CHAMA cha Waandishi
wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Jumapili Mei 20, 2012 saa nne asubuhi
kitatangaza mdhamini wa Tuzo za Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011.
Mdhamini huyo
atatangazwa kwenye mkutano ambao ataufanya Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto
pamoja na mdhamini wa tuzo hizo, ambapo mkutano huo utafanyika kwenye mgahawa mpya
uitwao City Sports & Lounge uliopo jirani na mnara wa askari
makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe, Posta Dar es Salaam.
TASWA inachukua fursa
hii kuwaalika waandishi wote wa habari za michezo kuhudhuria kwenye mkutano huo
ili tuweze kuanza pamoja katika mbio hizi za kuelekea kwenye Tuzo ya Mwanamichezo
Bora wa Mwaka 2011.
Tayari Kamati ya Tuzo
ishateuliwa na imetangazwa, hivyo baada ya mkutano huo taratibu nyingine
zitatangazwa kwa kadri zitakavyokuwa zimekamilishwa na Kamati Maalum ya Tuzo ya
Mwanamichezo Bora wa Tanzania.
Kwa miaka mitano
iliyopita walioshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa TASWA walikuwa ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle
(2007), Mary Naali (2008), ambao
wote ni wanariadha, wakati 2009 na 2010 alikuwa mcheza netiboli Mwanaidi
Hassan.
No comments:
Post a Comment