ZAIDI
ya B65 Tsh. Zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa Maegesho na utanuzi wa
njia za kurukia na kutua ndege katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
Zanzibar unaojuilikana ‘Abeid Amani Karume International Airport.’
Hayo yameelezwa katika hafla ya utiaji saini kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya SOGEA kutoka Ufaransa katika Ofisi za Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Malindi mjini Zanzibar.
Katika
hafla hiyo katibu Mkuu wa Wizara hiyo Vuai Haji Lila alitia saini kwa
niaba ya SMZ na Laurent Brouet ambaye ni msaidizi wa Meneja wa kampuni
hiyo kwa kanda Afrika ya Mashariki ndiye aliyeweka saini kwa niaba ya
kapuni yake.
Akifafanua juu ya utiaji saini huo Naibu
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Issa Haji Ussi alisema
pesa hizo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa Maendeleo wa
Benki hiyo (IDA) ambazo ziliombwa kwa ajili ya ujenzi huo.
Naibu
Waziri huyo alifahamisha kwamba kutekeleza ujenzi huo ni kutimiza
mikakati ya Serikali ya Zanzibar katika kukuza uchumi na kuongeza
uingiaji wa Watalii humu nchini.
Alisema kwamba kukamilika kwa ujenzi huo kutapelekea Ndege nyingi kuingia Zanzibar na wageni kupata nafasi ya kutembelea Nchini jambo ambalo litachochea maendeleo.
“Viwanja
vya Ndege ndivyo vinavyotumika sana kwa kuingiza watalii na uwanja wetu
ukikamilika tunatarajia kupokea watalii wengi”alisema Ussi ambaye ni
Naibu Waziri.
Ussi alisema mbali na kuongezeka Shughuli za Utalii bali na Wananchi wataweza kupata ajira nyingi tokea mwanzo wa ujenzi hadi kukamilika na pale utakapoanza kutoa huduma.
Naibu
Ussi alifahamisha ujenzi huo unategemewa kukamilika katika muda wa
Miezi 18 na wakandarasi hao watalazimika kukabizi kazi hiyo kwa Serikali
ya Mapinduzi kwa matumizi.
Nae
Msaidizi Meneja wa Kampuni hiyo kwa kanda ya Afrika Mashariki Laurent
Brouet alisema atahakikisha Kampuni yake Inakamilisha ujenzi huo kwa
wakati huo ambao umepangwa ili kuondoa Misuguano isiyo yalazima.
“Tutahakiksha ujenzi huu umekamilika kama Mkataba unavyojieleza” alisemanBrouet.
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika mikakati ya kuufanya Uwanja wa
Ndege Huo kuwa wa kisasa ili uweze kuruhusu kutua ndege nyingi kwa
wakati mmoja.
No comments:
Post a Comment