Posted: 08 May 2012 12:48 AM PDT
Na Agnes Mwaijega
KITUO
cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), kwa mara ya kwanza kimeikabidhi Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) cheti cha usimamizi bora wa uchaguzi katika
Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha. Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ofisa Utawala TCIB, Bi.Deborah
Mushi, alisema pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi
huo, bado NEC ilijitahidi kusimamia uchaguzi huo vizuri. Bi.
Mushi alisema kwa mujibu wa ripoti yao ya utafiti uliofanyika wakati wa
mchakato mzima wa uchaguzi, NEC iliendesha uchaguzi ambao ulikuwa huru
na haki. "Kwa asilimia 70 NEC ilijitahidi kufanya kazi yake
vizuri na ndiyo maana tumeamua kuipa cheti maalumu cha usimamizi mzuri
katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki," alisema. Hata hivyo alitoa
mwito kwa tume hiyo kuhakikisha inachukua hatua kali dhidi ya wale wote
waliotumia lugha ya matusi katika kampeni za uchaguzi huo. "Mimi
nadhani kwa upande mwingine ni wajibu wa NEC kuhakikisha inaajiri
watendaji wengi watakaosimamia suala la maadili katika chaguzi kwa ngazi
zote za serikali kuanzia kata hadi taifa," alisema. Alisema kuna
umuhimu wa Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa elimu endelevu kwa
wasimamizi wa masuala ya uchaguzi kwa kuanzisha vipindi maalumu kwa
ajili ya mafunzo na si kusubiri hadi wakati wa uchaguzi. Bi.
Mushi alitoa mwito kwa Serikali na NEC kuhakikisha zinatoa ruzuku
inayostahili kwa vyama vyote vya siasa ili viweze kushiriki kikamilifu
katika chaguzi. Kwa kipindi kirefu NEC imekuwa ikilaumiwa kwa
kushindwa kusimamia uchaguzi. Hatua ya NEC kupata cheti hicho
inatafsiriwa kuwa inachangiwa na uongozi mpya wa tume.
|
Posted: 08 May 2012 12:43 AM PDT
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, akiwasili eneo la
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana, ili kutoa ushahidi
ya kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia,
Profesa Victor Mahalu na aliyekuwa Ofisa Utawala wa Ubalozi huo, Bi.
Grace Martin, wanaokabiliwa na mashitaka ya kuhujumu uchumi na
kuisababishia Serikali, hasara ya zaidi ya Euro Mil 2. (Picha na Prona
Mumwi)
|
Posted: 08 May 2012 12:40 AM PDT
|
Posted: 08 May 2012 12:39 AM PDT
Rais
Jakaya Kikwete (kushoto), akimwapisha, Fenera Mkandara, kuwa Waziri
mpya wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ikulu Dar es Salaam jana.
(Picha na Nyakasagani Masenza)
|
Posted: 08 May 2012 12:31 AM PDT
Wakazi
wa jiji ambao majina na kazi wanazofanya (havikufahamika), walikutwa na
kamera yetu kando ya makutano ya Barabara za Msimbazi na Uhuru, Dar es
Salaam jana, wakiwa wameshikana mashati baada ya kutokuelewana katika
shughuli zao. (Picha na Rajabu Mhamila)
|
Posted: 08 May 2012 12:27 AM PDT
Ili
kukabiliana na tatizo la ulanguzi wa tiketi za usafiri wa boti ziendazo
visiwani Unguja na Pemba, baadhi ya mawakala wenye ofisi zilizopo Feri,
Posta jijini, wamechora bei halisi ya nauri katika kuta za ofisi zao,
kama zinavyoonesha katika picha iliyopigwa, Dar es Salaam jana. (Picha
na Charles Lucas)
|
Posted: 08 May 2012 12:24 AM PDT
Na Mwandishi wetu
IMEELEZWA
kwamba Taasisi ndogo ndogo zinazotoa mkopo nchini zipo katika hatari ya
kufilisika kutokana na mazingira hali yalisi ya maisha. "Hali
hii ni hatari kwa taasisi hizi kwani ipo hatari ya kuongezeka kwa
mikopo na kusababisha taasisi hizo kufilisika,"alisema Bw. Joel Mwakitalu, Mwenyekiti Makamu wa Tanzania Chama Taasisi za Fedha nchini (TAMFI). Alisema
duniani kote, mfumo wa kukopesha kwa kikundi ni mbinu bora kwa ajili
ya kuendeleza mikopo kwa maskini ambao hawana dhamana kwani wanatakiwa
kupata mikopo kutoka tawala na mabenki. Bw. Mwakitalu alisema
hivi karibuni alisikia katika vyombo vya habari kuwa vikundi
vinavyochukua mkopo vipo katika hali ngumu kutokana na mabadiliko ya
maisha,ukuaji wa miji ,changamoto na kuongezeka kwa watoa mikopo. kundi mikopo mbinu ilikuwa kuwa gumu kutokana na mabadiliko maisha, ukuaji wa miji changamoto na kuongezeka kwa watoa mikopo. "Mabadiliko ya maisha, ukuaji wa miji changamoto na kuongezeka kwa mikopo ni baadhi ya mambo kuchochea hatari ya kufilisika kwa taasisi hizo Alisema
baadhi ya sababu zinazochangia taasisi hizo kufilisika mfumo mbaya wa
ukopeshaji ambapo kuna mapungufu katika sheria na sera za serikali
gharama za maisha majanga matumizi mabaya ya fedha , matatizo ya
kifamilia na shinikizo. Wadau katika mjadala huo waliaafiki kuwa
watu wanaokopa kuanzia sh.milioni marejesho yake si mazuri
ukilinganisha na wanaochukua chini ya hapo . wakakubaliana naye kuhusu
hatari ya mikopo,hasa kwa kiasi sh. milioni 1.lakini wanaochukua chini
ya hapo marejesho ni mazuri Alisema kama mwanachama akishindwa
kurudisha mkopo wa sh.1000,000 inakuwa vigumu kwa wanachama kumsaidia
mwanachama mwenzao kutokana na mazingira ya hali halisi Mkurugenzi Mtendaji wa Tujijenge Microfinance Bw. Jimmy Makugira, alisema tatizo la ni kubwa . "Lakini baadhi ya taasisi ndogo za fedha zina lawama na lawama,wengine hawana wakaguzi wa ndani na pia wao huajiri maofisa ambao hawana uzoefu na kuaribu kila kitu. Washiriki
alilaumu kuwa ukosefu wa kumbukumbu kwa taasisi za mikopo ni miongoni
mwa sababu zinazochangia mteja moja kupata mkopo mara tatu au zaidi
kutoka taasisi nyingine kwa wakati mmoja na wengine hutumia vitambulisho
tofauti. Kazi ya TAMFI ni kuimarisha sekta ndogo za fedha za Tanzania kwa kukuza ushirikiano na ushirikiano kati ya mashirika ya wanachama wake, kutoa mafunzo, kufanya utafiti, na kushawishi serikali ya Tanzania.
