Posted: 17 May 2012 12:21 AM PDT
Na Salim Nyomolelo
ALIYEKUWA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito
zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi
vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.
Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.
Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.
"Kwa
kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba
maliasili ni ngumu... ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga
ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema Bw. Maige na kuongeza;
"Ndivyo ilivyotokea."
Alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia
ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia
sheria na kuwapa vitalu Watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha
wazungu kama sheria ilivyoelekeza.
"Ni Waziri gani
aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu
wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha
matendo na maamuzi ya kishujaa ya Maige ya 2011," alisema Bw. Maige na
kuongeza;"Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata.
Tena si siku nyingi.
Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu...bado
nasisisitiza hivyo."Alihoji kuwa; "NI waziri gani aliyefunga biashara
ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa
watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua
hatua."
Alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza
mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini,
mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.
Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.
Alisisitiza
kuwa maamuzi hayo magumu yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi
mkubwa. "Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema Bw.
Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka Bungeni na
kuongeza;"Watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda
haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."
Kuhusu sakata la
nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "Kila mbunge
aliyetaka alikopeshwa sh. milioni 290, wengine wameanzisha biashara na
wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.
Alisema
mwenye mashaka aende kwa Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi, au kwa
kamishna wa maadili, au CRDB tawi la Azikiwe na Dodoma alikokopa au
amtafute muuzaji.
Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei.
"Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei
tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo,"
alisema Bw. Maige.
Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani
ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza
wizara hiyo Novemba 2010.
Kuhusu biashara ya wanyamahai, Bw.
Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati
wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika,
walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.
Aliahidi
kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na
ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua
vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara
hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa
Mwangunga.
|
Posted: 17 May 2012 12:15 AM PDT
NA MICHAEL SARUNGI
UBALOZI
wa Marekani nchini umetaja mikakati mbalimbali ambayo Tanzania
inatakiwa kutumia kukabiliana na tatizo sugu la umeme na kuahidi
kusaidia eneo hilo.
Mikakati hiyo ilitajwa Dar es Salaam jana
katika mkutano uliowakutanisha mawaziri wa Waziri wa Nishati na Madini
na ujumbe wa ubalozi wa Marekani ulioongozwa na balozi wa nchi hiyo
nchini, Bw.Alfonso Lenhardt.
Bw.
Lenhardt katika mkutano huo alisema nchi yake ipo tayari kutoa
ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha tatizo hilo linakuwa ni jambo la
kihistoria.
Alisema Tanzania inahitaji mbinu na mipango kazi ya
kufikia malengo ya melenia ya mwaka 2025 inayolenga kuwapatia Watanzania
wengi nishati hiyo ya umeme.
"Ndugu wana habari Marekani ipo
tayari kuwekeza katika nishati hii na tayari tumewakilisha kwa waziri
wenu mipango na mbinu iliyoandaliwa na wataalamu kutoka nchini Marekani
kwa lemgo la kusaidia kuliondoa tatizo hili kama si kulimaliza kabisa"
alisema Bw. Lenhardt
Alisisitiza kuwa Tanzania ina vyanzo vingi vya umeme ambavyo vikitumika uzalishaji wa nishati hiyo utaongezeka.
Akizungumza
katika mkutano huo Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo,
alisema huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuwekeza katika vyanzo vyake
vya umeme ili kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema mojawapo ya
tatizo kubwa inalolikabili Shirika la TANESCO ni uchakavu wa miundombinu
hii inayochangia upotevu wa nishati hiyo.
|
Posted: 17 May 2012 12:14 AM PDT
Msemaji
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali, Kapambala
Mgawe, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam juzi, kuhusu
hatua za uchunguzi zitakazochukuliwa na jeshi hilo ikiwa ni pamoja na
kufukuzwa na kufikishwa mahakamani kwa askari atakayebainika kujiunga na
jeshi kwa kutumia vyeti vya kugushi bila kujali cheo alichonacho hivi
sasa, hatua hiyo inafuatia taarifa ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA),kubaini udanganyifu kugushi vyeti kwa baadhi ya wanajeshi na
polisi. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 17 May 2012 12:08 AM PDT
JUZI
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
ilitangaza imetangaza kwamba nyumba zote zilizojengwa kandokando ya
fukwe za bahari na mito zitabomolewa bila wamiliki kulipwa fidia
kutokana na kukiuka Sheria za Ardhi na Mazingira za mwaka 1992, 1995 na
2004.
Taarifa hiyo ilitolewa
kwa pamoja na mawaziri i katika Wizara hiyo, Prof. Anna Tibaijuka na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa,
walipozungumza na waandishi wa habari kuelezea migogoro ya ardhi
inayotokea nchini na mikakati ya wizara zao kutatua migogoro hiyo.
Prof.
Tibaijuka, alisema zoezi la kuwahamisha wakazi waliojenga kandokando ya
fukwe za bahari litahusisha mikoa yote iliyopakana na Bahari ya Hindi
ambayo ni Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kwa kuzingatia
sheria zilizowekwa ambazo zinakataza ujenzi wa nyumba kandokando ya
fukwe za bahari ndani ya mita 60 pamoja na mita 30 kandokando ya mto.
Kwa
upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk.
Terezya Huvisa, alisema kuwa zoezi la kuwahamisha wakazi waliovamia mito
linatarajiwa kuanza hivi karibuni na wataanza na wakazi waliovamia mto
Mbezi na Nduwe.
Alisema Setelaiti ya mwaka 2005 inaonyesha mto
Ndumbwi ulikuwa unaonekana wazi, lakini sasa wakazi wameuvamia na
kujenga kandokando ya mto huo, hata Mto Mbezi Beach pia
Alisema
kuwa ukaguzi kwa wakazi waliojenga ndani ya mita 30 kutoka kandokando ya
mito utafanyika hivi karibuni sambamba na zoezi la kuwabomolea nyumba
zao.
Tunaunga mkono tamko hilo la mawaziri hao kwani ni lazima
tufuate sheria zinazokataza kujenga kandokando ya fukwe za bahari, kwani
hizo ni sehemu maalum kwa watu wote kuzitumia
Hii ni kutokana na
kwamba kwa kujenga kandokando ya fukwe za bahari na mito ni hatari kwa
maisha kutokana na kuwa tumeshuhudia athari zilizotokea pindi tsunami
ilipoikumba nchi yetu, pamoja na mafuriko
Hatua hiyo ya wizara ni
njema kutokana na kwamba ina lengo la kuzuia majanga yanayoweza
kulikabili taifa endapo yatatokea majanga kama ya tsunami na kupasuka
kingo za mito pindi yanapotokea mafuriko.
Hata hivyo pamoja
na nia njema ya wizara tunachukua fursa hii kuiomba oparesheni hiyo
iende sambamba na udhibiti wa utoaji hati za kumiliki viwanja kiolela
kwani ndicho chanzo cha kuibuka ujenzi huo.
Tumeshuhudia majengo
mengi yakiota kama uyoga katika maeneo mbalimbali ya nchi hususani
fukweni mwa bahari na mito,huku wahusika wakiyafumbia macho .
Tuna imani kama wizara itadhibiti uchakachuaji wa hati za viwanja kwa kiasi kikubwa itasaidia kukomesha tatizo hilo.
|
Posted: 17 May 2012 12:04 AM PDT
Waziri
wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu,
akionesha ripoti ya Uwekezaji Afrika ya Mwaka 2011, na taarifa ya
ufuatiliaji wa hali ya uwekezaji, baada ya kuizindua Dar es Salaam jana,
kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC), Bw. Raymond Mbilinyi na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya
Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO), Bw. Emmanuel Kalenzi, ripoti hiyo
imetayarishwa kwa ushirikiano wa TIC na UNIDO. (Na Mpigapicha Wetu)
|
Posted: 17 May 2012 12:00 AM PDT
Na Darlin Said
TUME
ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba mpya hivi
karibuni imeanza kazi tangu ilipoapishwa na Raisi Jakaya Kikwete.
Wakati
wanaapishwa raisi Jakaya Kikwete moja ya ahadi iliyoitoa kuwa bega kwa
bega ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na tija na kupatikana kwa
maoni ya wananchi ambayo ndio chachu ya katiba itakayojenga Tanzania
mpya.
Tume hiyo yenye
wajumbe 30 kutoka Tanzania bara na Visiwani tayari imeshakabidhiwa jengo
maalum na magari 30 zikiwemo nyumba kwa wale waishio nje ya Dar es
salaam.
Kazi kubwa ya Tume hii ni kusimamia mchakato mzima wa
mabadiliko ya Katiba ili watanzania waweze kupata katiba mpya ambayo
itakidhi na kukata kiu yao.
Majukumu mengine ya tume hiyo ni pamoja na kukusanya maoni, kuyachambua na kuandika rasimu ya katiba ambayo itazaa katiba mpya.
Pia
kuhakisha elimu inatolewa ya kutosha kwa wananchi kuhusu katiba ili
wawe na ufahamu na uhuru wa kutoa maoni bila ya kukwazwa kuzuiwa au
kutishiwa.
Wakati huohuo Tume imepewa jukumu zito la kuakikisha
kwamba wanafanya kazi kwa hali na mali ili kuwatendea haki watanzania na
baadaye kufikia hatima ya kile kanachohitajika kwa maslahi ya nchi.
Wakati
wanakabidhiwa ofisi aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Bi.Celina
Kombani alisema tume imepewa kazi nzito isiyohitaji ubaguzi wa aina
yeyote ambao inahitaji uaminifu, nguvu, maarifa na uvumilivu.
Hivyo basi italazimika kufanya kazi katika mazingira magumu usiku na mchana kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla
Katika
makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba alivitaka
vikundi na wananchi waliopendekeza majina ya wajumbe wa tume kuiacha
huru ifanye kazi iliyopewa.
Hivyo waliopendekeza majina ya
wajumbe hawa wasitarajie kuwa wajumbe watafanya watakayo wao kwani tume
hiyo ni ya watanzania wote na si watu wachache
Nionavyo, kauli
ya Jaji Warioba ya kutaka wawe huru ilikuwa na dhamira nzuri lakini
bado kauli hiyo inachangamoto kubwa kwani inaweza kutafasiriwa kuwa
tume itapenda iachwe iandike Katiba ya watanzania bila kusukuma na mtu
yeyote.
Uundaji wa katiba ni nguzo na ujezi wa muafaka wa kitaifa na hakuna makubalino yanayoweza kupatikana bila msukumo wa wananchi.
Ingawaje
tume imetaka iwe huru lazima muwasikilize wananchi kwa kupokea maoni
yao bila ya upendeleo wowote ili iweze kutenda haki na kahakikisha
watanzania wanashiriki mchakato huo.
Kwa kufanya hivyo mtaweza
kuleta katiba mpya ambayo itaijenga Tanzania mpya yenye usawa katika
nyanza zote za kisiasa, kimila na utamaduni, bara na visiwani pamoja na
usawa dini.
Tunawaamini na kuwategemea kwani mchakato huu ni
muhimu na nyeti kwa mustakabali wa taifa, bila katiba iliyo bora
hatuwezi kuijenga Tanzania iliyo safi.
Aidha ili muweze kufahamu watanzania wanahitaji nini lazima mtoe elimu ya kutosha ili waelewe umuhimu wa wao kushiriki.
Kwa kukafanya hivyo mtawasaidia wananchi kuwa na ufahamu na uhuru wa kutoa maoni bila ya kukwazwa kuzuiwa au kutishiwa.
Kwani
Watanzania waliowengi hasa waishio vijijini bado hawajui katiba nini
na wala hawajui umuhimu wake kwao, hivyo elimu kwao ni muhimu kabla ya
kuomba maoni yao.
Mwenyekiti wa Tume na wajumbe wako muelewe kwamba tume hiyo ni nguzo ya mchakato wa katiba mpya waipendayo watanzania.
