Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo,(kulia) akifafanua jambo kuhusu Tamko la Serikali juu ya Hatma ya Wanafunzi waliofutiwa Matokeo ya Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2011, kushoto ni Kaimu Kamishina na Mkuu wa Idara ya Sekondari, Charles Philemoni, iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Elimu Dar es Salaam leo.(Picha na Shaaban Mpalule).
Serikali leo imetoa tamko la hatma ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi 2011, iliyofanyika makao makuu ya wizara ya Elimu Dar es Salaam leo, akizungumzia sakata hilo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema kuwa kati ya wanafunzi 983 545 ya waliofanya mitihani, 567,767 sawa na asilimia 58.28 wamefaulu mtihani huo, na kwamba kati ya wanafunzi 9,736 wamefutiwa matokeo kutokana na kubainika kufanya udanganyifu
No comments:
Post a Comment