|
Posted: 08 May 2012 12:18 AM PDT
Makamu
wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akiwapongeza Manaibu Waziri
wapya, baada ya kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam jana. (Picha na Michael
Machella)
|
Posted: 08 May 2012 12:16 AM PDT
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MBUNGE
wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya (CCM), Dkt.Mary Mwanjelwa, amesema hajutii
kukosa kuteuliwa katika Baraza jipya la Mawaziri lililoapishwa jana kwa
kuwa halikuwa lengo lake la kuwania ubunge na hana mpango wa kuhamia
CHADEMA, kama inavyoelezwa. Alisema uvumi huo unaenezwa na watu aliodai ni wapinzani wake kisiasa mkoani hapa. Akizungumza
na waandishi wa habari akiwa ameongozana na Katibu wa CCM mkoani Mbeya,
Bi.Cerena Shumbuso, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi, Bw.Bashiru
Madodi na viongozi wengine, Dkt.Mwanjelwa alisisitiza kuwa yeye ni kada
aliyeivishwa na kuandaliwa na CCM kwa miaka mingi, hivyo hawezi
kukurupuka kwenye kutoa maamuzi. Alisema kamwe hawezi kuhama
CCM kwa madai ya kukosa kuteuliwa katika nafasi za uwaziri kwa kuwa
makubaliano yake ya kuwania nafasi ya ubunge ni kuwatumikia wananchi wa
Mbeya na si kuteuliwa kuwa waziri. Alisema anafahamu kuwa CCM ina
wabunge wengi wasomi na wachapa kazi kama yeye, hivyo ni amri ya
mamlaka ya uteuzi kuangalia mbunge yeyote anayeonekana kufaa kuteuliwa
bila kuhojiwa wala mtu kuchukia na kuamua kukimbia chama. "Siwezi
kuhama CCM kamwe eti kwa sababu sijateuliwa kuwa waziri, hapana mimi
nimefurahi sana wenzangu ndani ya chama kuteuliwa na kuonekana wanafaa
tena anayeteua ni rais ambaye ninaamini hakurupuki na uwezo wake ni
mkubwa wa kupembua mambo, hivyo siwezi kukosa akili kwa kuhama chama
kwa madai ya kuchukia kutoteuliwa,"alisema. Alisema anaamini
kuwa bado anakubalika ndani ya chama hicho hususani Jumuiya ya Umoja wa
Wanawake iliyomteua kutokana na imani waliyonayo kwake atagombea tena
kupitia kundi la viti maalumu (CCM) mwaka 2015 kwa kuwa anaamini kuwa
amefanya mambo makubwa ndani ya jumuia hiyo hadi sasa. Dkt.Mwanjelwa
alisema kuwa atagombea nafasi hiyo baada ya kumaliza kipindi cha miaka
mitano ili kuonesha kuwa lengo lake ni kuwatumikia wananchi wa Mbeya.
|
|
Posted: 08 May 2012 12:13 AM PDT
Rais
Jakaya Kikwete (kushoto), akimuapisha Balozi Hamis Kagasheki, kuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha
mawaziri iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam jana.
(Michael Machella)
|
Posted: 08 May 2012 12:11 AM PDT
Na Gladness Mboma
MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, amesema watamshangaa Rais Jakaya
kikwete, kama hatamchukulia hatua za haraka kwa kumfikisha mahakamani
aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bw. Mustapha Mkulo na wenzake, waliotuhumiwa
moja kwa moja na wabunge kwa ubadhirifu.
Bw.Zitto alitoa kauli hiyo jana kwenye viwanja vya Ikulu, ambapo alishiriki tukio la kuapishwa kwa mawaziri na manaibu waziri. "Kuna
wale waliotuhumiwa moja kwa moja kama vile Mkulo, tunataka ndani ya
muda mfupi Rais atawafikisha mahakamani,"alisema Bw. Zitto ambaye juzi
aliwatahadharisha Mawaziri kutofanya sherehe na kuvishwa maua wakati
watakapoapishwa, alisema kuwa wapo mawaziri waliokwenda na maua hayo,
lakini yalikataliwa getini. Katika tukio la jana hakuna waziri
aliyevalishwa taji la maua baada ya kuapishwa na ndugu wa karibu, lakini
hakuna ushahidi kuwa yalizuiliwa mlango wa kuingilia Ikulu kama
alivyodai Bw. Zitto. Alisema kwamba sasa wana kazi ya kusimamia
Serikali ili iendelee kuwawajibisha wale wote wanaotuhumiwa kwa
ubadhirifu wa mali ya umma. Bw. Zitto alisema kuna watu ambao
hawana makosa, ila kosa lao limesababishwa na watendaji wa chini, hivyo
inabidi Rais Jakaya Kikwete ashikilie msimamo wake wa kuwawajibisha wale
watendaji wote waliosababisha hasara kwa umma. Alisema kuwa
wamedhihirisha kwamba bunge lina uwezo wa kung'ata na halina meno ya
plastiki na kwamba uteuzi wa mawaziri hao umetokana na shinikizo lao.