Ndani
ya miezi 18 mliyopewa kukamilisha zoezi hilo ni imani ya watanzania
muundo wa katiba inayokuja itakuwa imeboreshwa mazuri, imeondoa
mapungufu ili kujipima tulikotoka na tuendako.
Naamini wajumbe
wote wa tume wana sifa na uwezo mkubwa kiasi kwamba kama watazingatia
misingi mikuu ya uundaji wa Katiba Mpya na ya Kidemokrasia inaweza
kufanya kazi hiyo nzuri.
Aidha nawapongeza na kuwatakia kila la
kheri wajumbe wote waliochaguliwa kulitumikia taifa letu kwa kusimamia
na kuakikisha kuwa Watanzania wanapata katiba mpya ambayo itakidhi
mahitaji yao.
Ni rai yangu kwa wananchi kujitokeza na kuwapa
ushirikiano watakapohitaji ili kurahisiha mchakato wa kupata katiba mpya
kwa maendeleo ya nchi yetu.
|
Posted: 16 May 2012 11:58 PM PDT
Mwenyekiti
wa TPAWU Taifa,Bw. Jaicy Kayera (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa chama
hicho, Bw. Kabangwe Ndebile katika moja ya kikao.
|
Posted: 16 May 2012 11:50 PM PDT
Na Anneth Kagenda
TATIZO
la ajira kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa limeendelea kuwa sugu
nchini huku idadi ya watanzania ikifikia milioni 42 hali inayoweza kuwa
mbaya zaidi baada ya mika mitano.
Pia, umaskini umeshika kasi
Tanzania licha ya kuwa na rasilimali nyingi, ikiwamo ardhi yenye rutuba,
bahari, mito na maziwa, madini na wanyamapori.
Ongezeko
la watu nchini haliendani na maendeleo ya kiuchumi na kusababisha
umaskini hasa kwa vijana kuwa kubwa kuliko jitihada za kulimaliza tatizo
hilo.
Kila mwaka vijana 8000 wanaomaliza katika vyuo vya ualimu
nchini hupokelewa ajili ya kupewa ajira za ualimu pamoja na kwamba bado
hazitoshi.
Utoaji wa ajira hizo ni lengo la serikali ambayo
imekuwa ikitaka kumaliza tatizo hilo kwa vijana pamoja na kwamba
jitihada hizo bado hazijakidhi mahitaji kwa walengwa.
Kutokana na
kuwapo kwa tatizo la ajira nchini na kwa baadhi ya nchi nyingine
duniani, ajira zinazotolewa na serikali huwa hazikidhi mahitaji ya
walengwa.
Pia tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa likiongezeka
kila mwaka hususan mjini kutokana na vijana wengi kukimbia vijijini
kufuata huduma muhimu za jamii.
Wengi wao hukimbilia mijini kwa
kudhani kwamba wanaweza kupata ajira kirahisi jambo ambalo sio kweli na
badala yake huishia katika makundi ya uhalifu na vijiweni wakipiga debe.
Katika
kukabiliana na changamoto hii, serikali haiko peke yake badala yake ina
wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambao hawapendi kuona
vijana wakizurura na kushinda vijiweni.
Taasisi na wadau hao
wamekuwa wakijitahidi kutafuta miradi, kwenye viwanda na maeneo mengine
ili vijana wajishughulishe wakati wote pamoja na kwamba jitihada hizo
bado zinaendelea kutokana na kwamba mahitaji bado ni makubwa.
Meya
wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Antony Amani, anasema, baada
ya kuona tatizo hilo limekithiri aliamua kutafuta mbinu kupambana nalo.
Anasema,
baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo mwaka 2011 alikumbana na changamoto
nyingi na kubwa ambazo alitakiwa kuhakikisha zinapungua kama siyo kuisha
kabisa.
"Changamoto ya kwanza niliyokumbana nayo uso kwa uso na
ikanishangaza ni ile ya upungufu wa watu wenye hati za kumiliki ardhi
ambapo tangu dunia inaumbwa nilikuta idadi ikiwa ni watu 4,881 wenye
hati za kumiliki ardhi," anasema Dkt. Amani.
