Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwa katika viwanja vya Ikulu leo mara baada
ya kumaliza kazi ya kuwaapisha mawaziri na manaibu waziri wapya
aliowateua hivi karibuni, Mwandishi wetu ameshuhudia tukio hilo kwenye
viwanja vya Ikulu leo
Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba akihojiwa na mtangazaji wa BBC mara baada ya kuapishwa leo.
Rais Dk Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa watoto walliohudhuria na
wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa kwa mawaziri
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerari
Davis Mwamunyange kushoto ni Waziri wa Ulinzi Shamsi Vuai Nahodha
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mukangara akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete leo.
Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba akila kiapo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki akila kiapo
Mwandishi wandamizi wa Magazeti ya Mwananchi Communication Bathoromeo
Mkinga akisaidia mzee Sabodo kuelekea katika eneo la kukaa wageni
waalikwa, kushoto ni Waziri wa Wanawake Jinsia na Watoto Mh. Sophia
Simba.
Ridhiwan Kikwete akizungumza na aliyekuwa rais wa Yanga Jamal Malinzi wakati wa hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo. |
Miraji Kikwete akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo
Rais Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na mawaziri pamoja na manaibu waziri mara baada ya kuwaapisha leo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na manaibu Waziri mara baada ya kuwaapisha leo Ikulu.
RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA ATINGA KIZIMBANI KUTOA USHAHIDI KATIKA KESI YA BALOZI MAHALU
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akitoka katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kutoa ushahidi
wake katika kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini
Italia, Profesa Costa Mahalu, anayekabiliwa na shtaka la uhujumu
uchumi.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akiondoka Mahakama hapo baada ya kutoa ushahidi wake.
WABUNGE WA CHADEMA WADAI KUTOKUBALIANA NA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
NA PAULINE KUYE -NJOMBE
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo hakijakubaliana na baraza la Mawaziri
ambalo limeapishwa leo na Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete.
katika
Mkutano wa hadhara uliofanyika Mkoa mpya wa Njombe kwenye uwanja wa
polisi Makambako uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na viongozi
mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Iringa mjini Mheshiwa Peter
Msigwa, Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mbunge wa Mbozi
Magharibi ambaye pia ni katibu wa CHADEMA Tanzania Mheshimiwa David
Silinde,wamesema uteuzi huo mpya wa baraza la mawaziri uliofanywa mei 4
mwaka huu sio suluhisho la matatizo ya Watanzania.
Kwa
upande wake Silinde amesema kuwa, kinachotakiwa kifanyike ni
kubadilisha mfumo mzima na wale wote ambao wametajwa kwamba ni wezi wa
mali za umma waende jela na wafilisiwe na si kuachwa bure.
Naye
Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa Chama cha mapinduzi ni ukoo mmoja,
wote wanafanana kitabia, kwa kubadilisha Baraza la Mawaziri kutoka
nafasi moja kwenda nyingine haiwezi kusaidia kutatua ubadhilifu wa mali ya umma kwani bado ukoo ni ule ule.
Katika
ziara hiyo matawi matatu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo pamoja na
ofisi moja ya kata ilizinduliwa, huku zaidi ya wanachama wapya 600
walijiunga na chama cha CHADEMA
MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU NNE YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUMI NA BIASHARA MKOANI RUKWA LEO
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na washiriki wa
semina hiyo leo wakati akifungua mafunzo hayo rasmi yaliyoandaliwa na
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kuratibiwa na
Klabu ya Waandishi wa Habari ya Rukwa (Rukwa Press Club). Mafunzo hayo
yatadumu kwa muda wa siku nne na jumla ya washiriki 18 kutoka vyombo vya
habari tofauti vya Mikoa ya Rukwa na Katavi wanashiriki. Katika maneno
yake ya ufunguzi Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka waandishi wa habari wa
Rukwa kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi yao vizuri kutangaza vivutio na
fursa zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa wadau ili kuvutia wawekezaji.
Muwezeshaji
wa mafunzo hayo Ndugu Mnaku Mbali ambaye ni Muhariri wa gazeti la
Business Times la jijini Dar es Salaam. Lengo kubwa la mafunzo hayo
alisema ni kuwajengea uwezo zaidi waandishi wa Rukwa waweze kuandika
habari za biashara na uchumi katika uelewa chanya kwa maendeleo ya jamii
ya Rukwa na Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi
na muendeshaji wa Blog ya Pembezoni Kabisa ambaye pia ni mwandishi wa
gazeti la Mwanachi Mussa Mwangoka kulia na Joshua Joel wa ITV na Radio
One wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wengine kutoka Rukwa na Katavi wanaoshiriki mafunzo hayo. Wapili kulia ni mdau Ernest Kibada kutoka Katavi.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya leo.
MAMA TUNU PINDA APOKEA MICHANGO YA SH. 16M/-
Mke
wa Waziri Mkuu Tunu Pinda pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta Rose
Mkissi wakipokea vifaa vya michezo kwa ajili ya timu ya taifa ya
Netiboli- Taifa Queens kutoka kwa Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom
Bw. Salum Mwalim. Vodacom imeipatia Taifa Queens vifaa mbalimbali
vyenye thamani ya Shilingi Milioni Sita kuwezesha ushiriki mzuri wa timu
hiyo kwenye mashindano ya Afrika yanayoanza kesho (Jumanne Mei 8, 2012)
jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano Shiza Mwakatundu.
MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda leo amepokea
michango kutoka kwa kampuni za Vocacom na Zantel ikiwa ni mwitikio wa ombi lake
kwa Watanzania kuwaomba waichangie timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens).
Mama
Tunu Pinda amepokea vifaa vya michezo kwa ajili
ya mashindano kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania vyenye thamani ya sh.
milioni sita. Vilevile, Mama Pinda amepokea simu za mkononi 300 zenye simcard na muda wa maongezi kwa ajili ya
wachezaji na viongozi wao kampuni ya Zantel zenye thamani ya sh. milioni 10/-.
Makabidhiano hayo yalifanyika leo mchana (Jumatatu, Mei
7, 2012) kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo hiyo, Meneja
Mahusiano ya Nje wa VODACOM, Bw. Salum Mwalimu alisema wameitikia wito wa Mama
Pinda wa kuichangia timu ya Taifa Queens kwa sababu wametambua umuhimu wa kuiunga
mkono timu hiyo.
“Vifaa tulivyotoa ni jezi 20, tracksuit 20, raba pea
20 na bibs 20… tuna imani timu yetu ya taifa itaweza kupenya hadi ngazi ya
fainali,” alisema.
Naye Meneja Biashara wa Zantel, Bw. Ahmed Mokhles akikabidhi
simu hizo, alisema wametoa mchango huo kwa sababu wanaamini kwamba japokuwa
watakuwa hapa nchini, wachezaji na maafisa wao wana haki ya kuwasiliana na
familia zao.
“Kwa kutambua hilo, tumetoa simu 300 zenye muda wa maongezi
ambapo mtu akiongeza muda wa maongezi, ataongezewa muda mwingine wa sh. 10,000/-
kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu.”
Pia Zantel walitoa router
mbili kwa ajili ya ofisi za Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) ili ziweze
kuwasadia katika mawasiliano yao ya internet.
Mama Tunu Pinda aliwashukuru makampuni yote mawili kwa
michango yao, na akatumia fursa hiyo kuwashukuru zaidi Watanzania waliojitokeza
kwa wingi kuchangia mashindano hayo.
Akitoa ufafanunuzi kuhusu michango ambayo imekwishatolewa
hadi sasa, Mama Pinda alisema jumla ya sh. 178,230,000/- zimekwishapokelewa
hadi sasa zikiwa ni fedha taslimu na vifaa. Kati ya hizo, sh. milioni 114.8 ni
fedha taslimu na sh. milioni 53.4 ni vifaa vilivyotolewa na wadau mbalimbali
kuchangia mashindani hayo.
Alisema bajeti nzima ilikuwa sh. 158,439,000/- ambapo
sh. 82,656,000 zilikuwa ni gharama za kuendeshea kambi ya maandalizi ya timu ya
Taifa Queens na sh. 75,780,000/- zilikuwa ni kwa ajili ya kuendesha mashindano
yanayotarajiwa kuanza kesho.
Tanzania kupitia CHANETA imepewa heshima ya kuandaa Mashindano
ya Netiboli ya Kombe la Afrika ambayo yanatarajiwa kuanza kesho saa 8 mchana (Jumanne,
Mei 8-12, 2012). Mashindano hayo yanayojumuisha nchi saba za Botswana, Lesotho,
Zimbabwe, Zambia, Uganda, Malawi na Tanzania yatafunguliwa na Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete.
Ziara ya Rais Dk. Mohamed Shein Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akipokea taarifa ya kazi za utekelezaji
wa Mkoa wa Kusini Unguja,kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Abdalla
Mwinyi Khamis, leo alipoanza ziara yake na kutembelea miradi mbali
mbali ya maendeleo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akipokea taarifa ya kazi za utekelezaji
wa Mkoa wa Kusini Unguja,kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Abdalla
Mwinyi Khamis, leo alipoanza ziara yake na kutembelea miradi mbali
mbali ya maendeleo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe aliofuatana nao wakitoka
kuangalia mnara wa Redio ulioanza kufungwa na kampuni ya Ujenzi ya
Minara ya New Techinical Contractors Company ya Dar es Salaam,chini
Injinia Stivin Makange,(mwenye tai)huko Bungi Wilaya ya kati Unguja
leakiwa katika ziara ya Moa wa Kusini Unguja.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe aliofuatana nao wakitoka
kuangalia mnara wa Redio ulioanza kufungwa na kampuni ya Ujenzi ya
Minara ya New Techinical Contractors Company ya Dar es Salaam,chini
Injinia Stivin Makange,(mwenye tai)huko Bungi Wilaya ya kati Unguja
leakiwa katika ziara ya Moa wa Kusini Unguja.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Afia Tawala wa Mkoa wa Kusini Unguja Sabri Mohamed,akisoma
taarifa ya Mkoa wa Kusini Unguja,mbele ya Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipowasili
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini huko Tunguu,katika ziara ya kutembelea
maendeleo ya miradi mbali mbali ya Mkoani humo iliyoanza leo.[Picha
na Ramadhan Othman,Ikulu.]
taarifa ya Mkoa wa Kusini Unguja,mbele ya Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipowasili
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini huko Tunguu,katika ziara ya kutembelea
maendeleo ya miradi mbali mbali ya Mkoani humo iliyoanza leo.[Picha
na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar,walioshiriki katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakisikiliza kwa Makini
taarifa ya Mkoa wa Kusini Unguja iliyosomwa na Afisa Tawala wa Mkoa
Sabri Mohamed (hayupo pichani).[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Zanzibar,walioshiriki katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakisikiliza kwa Makini
taarifa ya Mkoa wa Kusini Unguja iliyosomwa na Afisa Tawala wa Mkoa
Sabri Mohamed (hayupo pichani).[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipata maelezo kutoka wa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari Utamadunu na Michezo Ali Mwinyikai alipotembela eneo
jipya linalojengwa Mnara wa Redio wa kurushia matangazo huko Bungi
Wilaya ya Kati Unguja,alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini
leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipata maelezo kutoka wa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari Utamadunu na Michezo Ali Mwinyikai alipotembela eneo
jipya linalojengwa Mnara wa Redio wa kurushia matangazo huko Bungi
Wilaya ya Kati Unguja,alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini
leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mzanzibar anayeishi nje
ya Nchi Dr. Ferouz Jafferji,alipowasili katika Skuli ya Sekondari ya
Unguja Ukuu alipotembelea madarasa ya kusomea yaliyokarabatiwa na
umoja wa Diyasphora pamoja na kuweka jiwe la msingi nyumba ya
Madaktari iliyopo Jirani na Skuli hiyo leo,akiwa katika ziara ya
Mkoa wa Kusini Unguja iliyoanza janakutembelea miradi mbali mbali ya
maendeleo katika ya Mkoa huo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mzanzibar anayeishi nje
ya Nchi Dr. Ferouz Jafferji,alipowasili katika Skuli ya Sekondari ya
Unguja Ukuu alipotembelea madarasa ya kusomea yaliyokarabatiwa na
umoja wa Diyasphora pamoja na kuweka jiwe la msingi nyumba ya
Madaktari iliyopo Jirani na Skuli hiyo leo,akiwa katika ziara ya
Mkoa wa Kusini Unguja iliyoanza janakutembelea miradi mbali mbali ya
maendeleo katika ya Mkoa huo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
SERIKALI YATAKIWA KUINGILIA KATI MGOGORO WA MAJI KATI YA DAWASCO NA WAKAZI WA MALAMBA MAWILI MBEZI
WAKAZI wa
Malamba Mawili Mbezi jijini Dar es Salaam, wameitaka serikali
kuingilia kati mradi wa maji katika eneo lao, baada ya Mamlaka ya Maji
safi na Maji Taka (DAWASO), kushindwa kutekeleza ahadi yake.
Wamefikia maamuzi
hayo baada ya mamlaka hiyo kukutana na wakazi pamoja na uongozi wa
eneo hilo ikiwataharifu kwamba inatarajia kujenga visima viwili vya maji
safi na kuvikabidhi kwao ifikapo Aprili mwaka huu bila mafanikio.
Akizungumza na Fullshangweblog jana Mwenyekiti wa eneo hilo Said Bakari alisema kuwa
anashangazwa na hatua ya Dawasa kukutana na wananchi wakiwemo
viongozi kwa madai ya kutatua tatizo la muda mrefu linalolikabili eneo
hilo na kuwatelekeza.
Alifafanua kuwa
kabla mamlaka aijakutana na wakazi hao , awali ilikutana na uongozi wa
eneo hilo na kuwapa semina ya siku .. kwa lengo la kuutambulisha mradi
kwa wananchi huku kwa maelezo kwamba tatizo hilo litatatuliwa ikiwa ni
pamoja na kuboresha miundombinu yake.
Alichanganua kuwa
maelezo ya awali waliyopewa na shirika hilo yalisema fedha
zitakazotumika kuchimbia visima hivyo ni kutoka katika mfuko wa Rais wa
Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete jambo ambalo
halijatekelezwa hadi sasa.
“Dawasa
walituahidi kutuchimbia visima viwili vya maji, ila kwa sasa wamechimba
kimoja na hicho hakitoi maji bali kimekaa na wala hakuna dalili za
muendelezo wa zoezi hilo, hivyo basi ikiwa walidhamiria kututatulia
tatizo la maji ni bora wangekamilisha malengo yao kuliko kutuacha njia
panda tusijue la kufanya wala sehemu ya kwenda”, Bakari.
Vile vile
anafafanua kuwa kikao kilichowakutanisha viongozi wa eneo hilo na
Shirika kilifanyika kabla ya Desemba mwaka jana huku kile
kilichowahusisha wakazi hao kilifanyika 31mwishoni mwa mwaka huo
kikitambulisha juu ya kuwepo kwa mradi huo.
“Sisi viongozi
wahusika akiwemo Diwani wa Kata hii hatujui gharama zitakazokamilisha
mradi huo mpaka kukamilika kwake, kitu ambachop kinatupa wasiwasi hasa
tunapotakiwa kutoa ufafanuzi na wananchi”.
Naye Ofisa
Uhusiano wa Dawasa Mery Msuya alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya mradi
huo, awali alilitaka gazeti hili kufika ofisini kwao, hata hivyo, siku
iliofuata alisema "Kwa sasa haitakuwa rahisi kwa kuwa niko njiani
nikielekea kwenye mkutano Ubungo Plaza" alisema Msuya.
SERIKALI YATAKIWA KUWSHIRIKISHA WAFUNGWA KATIKA KUPIGA KURA
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imetakiwa
kuwashirikisha wafungwa katika mchakato mzima wa kupiga kura, ikiwa ni
pamoja na kuwawezesha kupata haki ya kukutana na wenzi wao hasa
wanapokuwa kifungoni.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Chama cha
kurekebisha Mwenendo wa Watu waliomaliza Kifungo Tanzania (ERST),Dk.
Alfred Kaaya alisema kwamba kuna haja ya serikali kushirikiana na chama
hicho ili kusaidia kupunguza wimbi la uhalifu nchini.
Kaaya alisema kuwa
kitendo cha serikali kutolishirikisha kundi hilo itakuwa haijawatendea
haki hususan katika mchakato mzima wa upigaji kura sambamba na katiba
mpya.
“Wajibu wa serikali ni
kubadili mfumo wa magereza kutoka sheria ya mkoloni, ili kufuata sheria
ambazo sio kandamizi zenye malengo ya kufunza zaidi, sanjari na elimu
bora kwa watoto wanaoingia gerezani.
Vile vile alisema
lengo la chama hicho ni kuwaunganisha wafungwa waliomaliza kutumikia
vifungo vyao pamoja na kuwarekebisha kitabia sanjari na kusimamia haki
zao zilizosahaulika.
Hata hivyo
alichanganua kuwa chama kina mkakati wa kuwafungulia miradi mbalimbali
wafungwa waliomaliza vifungo ili waweze kutumia ujuzi wao kwa manufaa ya
jamii inayowazunguka.
“Lengo letu ni
kuwaanzishia miradi mbalimbali itakayowapatia ajira na kupunguza uhalifu
unaoweza kuwarudisha gerezani tena, hata hivyo jamii ielewe kwamba
kuwapokea watu hawa ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha katika shughuli za
maendeleo itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza uhalifu ndani ya
jamii yetu”.
Mbali na hayo
alibainisha kwamba chama hicho kina zaidi ya wanachama 182 huku kikiwa
na miradi mbalimbali ikiwamo upasuaji mbao na uselemala.
Kwa kiasi kibwa chama
hicho kimeweza kusimama baada ya kupatiwa msaada wa shl. milioni 100 na
Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP Leginald Mengi mwaka 2009.
MGOGORO WAFUKUTA UCHAGUZI JUMUIYA YA WAZAZI KATA YA NDUGUMBI KINONDONI
Na Mwandishi Wetu
UCHAGUZI wa viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tawi la Vigaeni, Kata ya Ndugumbi Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, unafukuta kutokana na kudaiwa kuwa na mchezo mchafu.
Uchaguzi huo bado haujajulikana utafanyika lini, ingawa zoezi la urudishwaji wa fomu za wagombea ulishakamalika tangu Jumapili iliyopita.
Baadhi ya wanachama wa jumuiya hiyo, wamesema zoezi la uchaguzi wa viongozi wao unaonekana kuwa katika zengwe kutokana na kurudishwa kwa majina ya wagombea.
Wanachama hao walidai kuwa kurudishwa kwa fomu ya mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Tawi la Vigaeni (jina linahifadhiwa) kunatokana na kutakiwa kuwepo kwa majina ya 'wateule' wao.
"Unajua kuwa kuna mambo ambayo hata hatuyaelewi kabisa, kwa mfano jina la mgombea wa nafasi ya mwenyekiti limetakiwa kurudi kisa liko moja, na mgombea hawezi kuwa peke yake," alisema mmoja wa wanachama hao.
Wakizungumza kwa nyakatio tofauti, wanachama wa tawi hilo wamedai kuwa kuwepo kwa tofauti ya jina moja kuondolewa, huku nafasi ya katibu ikiwa na mgombea mmoja, sambamba na nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu kata.
lilipowasiliana na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Tawi la Vigaeni, lilijibiwa kuwa katibu huyo hayupo kazini kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Mmoja wa wafanyakazi wa ofisi hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Shida, alisema yeye si msemaji, na kumtaka mwandishi kuwasiliana na katibu, ambaye kwa wakati huo alidai yuko nyumbani kwake na anaumwa.
Tawi hilo linadaiwa kufukuta kutokana na baadhi wa wagombea kuwekewa kauzibe kwa vigezo vya kutokuwa wakazi, kitu ambacho kinavumishwa ikidai kuna mbinu kwa baadhi ya watu kutakiwa kushika baadhi ya nyadhifa.
Hata hivyo, wagombea wote wa nafasi tofauti walizoomba wamefanyiwa usaili jana, huku nafasi ya mwenyekiti ikitakiwa kutafutiwa mpinzani, baada ya awali kuwasilishwa jina moja hadi siku ya mwisho ya kurudisha fomu iliyokuwa Mei 6.
Speaker Makinda attends the seventh Meeting of the East African Speakers Bereau in Kigali Rwanda
Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda arrives
at the Rwandan Parliament to attend the seventh Speakers bereau of the
East African Countries.. On her left is the EALAs Speaker Hon. Abdi
Rahim
Photo by Owen Mwandumbya
Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda greats
Hon. Ntawukuliryayo Jean Damascene, President of the Sanate of Rwanda
when she arrives at the Rwandan Parliament to attend the seventh
Speakers bereau of the East African Community today.
Hon. Ntawukuliryayo Jean Damascene, President of the Sanate of Rwanda
presents a gift to the Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon.
Anne Makinda when she arrives at the Rwandan Parliament to attend the
seventh Speakers Bureau of the East African Community today.
Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda leads her
countermets from EAC Member state to pray for the strong EAC
intergration before the start of the seventh Speakers beareau of the
East African Community today.
Chairman of the East African Speakers Bureau Hon. Rose Mukantabana,
Speaker of the Rwandan Parliament welcomes the speakers from EAC members
states after the officail opening of the one day meeting of the seventh
meeting of the Speakers Bureau of the East African Community today. On
her right is Hon. Abdi Rahim Speaker of the EALA and on her left is
Hon. Rebecca kadaga, speaker of the Ugandan Parliament.
KAMPUNI YA SEMES YAJIDHATITI KUOKOA WANAWAKE ARUSHA
NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA
KAMPUNI ya Semes ya jijini la Arusha imeweka mikakati ya
kuhakikisha kuwa inawaakomboa wanamke wa
nchi ya Tanzania kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali sanjari na kuwapatia mitaji ili iwawezeshe kujikwamua
kiuchumi.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Elias Seme
alipokuwa katika sherehe za kuzindua kikundi cha kampuni hiyo jijini hapa
Alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa wanawake wanaondokana na
hali ya utegemezi kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa
kipaumbele katika kuwakomboa kwa kuwapatia mitaji mbali mbali .
Alieleza kuwa mwanamke ndie mwenye huruma na ana uwezo wa
kupangilia mipango zaidi ya wanaume hivyo wanayo fursa kubwa ya kuwezeshwa ili
waweze kujikwamua kiuchumi
Bw Seme aliongeza kuwa kampuni hiyo tayari.imeshatoa mitaji
ya shilingi milioni tano kwa mwaka huu ambapo pia wameweza kuanzisha vikoba
kwa lengo la kukopeshana ili kuboresha
maisha yao
Aliongeza kuwa mbali na hayo kampuni hiyo imefanikiwa kutoa ajira kwa
vijana 21 ambapo lengo halisi ni kuweza kutoa ajira kwa watu
50-60 kwa mwaka .
Akielezea changamoto inayoikabili kampuni hiyo alisema kuwa
ni pamoja na ushindani wa kibiashara ambapo kumekuwepo na makampuni mengi
kutoka nchi ya nje yanayohusiana na
maswala ya usafi hivyo kuwepo na
upinzani mkubwa.