|
Posted: 08 May 2012 12:08 AM PDT
Rais
Jakaya Kikwete (kushoto), akimuapisha Dkt. Hussein Mwinyi, kuwa Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye
Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam jana. (Picha na Nyakasagani Masenza)
|
Posted: 08 May 2012 12:05 AM PDT
Makamu
wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimpongeza Bi. Janeth
Mbene, baada ya kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam jana kuwa Naibu Waziri wa
Fedha na Uchumi. (Picha na Nyakasagani Masenza)
|
Posted: 08 May 2012 12:03 AM PDT
Rais
Jakaya Kikwete (kushoto), akimuapisha Mhandisi Paul Chiza kuwa Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, wakati wa hafla Ikulu Dar es Salaam
jana. (Michael Machella)
|
Posted: 07 May 2012 11:58 PM PDT
Na Mwali Ibrahim
BINGWA
wa mchezo wa Kickboxing nchini, Japhet Kaseba ametamba KO ya Francis
Cheka dhidi ya Mada Maugo, haimtii hofu katika pambano lao
litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Kaseba amejitapa
hivyo licha ya pambano lao la mwaka 2009 dhidi ya Cheka kukung'utwa kwa
KO ambapo pambano la sasa litakuwa katika uzito wa kilogram 75, raundi
12 huku Cheka akiutetea ubingwa wake wa IBF aliounyakua baada ya
kumtwanga Maugo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseba alisema
yeye hatishwi na matokeo hayo zaidi anaendelea na mazoezi ili
kuhakikisha katika pambano hilo hafanyi makosa.
"Yale ni matokeo
yake na Maugo lakini mimi hayanitishi zaidi ya kunipa changamoto ya
kuweza kujiweka sawa na kuweza kumkabili katika mashindano hayo,"
alisema.
Alisema tayari ameishaanza mazoezi kwa ajili ya pambano
katika gym yake iliyopo komakoma, Mwanyamala na ana imani atafanya vyema
kwani ana muda mrefu wa kujiandaa.
Alisema katika kipindi chote
kabla hajapata pambano alikuwa akifanya mazoezi, hivyo ana imani hadi
kufikia siku hiyo atakuwa amepata mazoezi ya kutosha.
|
Posted: 07 May 2012 11:56 PM PDT
Na Amina Athumani
TIMU
ya Taifa ya netiboli (Taifa Queens), leo itafungua pazia la michuano ya
Kombe la Afrika kwa kuumana na Lesotho katika mchezo utakaopigwa saa
nane mchana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kabla ya mchezo huo
utatanguliwa na mchezo kati ya Botswana itakayomenyana na Malawi ambapo
mchezo huo nao utachezwa kwenye uwanja huo huo. Akizungumza
Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Netoboli Tanzania
(CHANETA), Rose MKisi alisema maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo
imekamilika.
Alisema timu zote nane zimeshawasili kwa ajili ya
michuano hiyo itakayofunguliwa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mama Salma Kikwete.
Alisema tayari viongozi mbalimbali
kutoka Shirikisho la Netiboli Duniani (IFNA) pamoja na waamuzi
mbalimbali watakaochezesha michuano hiyo wamewasili.
Alisema
ratiba nyingine ya michuano hiyo itatolewa leo mara baada ya ufunguzi
zitakazopambwa na nyimbo za mataifa mbalimbali yanayoshiriki michuano
hiyo kwa kupigwa kwa blast band. Alisema kwa upande wa Taifa
Queens ipo kwenye ari ya ushindani na kwamba makocha wote kutoka Bara na
Zanzibar wamejipanga kuhakikisha timu hiyo inaaza vema michuano hiyo. Taifa
Queens inaundwa na Pili Peter, Irene Elias, Beth Kazinja, Jacqueline
Skozi, Restuta Boniface, Doritha Mbuta na Lilian Sylidion. Wengine
ni Matalena Muhagama, Paskalia Kibayasa, Siwa Juma, Subira Juma, Subira
Songwe, Penina Mayunga, Evodia Kazinja, Niza Nyange, Mwanaid Hassan,
Lydia Samwel na Joyce Edward.
