujikinga dhidi ya matatizo mengi yanayosababishwa na mfumo wa maisha.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye mara baada ya kushiriki katika mahadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Yoga yaliyofanyika katika viwanja vya Coco.

Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa mchezo huo unatoa fursa kwa watu wa kabila, dini na mataifa mbalimbali kujumuika pamoja na kujifunza utamaduni na michezo mbalimbali. “ Yoga sio kwa jamii ya kihindi peke yake ila ni kwa ajili ya watu wote Duniani na nawashauri watanzania wenzangu tujifunze mchezo huu kwa manufaa ya afya zetu na maendeleo ya michezo nchini”.Alisema Mhe. Nnauye.

Kwa upande wake Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya ameshukuru Serikali kupitia Wizara ya abariHhhhhhahahahahwjvuajdsdhA

ISDUHDWWFUFWEGUA Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha Siku ya kimataifa ya Yoga na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi katika kuendeleza michezo nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Kabaddi ambao ni wasimamizi wa mchezo wa Yoga nchini Bw. Abdallah Nyoni amesema Siku ya kimataifa ya Yoga ni fursa kwa watanzania kujifunza mchezo huo hasa vijana ili kujenga uwezo kwa watanzania kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni juhudi za kuendeleza michezo na na kuongeza ajira nchini.

Yoga ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika falsafa ya Uhindi, hujumuisha umoja wa roho na mwili, mawazo na matendo na uelewa kati ya mwanadamu na mazingira yanayomzunguka pamoja na mtazamo wa kuijumla wa afya ya binadamu.

Desemba 11,2014,Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha mapendekezo na kukubali azimio ambalo lilitambua Juni 21 kila mwaka iwe siku ya Kimataifa ya Yoga kwa kusambaza taarifa zaidi kuhusu faidi za Yoga duniani.
==================================================

World Sickle Day June 19, 2016

No comments:

Post a Comment