Kocha mkuu wa timu ya Simba Milovan Cirkovic
akiwa amebeba picha na msalaba wa mchezaji wake Marehemu Patrick
Mafisango aliyeafariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia Alhamiswi
katika maeneo ya Chang'ombe Veta, wakati mwili wake ulipopelekwa kwenye
uwanja wa ndege wa Mawlimi J.K.Nyerere kwa ajili ya kuusafirisha kesho
kwenda nyumbani kwao nchini Rwanda kwa mazishi.
Marehemu Patrick Mutesa Mafisango aliagwa leo
kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe na umati mkuwabwa wa mashabiki
wa mpira wa miguu pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba Boniface Pawasa akilia kwa uchungu
wakati alipokewanda kuuaga mwili wa aliyekuwa rafiki yake marehemu
Patrick Mafisango aliyeagwa leo.
Mwili wa marehemu ukiandaliwa tayari kwa kupelekwa uwanja wa ndege ili
kuusafirisha kwenda nchini Rwanda mara baada ya kuagwa rasmi leo.
Makamu Mwenyekiti wa Simba akionekana mwenye majonzi huku akiwa amebeba
shada la maua wakati wmili wa marehemu Patrick Mafisango ukiondolewa
kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe leo.
Viongozi pamoja na mashabiki wa timu ya Simba wakiubeba mwili wa marehemu kuupelekwa kwenye gari.
Mwili wa marehemu Patrick Mafisango ukiingizwa kwenye gari
Msafara ukielekea uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K. Nyerere.
Mwenyekiti wa timu ya Simba Ismail Aden Rage akielekeza msafara mara baada ya kufika uwanja wa ndege.
Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari maalum kwa ajili ya kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti uwanja wa ndege.
Gaqri maalum likiupeleka kwenye chumba cha kuhifadhi.
Mdogo wake marehemu Patrick Mafisango kushoto ambaye hakutaka jina
lake kutajwa akiwa ameshika shada la maua pamoja na mmoja wa
waombolezaji.
Maiti ya Marehemu
Patrick Mafisango aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba ukiingizwa kwenye
chumba maalum cha kuhifadhia maiti tayari kwa kuusafirishwa kesho
kuelekea nchini Rwanda kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment