Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Air Tanzania ATC Paul Chizii
akikata keki kama ishara ya uzinduzi wa safari rasmi za ndege hiyo aina
ya Boeing 737-500 hapa nchini kutoka Dar es salaam - Arusha-Mwanza- Dar
es salaam kila siku kwa shilingi 199,000 ikiwani bei ya promosheni
iliyotolewa na kampuni hiyo kwa wateja wake.
Hafla hiyo imefanyika katika viwanja viwili tofauti katika uwanja wa
ndege wa KIA ambapo wafanyakazi na watu mbalimbali waliilaki ndege hiyo
kwa furahi huku kukiwa na vinywaji na vitafunwa na kufuatiwa na sherehe
rasmi iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kabla ya kurejea
jijini Dar es salaam.
Katika picha kulia ni wafanyakazi ndege hiyo Erica kushoto na Doris
wakipiga makofi wakati mkurugenzi huyo alipokuwa akikata keki kwa ajili
ya uzinduzi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Air Tanzania ATC Paul Chizii
akikata utepe wakati akizindua safari za ndege ya Shirika hilo kwenye
uwanja wa ndege wa Mwanza.
Kutoka kulia ni wadau wa kampuni ya ndege ya ATC Rinah, Neema na Marina wakiwa katika sherehe hiyo jijini Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Air Tanzania ATC Paul Chizii
akifurahia jambo na mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo Dada
Mawanamvua.
Mkurugenzi wa Fllshangweblog Bw. John Buku,ku akipozi kwa picha na
mwandishi wa habari Said wakati ndege hiyo ikielekea jijini Mwanza
kutoka KIA.
Mfanyakazi wa ndege hiyo Erica Mchata akiwajibika kazini.
Baadhi ya abiria waliosafiri na ndege |
Abiria wakishuka kwenye ndege baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Abiria wakishuka kwenye ndege baada ya kuwasili jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment