Leo, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) inayomiliki kinywaji cha Tusker, inazindua kampeni mpya kusheherekea ubora na urithi wa kinywaji hicho uliodumu tangu ilipoingia nchini mwaka 1922.
Tusker inayozalishwa Tanzania kwa vimelea asilia kwa 100% inaonyesha uasilia wa kinywaji cha Afrika kwa 100%. Kampeni hiyo itakayokuwa na hamasa za kipekee itahusisha Matangazo ya mvuto wa kipekee,Ubalozi maalumu kuwakilisha kinywaji cha Tusker na Matukio ya kipekee katika maeneo mbalimbali nchi nzima katika Promosheni maalumu itakayojulikana kama Tusker ‘Life and Soul’.
“Ikiwa ni bia ya pekee iliyokuwepo wakati Tanzania ikipata uhuru wake mwaka 1961, Kinywaji cha Tusker kimeendelea kuwa na ladha yake ya kipekee na ubora wa kipekee tangu wakati huo”, alisema Ephraim Mafuru,Mkurugenzi wa Masoko wa SBL.
Aliongeza kusema kuwa “Tusker imekuwa kinywaji bora kwa wakati wote na kimekuwa kinywaji kinachoweza kutumika katika sherehe na hafla mbalimbali huku kikitumika kuwakusanyana kuwaweka pamoja watu wenye rika na hulka tofauti katika maisha ya kila siku”,
Alisema promosheni ya kitaifa kwa wateja wote iliyomalizika hivi karibuni iliyojulikana kama ‘Tusker Milioni 500 kwa Mashabiki’ ilikuwa ya mafanikio makubwa ambapo zaidi ya watanzania 121 walijazwa mamilioni ya shilingi.
“Tunajivunia kinywaji cha Tusker ambacho kupitia promosheni hiyo kimeweza kutengeneza mamilionea ambao kwa hakika fedha hizo zimeingia katika uchumi wa Tanzania”, alisema Mafuru
Alisema kinywaji hicho pia kinajivunia udhamini wake katika shindano la Tusker All Stars ambapo Peter Msechu mwakilishi wa Tanzania alishiriki katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika Nairobi, Kenya wiki chache zilizopita.
Kwa upande wake, Meneja wa kinywaji hicho Rita Mchaki alisema “Kujihusisha kwetu katika matukio tofauti ya kihuduma katika taifa hili kunatupa ujasiri wa kujivuna na kutembea kifua mbele”.
Mchaki alisema kinywaji cha Tusker kitaendelea kusaidia mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika maeneo tofauti katika kuhakikisha jamii ya kitanzania inakuwa na maisha bora.
“Tuna furaha kushiriki na jamii ya kitanzania katika kampeni yetu mpya ambayo itaanza hivi karibuni.Tunaomba watanzania waangalie mara kwa mara matangazo yetu yatakayoanza kurushwa hivi karibuni”, alisema.
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRMF) limehamisha mechi ya kundi D ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco kutoka Casablanca na sasa itachezwa Marrakech.
Mechi hiyo itachezwa saa 1.30 jioni Oktoba 9 mwaka huu. Pia Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo ziko kundi hilo zitacheza Oktoba 9 mwaka huu na muda huo huo ili kuepuka kupanga matokeo. Mechi hiyo itachezwa jijini Algiers.
Kwa vile hakuna mashirika ya ndege ya kimataifa yanayokwenda Marrakech, FRMF ndiyo itakayogharamia usafiri wa Taifa Stars kutoka Casablanca hadi Marrakech. Kwa mashabiki wa Tanzania wanaotaka kwenda kuishangilia Taifa Stars nauli kwa ndege za Morocco kutoka Casablanca- Marrakech- Casablanca ni dola 120.
Waamuzi wa mechi kati ya Stars na Morocco watakuwa Gassama Bakary, Jawo Dickory, Touray Sulayman na Camara Bakary, wote kutoka Gambia. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Zoumaro Gnofame kutoka Togo.
Kocha Jan Poulsen anatarajia kutangaza kikosi Septemba 26 mwaka huu kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco na kitaingia kambini Septemba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment