TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, June 27, 2016

MKUTANO WA MASHAURIANO YA KITALAM JUU YA KUANZISHA VITUO BORA VYA UVUVI WAFANYIKA ZANZIBAR

Na Mwashungi Tahir- Maelezo Zanzibar

WAZIRI wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Hamad Rshid Muhammed, amesema ipo haja kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU kuungana kwa pamoja katika kuangalia soko la ndani katika masuala ya uvuvi ili kukuza uchumi wa nchi hizo.

Akifungua mkutano wa siku mbili wa Nchi wanachama wa Umoja wa Arika AU, wa kujadili namna ya uzalishaji wa samaki, taaluma bora ya uvuvi na namna ya kuwawezesha wavuvi, uliofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Mazizini, Hamad alisema soko la Afrika limekuwa likishuka kutokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha katika sekta hiyo.

Alisema mara nyingi nchi hizo zimekuwa zikijadili suala la kilimo kutokana na kuonekana ndio muhimu kwa jamii, lakini sasa ipo haja kuzungumzia suala la bahari kwa umuhimu wake hasa katika kukuza kipato cha wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, aliwataka Waafrika kutumia fursa zilizopo katika nchi zao katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuwapatia wadau husika elimu itakayowajengea uwezo wa kujua nyenzo ziliopo nchini ili waweze kufaidika nazo pamoja kuwashawishi kutumia masoko ya ndani kwanza kabla ya kutumia masoko ya nje.


Meza kuu ikisikiliza utaratibu wa Mkuta kutoka kwa Masta Solomon hayupo (pichani). Mkurugenzi kutoka Umoja wa Africa- Ofisi ya rasilimali wanyama Simplice Noula akitoa tarifa ya ofisi yake katika Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
Waziri wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid Muhammed akifungua Mkutano wa siku mbili wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa, uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.



Sehem ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza mgeni rasmin Waziri wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid hayupo (pichani) alipokuwa akifungua Mkutano huo.

Afisa Mkuu kiongozi wa Uvuvi kutoka Umoja wa Africa Dk. Mohamed Seisay akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Mkutano wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa.



Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa.

Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

————————————————
“Tunalo tatizo wenyewe sisi wa Afrika hatulitumii ipasavyo soko la ndani,tunahangaika masoko ya nje wakati uchumi wetu wenyewe bado haujakuwa, hivyo ipo haja kuungana wa nje na wa ndani ili tuweze kupanua soko letu kwa matumizi yetu” alisema.

Nae Mkuu wa Huduma za Wanyama na Mratibu wa Umoja wa Afrika, Simplece Novala alisema madhumuni ya kufanya mkutano huo ni baada ya kuona tatizo la soko katika samaki, ili kuweza kubuni njia zitakazosaidia kukuza soko hilo na kujipatia ajira kwa wananchi katika nchi husika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Uvuvi kutoka Tanzania bara,Fatma Sobo alisema Tanzania bado ina tatizo kubwa katika masuala ya biashara ya samaki, inatokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha, wavuvi waliopo ni wadogo wadogo, vifaa duni walivyonavyo ambavyo wanachangiwa na mabenki kuwanyima mikopo ya kuweza kujinunulia vifaa ili waweze kuvua samaki wakubwa na kuongeza kipato kwa taifa.

Hivyo, alisema kufanyika kwa mkutano huo hapa Zanzibar, utawasaidia kupata elimu ya kutosha na kuwajengea uwezo wa namna gani wataweza kuboresha huduma za msingi katika masuala mazima ya uvuvi.

Akizungumzia biashara ya samaki ya ndani ya Afrika, Fatma alisema, bado Tanzania ina tatizo la kuangalia zaidi kiwango cha samaki wanachopeleka nchi za nje badala ya kuangalia samaki wa ndani, kwani jambo hilo linapelekea kuonekana samaki wa ndani hawana ubora.

No comments:

Post a Comment