Washiriki Kutoka Tanzania kulia Bi Fauzia Haji kutoka Idara ya Mazingira
Zanzibar,Katikati Bi Imelda Adam Afisa Mazingira mwandamizi Ofisi ya
Makamu wa Rais, na Bw. Ladslaus Kyaruzi Afisa Mazingira Mwandamizi
kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais wakijiandaa kuwasilisha mada kwa niaba ya
nchi za Africa katika mkutano wa Sayansi na Taaluma ya Mabadiliko ya
Tabia Nchi unaendelea Mjini Bonn Ujerumani kuhusu Madhara yatokanayo na
mabadiliko ya tabia nchi.
Bi Emelda Taikwa Adam, Afisa Mazingira mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu
wa Rais Akiwasilisha maoni ya Tanzania katika masuala ya Kilimo na
mabadiliko ya Tabia nchi, katika mkutano wa sayansi ya Taaluma ya
mabadiliko ya tabia nchi unaendelea mjini Bonn Ujerumani (Picha na
Evelyn Mkokoi)
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
BONN UJERUMANI
Tanzania kama nchi nyingine zinazoendelea imepata fursa ya kuwasilisha maoni yake
kuhusu kilimo katika kuhimli mabadiliko ya Tabia nchi katika mkutano
kimataifa wa 36 wa sayansi na taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi,
unaendelea mjini Bonn Ujeremani.
Akiwasilisha maoni hayo, katika Mkutano huo Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Bi Emelda Taikwa Adam ameeleza kuwa, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania
zinatakiwa kuangalia zaidi katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ili
kuweza kuongeza uzalishaji na kuhakikisha usalama wa chakula kupitia
sekta ya kilimo kwani ndo uti wa mgongo wa Taifa.
Bi Emelda aliongeza kuwa, katika kuhimili mabadiliko ya Tabia nchi Tanzania kupitia sekta ya kilimo na tafiti zilizokwisha fanyika kuonyesha kuwa kuna matumizi salama ya mbegu zinazohimili ukame, pamoja na matumizi sahihi ya kilimo cha umwagiliaji, na kuna kila sababu ya matumizi ya teknolojia zaidi ya kisasa na kujenga uwezo kwa wakulima wa kawaida ili kuweza kuhakikisha usalama wa chakula.
“Tafiti
zinaonyesha kuwa kilimo huchangia 13% katika kuzalisha gesi joto hivyo
basi kuna umuhimu mkubwa wa kuingiza masuala ya kilimo katika kuhimili
mabadiliko ya tabia nchi, kwa sababu nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hutegemea kilimo alisisitiza.”
Akizungumzia
athari za mabadiliko ya Tabia nchi katika sekta ya kilimo bi Emelda
amesema kuwa, kupungua kwa mvua kunakopelekea ukame nchini na kuongezeka
kwa gesi joto kumeathiri kwa kiasi kikubwa sana sekta ya kilimo, na
katika kupunguza gas joto katika kilimo kunahatarisha usalama wa chakula
na kupoteza ardhi kwa wenyeji.
Aliongeza kuwa pamoja na kwamba sekta ya kilimo imekuwa na mikakati
mbalimbali inayotekelezeka katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi,
Tanzani inatakiwa kuwa na mfumo ambao utahakikisha kuwa upunguzaji wa
gesi joto katika kilimo unatokana na jitihada za kuhimili mbadiliko ya
tabia nchi.
No comments:
Post a Comment