Michuano hiyo itafikia kilele chake
Mei 12, mwaka huu ambapo hii ni mara ya pili kufanyika kwa michuano
hiyo ambapo mara ya kwanza ilifanyika 2009. Michuano hiyo itaiwezesha Tanzania kupanda viwango vya Dunia vya IFNA ambapo kwa sasa Tanzania ipo nafasi ya 20.
|
Posted: 07 May 2012 11:55 PM PDT
Na Rehema Mohamed
MAWAKILI
upande wa utetezi katika kesi inayomkabili msanii maarufu nchini,
Elizabert Michael 'Lulu', wamewasilisha mahakamani ombi la kutaka
mahakama hiyo imuone mshtakiwa huyo ana miaka chini ya 18 hivyo kesi
hiyo ihamishiwe katika mahakama ya watoto.
Ombi
hilo liliwasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na
mmoja wa mawakili wanaomtetea Lulu, Kened Fungamtama mbele ya Hakimu,
Agustina Mmbando wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Wakati
Fungamtama akiwakilisha ombi hilo, aliiambia mahakama hiyo kuwa
mshtakiwa huyo ana miaka 17, hivyo shauri lake linatakiwa kuhamishiwa
katika mahakama ya watoto. Aliongeza kuwa upande wa mashtaka
haujawasilisha mahakamani hapo pingamizi lolote kuhusu umri wa miaka
hiyo hata pale mshtakiwa mwenyewe alipoieleza mahakama kuwa ana miaka 17
badala ya 18. Katika kuunga mkono ombi hilo Fungamtama
aliwasilisha cheti cha kuzaliwa alichodai kuwa cha mshtakiwa ili
mahakama hiyo iweze kujiridhisha kuhusu umri wa mshtakiwa huyo
kinachoonesha mwaka na mahali alipozaliwa. Hata hivyo wakili wa
serikali katika kesi hiyo, Elizabert Kaganda alipinga ombi hilo na kudai
kuwa ameshtushwa na ombi hilo kwakuwa kesi imekuja kutajwa na kwamba
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza ombi lolote kwakuwa kesi hiyo
haitasikilizwa mahakamani hapo. Kaganda alidai kuwa kesi hiyo
bado ipo katika hatua ya upelelezi ambao bado haujakamilika na kwamba
miongozi mwa vitu wanavyovichunguza ni pamoja na umri wa mshtakiwa huyo. Aliongeza
kuwa katika cheti cha kuzaliwa kilichooneshwa mahakamani hapo na
Fungamtama, alidai kuwa hawawezi kukiamini kwani kina jina la Dayana
Elizabert wakati mshtakiwa anaitwa Elizabert Michael. "Mheshimiwa
hakimu tunaomba tupewe hicho cheti tukichunguze pia tupewe muda
tuchunguze zaidi kuhusu umri wake,kama itabainika ana miaka chini ya 18
mshtakiwa ana haki zote za kushtakiwa katika mahakama ya watoto"alisema
Kaganda. Akitoa uwamuzi wa maombi hayo hakimu Mmbando aliutaka
upande wa utetezi kusubiri kesi hiyo itakapowasilishwa katika Mahakama
Kuu ndipo wawasilishe maombi hayo kwakuwa mahakama hiyo hivi sasa haina
mamlaka. "Mahakama hii inajua kuwa shauri lililo mbele yake ni la
mauaji,hatuna mamlaka ya kutoa uamuzi wowote kwa sasa ,maombi yoyote
yafanyike Mahakama Kuu"alisema Mmbando. Kesi hiyo imeahirishwa
hadi Mei 21, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo
Lulu anashtakiwa kwa kudaiwa kusababisha kifo cha msanii mwenzake wa
filamu, Steven Kanumba.