Anasema kuwa, kwa
uzoefu wa siku nyingi alionao hakutegemea Manispaa kama hiyo kubwa iwe
na hati kidogo kiasi hicho hivyo kujiapiza kwamba suala hilo lazima
alivalie njuga.
"Na cha kushangaza zaidi kumbe kuna watu
waliowahi kulizwa na wajanja wa mjini ambapo mwaka 2003 waliambiwa
kwamba watu 8000 watapewa viwanja kumbe ulikuwa uongo," anasema.
Anaeleza kuwa, mgogoro huo uliodumu kwa miaka 8 huku mapato ya ndani yakiwa ni milioni 9 kwa mwaka.
Anasema
kuwa, aliamua kuungana na watendaji kuingia kwenye mkakati wa kuanza
kutafuta fedha kwa lengo la kuanza rasmi kupima viwanja na ambapo jumla
ya sh. bilioni 2.9 zilipatikana kutoka Unity Trast Of Tanzania (UTT).
"Fedha
hizi zilipatikana na tukaanza kulipa fidia na kupata viwanja,
kutengeneza barabara katika maeneo ambayo viwanja vinapimwa ili paweze
kufikika kwa haraka," anasema Meya huyo.
Anasema kuwa lengo la
kufanya hivyo ni kupima viwanja 5000 ndani ya miaka miwili na
kuwakabidhi wananchi hati zao ili wapate mikopo kupitia hati hizo.
Anasema,
zoezi hilo linaendelea vizuri na watu wanaendelea kununua viwanja huku
barabara zikiendelea kutengenezwa katika maeneo yote ya Manispaa yake
kuzunguka mji wa Bukoba.
Anasema kuwa, changamoto nyingini ni ile
ya mapato kidogo ambapo alisema kuwa baada ya kuliona hilo alitambua
wazi kwamba tatizo linatokana na wawekezaji kuwa wachache hivyo ameanza
maongezi na mashirika mbalimbali pamoja na taasisi.
"Nilizungumza
na shirika la Nyumba NHC, PPT na PSPF na kuyashawishi yajenge nyumba
ili kuwakopeshe wananchi wote ambao watalipa kwa awamu kadhaa na ndani
ya miaka miwili mambo yatakuwa mazuri," anasema Dkt. Amani.
Anasema,
katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa ajira, amelenga
kukuza uchumi kwa wanabukoba ambapo amelenga kuwasaidia wananchi zaidi
ya 2000 kupata ajira.
Anasema, atahakikisha anakuza pato la
mwananchi wake ambapo amelenga mwananchi apate pato kutoka sh. 400,000
za sasa hadi kufika 650,000 pamoja na kutengeneza vitega uchumi ambavyo
vitamsaidia kufikia hapo na kukuza uchumi kwa kasi ikiwa ni pamoja na
wananchi kupata ajira.
"Kwa kufanya hivyo hautakuta vijana wangu
na wananchi kwa ujumla wanalanda landa bila kazi yoyote na hilo ndilo
ninalosema katika ukuzaji wa uchumi na ajira kwa wanabukoba lakini ajira
hizi lazima ziwepo kutokana na kwamba zoezi hilo linaweza kwenda ili
kupambana na tatizo la ajira ambalo ni changamoto kubwa, kinacholengwa
kufanyika hivi sasa ni kuhamishwa kwa stendi ya Bukoba Mjini na
kuipeleka eneo la Kyakailabwa.
Anasema, baada ya kupelekwa kwa
stendi hiyo vijana watapata ajira kubwa kutokana na mabasi yatakapokuwa
yakifika kutoka katika mikoa mbalimbali watatakiwa kuwabeba kwa kutumia
usafiri wa aina mbalimbali wasafiri wanaorudi na kwenda kwenye safari
zao.
