Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki pamoja na wadau wa Wasaidizi wa sheria
Naibu Waziri wa katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki kushoto akisalimiana na Bi. Flora Masoy
Na Mohammed Mhina na Martha Komba
SERIKALI imeanza mchakato wa uazishwaji wa mfumo wa Wasaidizi wa Sheria
(Paralegals) ili waweze kutambulika kwa lengo la kuwawezesha kutoa
huduma za kisheria kwa wananchi hasa wa maeneo ya vijijini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki, wakati alipokutana na Wanaharakati wa Kisheria wa Asasi zisizo za Kiserikali ofisini kwake jijini Dar-Es-Salaam.
Mhe. Kairuki amesema kuwa mchakato huo utakapokamilika utawezesha Wasaidizi
wa Sheria kutambuliwa na sheria husika na hivyo kupanua wigo kwa
wananchi wa mijini na vijijini kuwa na msaada wa kisheria wanapopatwa na
matatizo.
“Natambua
umuhimu wa uundwaji wa Sheria hii ya Paralegals ndio maana tumeanza
mchakato huu kwa kuufanyia marekebisho na kueleza dhana nzima ya
Palalegals,” Alisema.
Amewataka Wanaharakati hao kuendelea kuwasisitiza Wasaidizi wa sheria kuhakikisha kuwa wanatoa Huduma zao kwa uwazi zaidi ili wananchi waweze kufaidika hiyo.
Amesema Serikali itahakikisha kuwa inaweka mazingira bora yatakayowawezesha Wasaidizi wa Sheria kufanya kazi zao vizuri lakini kwa kuzingatia misingi ya Sheria na Haki za Binadamu.
Wanaharakati
hao wamesema kuwa mpaka sasa Wasaidizi wa Sheria (Paralegals) bado
hawajatambulika kisheria na kwamba sheria haitoi nafasi kwa Mawakili wa
Serikali au wa kujitegemea kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo na
Mabaraza ya Kikata maeneo ambayo ndiyo yenye matatizo makubwa ya
kisheria kwa wananchi wa kawaida.
Akizungumza
kwenye mkutano huo Wakili wa Kujitegemea Bw. Alphonse Katemi amesema
wananchi wengi wanakosa haki kwa sababu mfumo wa kisheria hauruhusu kwa
Mawakili kutoa huduma za kisheria katika Mahakama za mwanzo na Mabaraza
ya Kata.
“Kwa
hiyo ni suala ambalo kwa kweli wananchi wengi wanakosa haki kwa sababu
ni mfumo wa kisheria mawakili kwenye mabaraza haya ya ardhi hawaruhusiwi,”
Alisema Katemi na kuongeza kuwa huko ndiko kwenye maeneo ambayo
yanawatesa sana na kuwaumiza wananchi wa nchi hii.
No comments:
Post a Comment