Na Darlin Said
KWA
nyakati tofauti Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekuwa ikitoa
taarifa juu ya mlundikano wa wafungwa na hali mbaya ya magereza nchini.
Mfungwa
ni mtu aliyeadhibiwa kwenda Gerezani baada ya kutenda makosa au uhalifu
katika jamii ili kujifunza na kutorudia kosa hilo.
Adhabu
hutolewa kisheria na mahakama ambapo hutumikia adhabu hiyo huku
akisimamiwa na kurekebishwa tabia zao.Mfungwa hupokea mafunzo mbalimbali
na kupelekea kupata ujuzi katika ufundi, ukulima, ufugaji na fani
nyingine nyingi.Ni
tegemeo la serikali na jamii kuwa, mfungwa anamaliza kutumikia kifungo
chake awe amebadilika kitabia na kuwa raia mwema anayeweza kushiriki
katika kuleta maendeleo ya jamii inayomzunguka.Kwa kulitambua
hilo Chama cha kurekebisha mwenendo wa watu waliomaliza kifungo Tanzania
(E.R.S.T) kilianzishwa mwaka 2009 chini ya mwenyekiti Bw.Shafii Kondo
ili kuwapatia mafunzo.
Pia, ni kuwaunganisha wafungwa waliomaliza vifungo vyao na kuwarekebisha
tabia zao ili wasiweze kufanya tena uhalifu ambao utawasabishia kurudi tena gerezani.Lengo
lengine ni kutoa elimu katika jamii ili waweze kuwapokea na
kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kutumia
ujuzi walioupata gerezani.Vilevile kuhakikisha wanasimamia vema
haki za wafungwa zilizosaulika mfano haki ya kupiga kura na ya kukutana
na wanandoa wenzao.
Pia kuhakikisha kwamba wanatoa msaada wa
kifedha, vifaa na rasilimali ardhi ili iwe changamoto kwa waliomaliza
vifungo kujiunga na Taasisi za aina hii ili waweze kujiepusha
kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.Ili waweze kufanikisha
malengo yao chama kimeanzisha miradi mbalimbali ikiwemo shughuli za
kuchana mbao, karakana, ukulima na ufugaji.
Kwa uhalisia tunaona
kwamba, katika magereza nchini kuna matatizo ya kisheria yanayopelekea
wafungwa kukosa uhuru wao ambayo ni kinyume na haki za binaadamu.Kwa
mfano katika sheria zetu wafungwa hawana haki ya kupiga kura kumchagua
kiongozi anayemtaka na pia hawana haki ya kukutana na wanandoa wao
ambapo ni kinyume na haki za kibinaadamu.Serikai inatakiwa
kubadili mfumo wa sheria ya magereza kutoka mfumo wa kikoloni ambazo
zinaonekana kandamizi kwa wafungwa na kuwanyima haki zao za msingi.
Sheria
ziliopo ni za kikoloni wakati wafungwa ni wa kisasa, pia washirikishwe
kutoa mawazo yao katika mchakato wa kubadilisha katiba kwani ni haki
yao ya msingi. Katika magereza bado sheria hazijaboreshwa
ukilinganisha na sehemu nyingine hali inayopelekea kuwa na matatizo
mbalimbali ikiwemo msongamano wa wafungwa.Magereza mengi
yamefurika wafungwa na mahabusu kupita kiasi, huduma za chakula,
matibabu na haki nyingine za wafungwa zimekuwa ama haziheshimiwi kabisa
au pale zinapoheshimwa ni kwa kiwango cha chini kabisa.
Nionavyo
gerezani kuna matatizo mengi ambayo wafungwa wanakumbana nayo ambao
aidha yanasabashwa na sheria zilizopo ambayo wafungwa ndio
wanayoyafahamu vema kuliko mtu yeyote.
Mfano wafungwa kutoruhusiwa
kuwa karibu na waume/wake zao ni tatizo kubwa ambalo linaweza ikapelekea
tatito la ushoga gerezani.Lakini
kama kungekuwa na sheria inayoruhusu wafungwa kukutana na wake zao
ingesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hilo na maambukizi ya VVU.
Aidha upande wa serikali itilie mkazo kwa kufanya magereza yawe
ni vyuo vya mafunzo ya kuwafanya wafungwa wapate ujuzi mbalimbali na
siyo sehemu ya kupata adhabu na unyanyaji .Tunafahamu na
kutambua kuwa magereza siyo hoteli ya kitalii kwa maana hiyo iwe na
huduma za kiwango cha juu sana, lakini pia siyo sehemu ya kuwatesa
wafungwa na kukataa walau kutambua haki zao za msingi.
Tujifunze
kutoka kwa ngugu zetu wa visiwani badala ya kuita magereza wanaita vyuo
vya mafunzo hii inasaidia jamii kuwaona wafungwa ni wenzetu ambao wapo
mafunzoni.Kwa upande wa magereza ya watoto, serikali
ihakikishe kuwa inawapatia watoto hao elimu bora na wasiwape adhabu
kubwa zisizo endana na umri wao. wa kufanya hivyo tunaweza kujenga taifa
linalowajali wafungwa ingawaje wametenda makosa au uhalifu katika
jamii.
Serikali
imetakiwa kuwashirikisha wafungwa katika mchakato mzima wa kupiga kura,
ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kupata haki ya kukutana na wenzi wao
hasa wanapokuwa kifungoni.
No comments:
Post a Comment