Alitaja mikakati waliyonayo kuwa ni pamoja na kuongeza
vitega uchumi zaidi na kujiboresha ili iweze kujiongezea mapato zaidi ili
kuwawezesha vijana wengi kujipatia ajira.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda awasili Kigali jana Usiku kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda awasili Kigali Rwanda kuhudhuria
Mkutano wa saba wa Maspika wa Mabunge wananchama wa Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Hapa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili jana katika Uwanja wa
Ndege wa Kigali baada ya kupokelewa na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la
Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (kulia). Mhe. Makinda
yupo Kigali Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge
wananchama wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo
Picha na Owen Mwandumbya
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza na
Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana mara baada
ya Kuwasili Mjini Kigali kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa
Mabunge wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika
leo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipata
maelezo ya awali kuhusu Mkutano huo kutoka kwa maafisa wa Bunge la
Tanzania. Wa kwanza Kushoto ni Bi. Justina Shauri , Afisa Dawati wa
Bunge la Afrika Mashariki kutoka
Bunge la Tanzania na Ndg. Charles Mloka, Mkurugenzi wa Kamati za Bunge
anayemuwakilisha Katibu wa Bunge katika Mkutano huo.
Mhe. Makinda na Mwenyeji wake wakiondoka Uwanja wa Ndege mara baada ya Kuwasili.
TGNP YAWANOA WANAHARAKATI TOKA MIKOANI KATIKA MBINU ZA URRAGHBISHI
Mchoraji wa katoon magazeti ya The Guardian Muhidin Msamba,
akimsawadia Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Zawadi ya picha ya kuchora
wakati wa mafunzo hayo.
Leo TGNP imezindua warsha ya uraghbishi ya wiki moja
kwa wanaharakati kutoka mikoani pamoja na Dar es Salaam, ili kunoa
uwezo wao wa kufanya kazi na jamii husika kuibua masuala nyeti
katika jamii hizo zikiwemo mafanikio na changamoto, kuchambua visababishi
vya matatizo au mafanikio hayo kwa kina na kupanga mikakati ya
kushughulikia kero hizo pamoja na wanajamii .
Warsha hiyo inalenga kuimarisha uelewa wa pamoja wa mtizamo
ya kiitikadi kuhusu dhana za ukombozi wa wanawake
kimapinduzi na makundi yaliyoko pembezoni na kuitekeleza
kwa vitendo; kujenga uelewa wa pamoja kuhusu
uraghbishi na mbinu shirikishi zinazotumika katika
uraghbishi, kuongeza uelewa wa kampeni ya hiaki ya uchumi
katika kudai kazi zenye heshima utu na kipato, uhifadhi wa kumbukumbu,
mbinu za mawasiliano na uwezo wa kuvitumia katika Ujenzi
wa Vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika ngazi ya
kanda.
Wawezeshaji wa warsha hiyo ni Bw. Richard Mabala
Mkurugenzi wa TAMASHA ambayo ni asasi ya kiraia iliyobobea
katika kuwawezesha vijana na jamii kwa ujumle kutumia mbinu
za uraghbishi kama chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii
husika. Bw. Winston Chuchil Mkurugenzi Msaidizi wa TAMASHA ni
mwezeshaji mwenza ambaye naye pia amebobea katika mbinu za uraghbishi.
Washiriki wa Warsha hiyo wametoka katika mikoa ya Shinyanga, Morogoro,
Arusha, Dodoma, Mwanza , Mbeya, Dar es Salaam na Pwani wakiwakilisha
asasi mbalimbali za kiraia ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kuleta
mabadiliko chanya katika jamii za mikoa husika.
Baada ya warsha washiriki wakishirikiana wanajamii na
TGNP wataendesha zoezi la uraghbishi katika mikoa husika ambapo
watatumia mbinu mbali mbali za uraghbishi katika kuibua
masuala nyeti yanayogusa jamii husika, kuyachambua kwa kina ili kupata
kiini cha matatizo au mafanikio, hayo na kutafuta mbinu
mbali mbali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo, mbinu zitakazotumika,
nani atafanya nini kuanzia ngazi binafsi, jamii na taifa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Saudi Arabia
nchini, Hani Abdullah Mominah kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake
jijini Dar es salaam May 7, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Nchini,
Hani Abdullah Mominah, ofisini kwake jijini Dar es salaam May 7, 2012.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
41,733 WASHUHUDIA MECHI YA SIMBA, YANGA
Watazamaji
41,733 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyochezwa jana (Mei 6
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh.
30,000 VIP B na sh. 40,000 VIP A. Watazamaji 36,980 walinunua tiketi za
sh. 5,000 wakati 203 walikata za sh. 40,000.
Mechi
hiyo ambayo ni moja kati ya saba zilizochezwa siku hiyo kufunga msimu
wa 2011/2012 iliingiza sh. 260,910,000. Kila klabu ilipata sh.
62,646,395.85. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh.
39,799,830.51 wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
lilipata sh. 19,908,361.95.
Gharama
za mechi kabla ya mgawo ni nauli ya ndani ya waamuzi na kamishna sh.
20,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, mwamuzi wa akiba sh.
30,000, gharama za tiketi sh. 8,539,950, maandalizi ya uwanja (pitch
preparation) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi wa uwanja
sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Mgawo
wa uwanja ni sh. 19,908,361.95, gharama za mechi sh. 19,908,361.95,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 9,954,180.97, Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,990,836.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 10,467,324.78.
Kumbukumbu
SLEYUM MOHAMED ZAHOR (1922-2003)
HATIMAYE leo umetimiza miaka tisa tangu ulipofariki dunia mwaka 2003
baada ya kuugua kwa muda mrefu na kuzikwa katika makaburi ya Kigilagila,
Kiwalani, Dar es Salaam.
Kifo chako kimetuachia pengo na upweke mkubwa. Tunazikosa simulizi zako, maono yako, ucheshi wako, busara zako na hekima zako.
Unakumbukwa sana na mke, Bibi Fatuma Rashid na watoto wako, Rashid, Pili, Amisa, Shani, Asha, Saumu, Nuru na Hilali pamoja na wajukuu zako wote.
Hakika sisi zote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake lazima tutarejea. Tunaamini maandiko ya kwamba kila chenye roho, lazima kitaonja mauti.
Mungu ailaze roho yako mahali pema, peponi. Amin
Kifo chako kimetuachia pengo na upweke mkubwa. Tunazikosa simulizi zako, maono yako, ucheshi wako, busara zako na hekima zako.
Unakumbukwa sana na mke, Bibi Fatuma Rashid na watoto wako, Rashid, Pili, Amisa, Shani, Asha, Saumu, Nuru na Hilali pamoja na wajukuu zako wote.
Hakika sisi zote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake lazima tutarejea. Tunaamini maandiko ya kwamba kila chenye roho, lazima kitaonja mauti.
Mungu ailaze roho yako mahali pema, peponi. Amin
Uongozi wa azam waipongeza timu yao kwa kuibuka washindi wa pili ligi kuu ya Vodacom
Makamu Mwenyekiti wa timu ya AZAM FC.Bw Said Mohamed akitoa hotuba jana
katika ukmbi wa hoteli ya JB Belimont jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuipongeza timu
ya Azam Fc kwa kuwa mshindi wa pili wa ligi kuu ya Vodacom .
Kocha wa Azam Fc Bw;John Stewart Hall.nae akitoa msisitizo katika hafla hiyo
Katibu mkuu wa Tff Bw;Angetile Osiah akisisitiza jambo katika hafla ya kuipongeza timu ya Azam Fc.
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage nae akisisitiza jambo katika hafla hiyo.
Mtangazaji wa Radio One .Bw. Omari Katanga akikabidhiwa Tuzo na Mbunge
wa Kinondoni Idd Azan kwa kuwa mmoja wa waandishi bora wa michezo Tuzo
hizo zilitolewa na
uongozi wa klabu ya Azam wakati wa hafla ya kuipongeza timu ya Azam Fc
kwa kuwa mshindi wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Mkurungenzi wa michezo katika wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Bw. Leonard Thadeo katikati akimsikiliza Mbunge wa Kinondoni Idd Azan wakati wa hafla hiyo kushoto ni makamu mwenyekiti wa Azam FC Bw Said Mohamed
No comments:
Post a Comment