|
Posted: 07 May 2012 11:53 PM PDT
Mtuhumiwa
wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii maarufu wa filamu nchini, Steven
Kanumba, Bi. Elizabeth Michael 'Lulu', akiwa chini ya ulinzi mkali wa
askari magereza, wakati akitolewa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam jana, mara baada ya kesi kuahirishwa kwa mara ya
tatu. (Picha na Prona Mumwi)
|
Posted: 07 May 2012 11:48 PM PDT
|
Posted: 07 May 2012 11:45 PM PDT
Na Grace Ndossa
NAIBU
Waziri wa Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni, Amos Makalla amesema
changamoto zilizopo kwenye sekta ya michezo atahakikisha anazitafutia
ufumbuzi.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana baada ya
kuipishwa kuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo na Rais Jakaya Kikwete na
kueleza kuwa anatambua changamoto zilizopo katika sekta hiyo "Natambua
changamoto zilizopo katika sekta hiyo, hivyo wadau wa michezo wamepata
mtu anayefaa katika nafasi hiyo na kuahidi kuchapa kazi kwa kushirikina
na wanamichezo,"alisema Makalla. Aliongeza:"Kwa kuwa mimi ni
mwanamichezo nitahakikisha nafasi hiyo naitumia vyema kuimarisha
changamoto zinazoikabili sekta hiyo". Alisema changamoto zilizopo katika sekta hiyo anazitambua na hivyo atazifanyia kazi ili waweze kusonga mbele bila kurudi nyuma. Hata
hivyo, alitamba kuwa anaimudu nafasi aliyochaguliwa kwani kwa
kushirikiana na waziri wataangalia changamoto zilizopo katika sekta hiyo
na kuzifanyia kazi. Alisema kuwa wadau wa michezo wakae mkao wa kula kwani hata yeye ni mwana michezo na ni Kapteni wa time ya Wabunge.
|
Posted: 07 May 2012 11:43 PM PDT
Na Victor Mkumbo
WACHEZAJI
na viongozi wa klabu ya soka ya Azam FC, wamepewa tuzo na uongozi wa
klabu hiyo baada ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na kushika
nafasi ya pili. Wachezaji hao walipewa tuzo za vyeti baada ya kuonekana kujituma vilivyo katika Ligi Kuu na kuonesha ushindani mkubwa. Katika
hafla hiyo, iliyofanyika Dar es Salaam juzi usiku, mshambuliaji John
Bocco alizawadiwa tuzo ya kuwa mfungaji bora wa msimu uliopita baada
kufunga mabao 19 ambapo hakuna mchezaji wa timu yoyote aliyofikia idadi
hiyo. Naye Mwenyekiti wa klabu hiyo, Abubakar Bakhresa, alisema
wachezaji hao hawana budi kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha
likizo. Alisema kwakuwa wametoa mchango mkubwa katika kufanikisha
timu hiyo kushika nafasi ya pili, wasibweteke bali waendelee na nidhamu
waliyokuwa nayo katika kipindi chote cha msimu uliopita. Alisema kutokana na mafanikio hayo wanatarajia mwakani kujipanga vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.
|
Posted: 07 May 2012 11:41 PM PDT
Watoto
Yasini Juma (kushoto) na Haruna Magara wakiwania mpira wakati wa mchezo
wao uliofanyika nyumbani kwao Buguruni Kisiwani Dar es salaam
juzi.Ukosefu wa viwanja vya kuchezea kunasababisha watoto mbalimbali
kucheza sehemu zozote zenye nafasi.Picha na Rajabu Mhamila
|
Posted: 07 May 2012 11:35 PM PDT
Na Zahoro Mlanzi
MECHI
ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, timu za Simba na
Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
260,910,000 huku kila timu ikipata sh. 62,646,395. Mchezo huo
ulikuwa ni moja kati ya michezo ya kufunga pazia la ligi hiyo uliochezwa
juzi ambapo Simba iliweka historia nyingine kwa kuibuka na ushindi
mnono wa mabao 5-0. Kwa
ushindi huo, Simba ambayo ilishatwaa ubingwa huku ikiwa na mechi moja
mkononi, imefanya ubingwa huo kuwa na raha ya aina yake baada ya
kuifunga Yanga. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo
vya habari Dar es Salaam na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura ilieleza kwamba mechi hiyo
ilihudhuriwa na watazamaji 41,733. "Viingilio katika mechi hiyo
vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti
vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh. 30,000 VIP B na sh. 40,000
VIP A ambapo watazamaji 36,980 walinunua tiketi za sh. 5,000 wakati 203
walikata za sh. 40,000," alisema Wambura. Alisema kutokana na
mapato hayo kila timu ilipata sh. 62,646,395, asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 39,799,830 wakati TFF ilipata sh.
