MCHEZAJI wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) na
timu ya Simba Patrick Mutesa Mafisango (32), amefariki dunia jana
alfajiri kwa ajari ya gari.
Amepata ajali hiyo akitokea kwenye Ukumbi wa Starehe wa Club Maisha
uliyopo Masaki. Akizungumza Dar es Salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa
klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu, alisema Mafisango alikubwa na
mauti hayo eneo la Keko jirani na Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam.
Alisema Mafisango amekufa kwa ajali ya gari, baada ya gari alilokuwa
anaendesha kuacha njia na kugonga mti ulio pembezoni mwa barabara ya
Chang’ombe majira ya saa kumi kasorobo alfajiri na kufariki papo hapo.
Kaburu ameongeza gari hilo ndani lilikuwa na abiria wengine wanne,
lakini aliyekutwa na mauti baada ya ajali ni Mafisango pekee. Alisema
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
tayari kwa kusafirishwa kwenda kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) ambako atazikwa.
Kaburu alisema ingawa alikuwa na uraia wa Rwanda na akiichezea timu
ya taifa ya nchi hiyo (Amavubi), Mafisango alikuwa ni mzaliwa na raia wa
DRC na uamuzi wa kuzikiwa huko ni wa familia yake. Msiba wa Mafisango
uko katika eneo la Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka
Mawili eneo la njia Panda ya Sigara.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa kesho Ijumaa saa nne asubuhi
katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam kabla ya
mwili wake
kusafirishwa kwenda Kinshasa majira ya saa kumi jioni.
kusafirishwa kwenda Kinshasa majira ya saa kumi jioni.
Mafisango alizaliwa Machi 30, 1980 huko Kinshasa Zaire wakati huo na
ameacha mke na mtoto mmoja wa kiume, Chris Paul, mwenye umri wa miaka
mitano.
Mafisango ameichezea Simba kwa msimu mmoja tu akitokea Azam ya Dar es Salaam lakini kabla ya hapo alichezea pia TP Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda na pia aliwahi kuwa nahodha wa Amavubi kwa takribani miaka mitano.
Mafisango ameichezea Simba kwa msimu mmoja tu akitokea Azam ya Dar es Salaam lakini kabla ya hapo alichezea pia TP Mazembe ya DRC, APR ya Rwanda na pia aliwahi kuwa nahodha wa Amavubi kwa takribani miaka mitano.
Mara baada ya taarifa hiyo wanachama wa klabu ya Simba na wachezaji
walipatwa na mshtuko mkubwa ikiwa ni pamoja na kuamua kwenda Muhimbili
kuhakikisha kama ni kweli mwenzao huyo amewatoka.
kuhakikisha kama ni kweli mwenzao huyo amewatoka.
Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa karibu na Marehemu kama
marafiki ni Haruna Moshi Boban ambaye yupo kwenye kambi ya timu ya
Taifa, Taifa Stars alishindwa hata kufanya mazoezi na kuomba apewe
nafasi ya kwenda kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzake katika chumba cha
maiti.
Boban ambaye watu wamemzoea kumuona akiwa kimya alionekana mwenye
uzuni nyingi kwa kulia moja kwa moja huku akiomba apewe nafasi ya
kushuhudia mwili wa mpendwa wake huyo. Wengine ni haruna Niyonzima,
ambaye anaichezea Yanga, Uhuru Suleman ambao walionekana wakishindwa
kuvumilia.
Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea
kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda
(Amavubi), Patrick Mafisango kilichotokea jana alfajiri (Mei 17 mwaka
huu) kwa ajali ya gari Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana na ofisa habari wa TFF Boniface Wambura,
alisema kuwa msiba huo ni mkubwa kwa familia ya mpira wa miguu kwani
Mafisango kwa kipindi chote alichocheza mpira hapa nchini akiwa na timu
za Azam na baadaye Simba, aliifanya kazi yake (kucheza mpira) kwa bidii.
Kifo chake ni pigo kubwa si tu kwa familia yake na timu alizochezea,
bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati ambapo changamoto zake
zilikuwa dhahiri uwanjani. Wakati mauti inamkuta, Mafisango alikuwa
ameitwa Amavubi kwa ajili ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya
Afrika zinazochezwa mapema mwezi ujao.
TFF inatoa pole kwa familia ya Mafisango, klabu ya Simba, Shirikisho
la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na kuwataka kuwa na subira na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke
roho ya marehemu Mafisango mahali pema peponi.
Habari hii ni kwahisani ya Gazeti la Jambo Leo.
No comments:
Post a Comment