19,908,361. Alisema gharama za mechi kabla ya mgawo ni nauli ya
ndani ya waamuzi na kamishna sh. 20,000, posho ya kujikimu kwa kamishna
sh. 40,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh.
8,539,950. Pia alisema maandalizi ya uwanja ni sh. 400,000, umeme
sh. 300,000, ulinzi na usafi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina ni sh.
2,000,000.
|
Posted: 07 May 2012 11:33 PM PDT
Na Elizabeth Mayemba
KUFUATIA
kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Simba, mmoja wa aliyekuwa Mjumbe wa
Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga Habert Marwa,baada ya kuonyesha
kusikitishwa sana na kipigo hicho, alisema ili timu hiyo iwe na
mafanikio makubwa haina budi iongozwe na vijana.
Akizungumza
Dar es Salaam jana na mwandishi wa habari hizi baada ya kuhojiwa Marwa
alisema, ili timu iwe na hadhi yake ni lazima iongozwe na isimamiwe na
vijana ambao ndiyo nguvu kazi.
"Kama jina lenyewe la timu Young
Africans, hivyo nguzo ya ushindi ni vijana kama ilivyo pia kwa
wachezaji, kama uongozi utasajili wachezaji wazee lazima timu ifanye
vibaya, lakini wakisajili wachezaji wenye umri mdogo watafanya vizuri
katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa kuwa watakuwa
ni damu changa," alisema Marwa.
Alisema timu inapofungwa
wanaoumia na kusononeka wengi wao ni vijana ambao pia hujitolea kwa hali
na mali kuichangia timu kimapato kwa kulipia viingilio na kuishangilia
timu yao inapocheza.
Kwa hali hiyo Marwa alishauri vijana wenye moyo na jitihada za namna hiyo ndiyo wanaostahili kupewa jukumu la kuiongoza Yanga.
Marwa
alisema Mwenyekiti wa klabu hiyo, Llloyd Nchunga alifanya kosa kubwa
sana kuwakabidhi wazee timu bila kushauriana na vijana baada ya uongozi
wake kushindwa.
"Tunaamini kabisa wazee wanamawazo mazuri sana ya
kuushauri uongozi unapokuwa na dhamira sahihi ya ushindani, kwani
uzoefu walioupata enzi hizo wakiwa viongozi tena vijana ungewasaidia
viongozi kwa wakati huu kufanya vizuri," alisema.
Alisema
aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Davis Mosha ambaye
alijiuzulu wadhifa huo, alijitahidi kwa kiasi kikubwa kuwashawishi na
kuwashirikisha yeye na vijana wengine kuchangia kwa fikra na uwezo wa
kiuchumi pamoja na nguvu kazi ili timu hiyo iweze kupata mafanikio na
hadhi yake pindi tu baada ya yeye kuchaguliwa. "Baada ya Mosha kujiuzulu wengi wao na mimi nikiwemo tulijiuzulu siku moja baada ya yeye kujiuzulu," alisema Pia
aliwaasa vijana kujitokeza kwa wingi kwenda kuchukua kadi za uanachama
wa klabu hiyo, badala ya kuwa mashabiki tu ili wapate fursa ya kuchagua
viongozi bora na imara. Hata hivyo alipoulizwa uwepo wake ndani
ya klabu hiyo alisema "Baada ya kujiuzulu niliendelea kuwa mwanachama na
shabiki kama ilivyokuwa awali, ikiwa na kutoa mawazo kama nilivyotoa
mchango wangu huu wa mawazo kwa sasa,"alisema.
|
No comments:
Post a Comment