Anaongeza kuwa katika stendi ya Kyakailabwa biashara nyingi
zitakuwa zikifanyika na vijana wengi wataweza kujiajiri kupita
kitegauchumi hicho kuliko kuendelea kukaa bila kazi kama hali ilivyo
sasa.
Anasema kuwa vile vile katika soko la Kyakailabwa
wanategemea kujenga shoplaite kubwa, mzuri na ya kisasa ambayo itatumiwa
na wananchi pamoja na Jeshi.
"Jengo litakalojengwa ilipo stendi
litakuwa ni kubwa, zuri na litakuwa na vitengo tofauti tofauti vya
kufanyia shughuli za uzalishaji lakini pia litatoa hata ajira kwa vijana
kwani lazima wasomi na vijana wengine wajishughulishe humo," anasema.
Kwa
upande wa elimu anasema kuwa Manispaa imeanzisha Chuo cha Ualimu hivyo
vijana wengi wataweza kujiunga katika chuo hicho na siyo kuangaika huko
na kule.
"Pia tuna Tawi la Tumaini ambalo tunategemea lianze
Septemba, 2012 lakini pia kwa upande wa shule za manispaa hatuna tatizo
lolote kwani tumepata ufaulu wa asilimia 83 huku tukiwa na vyumba vya
madarasa kwa asilimia 100 hivyo hatuna upungufu wowote" anasema.
"Mimi
nimetembea nchi nyingi na nimeona majengo makubwa na mazuri hivyo
tunampango wa kujenga soko ambalo ni la kisasa na la kimataifa ambalo
kwa hapa Tanzania halipo," anasema Dkt.Amani.
Anatoa wito kwa wazawa wa Mkoa huo kutoukimbia mji huo na kuwataka wafike kwa ajili ya kuwekeza, kujua maendeleo ya mkoa wao.
"Lakini
pia si tu wazawa bali tunawakaribisha hata watu wengine kwa ajili ya
kuja kuangalia maendeleo yetu hata wale wa nchi jirani kwani kutoka
bukoba hadi huko ni kilometa 290 wakati ni karibu sana kutoa bukoba hadi
Kigali hivyo waje," .
|
Posted: 16 May 2012 11:49 PM PDT
Meya wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Dkt.Antony Amani, akichangia mada kwenye moja ya mikutano ya maendeleo.
|
Posted: 16 May 2012 11:38 PM PDT
Mfanyabiashara
ya miche ya michaichai akimshawishi mteja aliyeko ndani ya gari kununua
miche hiyo, kama alivyokutwa makutano ya Barabara za Nyerere na Lugoda,
Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 16 May 2012 11:34 PM PDT
Na Nyakasagani Masenza
KITUO
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesifia ushirikiano mkubwa kinaoupata
kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO)
katika kuhamasisha uwekezaji nchini.
Pongezi hizo zilitolewa na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Raymond Mbilinyi, wakati wa
uzinduzi wa ripoti ya taasisi hizo mbili za uwekezaji Afrika 2011 na
taarifa ya ufuatiliaji wa hali ya uwekezaji iliyofanyika jana jijini Dar
es Salaam.
"Uhusiano kati
ya TIC na UNIDO ni wa muda mrefu tangu mwaka 2000, tunatarajia kuwa
tutaendelea hivyo ili kuhamasisha uwekezaji endelevu hapa nchini,"
alisema Bw. Mbilinyi.
Alisema kwa msaada wa UNIDO, umewezesha
kituo hicho kuhakiki miradi iliyosajiliwa na TIC na kuthibitisha kwamba
karibu asilimia 80 ya miradi hiyo inafanya kazi.
Aliongeza kuwa
kupitia UNIDO, kituo hicho kiliweza kuendesha mafunzo ya kuendeleza
biashara nchi nzima na kusaidia kuendeleza miradi 400 ambapo miradi 80
ilichaguliwa na kuendelezwa zaidi na kuifanya iweze kukopesheka,
kutafutiwa masoko na kuunganishwa na wadau wengine ndani na nje ya nchi.
"UNIDO imeendelea kuisaidia TIC katika kujenga uwezo wa wafanyakazi wake hadi sasa," alisema.
Kwa
upande wake, mwakilishi wa UNIDO nchini, Bw. Emmanuel Kalenzi, alitoa
shukrani zake kwa kwa TIC kwa kuongoza taasisi nyingine kwa niaba ya
serikali katika utafiti huo wa masuala ya uwekezaji.
Waziri wa
Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu, alisema
ingawa Tanzania imeweza kuvutia mitaji ya uwekezaji toka ndani na nje ya
nchi, bado haijaweza kufahamika hasa ni miradi mingapi inafanya kazi
vizuri na ni thamani kiasi gani imeingiza kwenye uchumi.
|
Posted: 16 May 2012 11:33 PM PDT
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akimsikiliza Mkururugenzi wa
Mawasiliano wa Shirika la Utafiti na Tiba Afrika (AMREF), Bi. Wanjiru
Ruhanga, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya miaka mitatu ya Kuchangia
Mafunzo ya Wakunga Nchini, Dar es Salaama juzi, utakaoratibiwa na
shirika hilo ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. (Picha na Charl;es
Lucas)
|
Posted: 16 May 2012 11:29 PM PDT
Na Thomas Dominick Musoma
MAKADIRIO ya Rasimu ya bajeti ya Mkoa wa Mara kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013,kwani
mkoa umeomba kuidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 163 sawa na
ongezeko la asilimia 22.5 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2011/2012.
Akisoma makadirio ya bajeti hiyo Katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) Ofisa Mipango wa Mkoa huo, Bw. Nesphory Bwana alisema kuwa sehemu kubwa ya ongezeko la bajeti hiyo ni mishahara iliyoongezeka kwa asilimia 44.7. ongezeko hilo la mishahara limetokana na muundo mpya wa sekretarieti ya mkoa na halmashauri ambapo jumla ya watumishi 152 wataajiriwa na sekretarieti ya mkoa na watumishi 2,607 wataajiriwa na katika halmashauri za wilaya.
Alisema sh.bilioni 103.456 ni kwa ajili ya mishahara, bilioni 18.238 kwa ajili ya matumizi mengineyo, bilioni 31.324 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na bilioni 10.443 ni makusanyo ya vyanzo vya ndani
“Pamoja na maombi hayo hapo juu, Mkoa wa Mara unaomba kiasi cha bilioni 22.573 kama maombi maalumu kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Sekretarieti ya mkoa na halmashauri zake,”alisema Bw. Bwana.
Alisema kuwa bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vya wananchi toka katika ngazi za msingi yaani vijiji, mitaa na kata ushauri toka katika wizara mama ya OWM- TAMISEMI na wizara za kisekta, wizara ya Fedha, Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Mabaraza ya Madiwani na kamati za kudumu halmashauri.
Pia alisema kuwa imezingatia mawazo na mapendekezo ya wadau mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara, wenye viwanda, sekta ya kilimo, utalii na wengine wengi.
Awali akifungua mkutano huo Mkuu wa Mkoa huo Bw. John Tuppa aliwaomba wajumbe na kujadili kwa kina na kutoa maamuzi sahihi yatakayosaidia mkoa huo na kupewa baraka na wajumbe hao.
“Ukomo wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13 tuliopewa Serikali ni sh. bilioni 163 ambao ni ongezeko la bilioni 32 ya bajeti ya mwaka jana, ambapo ongezeko hilo lipo kwenye mishahara, matumizi ya kawaida imepungua kwa asilimia 40 ambapo katika utendaji kutakuwa na kazi kweli,”alisema Bw.Tuppa.
Alisema
kuwa makusanyo ya ndani ndiyo yatakayookoa mkoa kwani alidai kuwa hii
inatokana na fedha za uendeshaji na maendeleo kuwa ndogo.
|
Posted: 16 May 2012 11:28 PM PDT
Katibu
Mkuu wa Chama kipya cha siasa nchiniAlliance For Democratic Change
(ADC) Bw. Lucas Kadawi Limbu, akipokea kadi kutoka kwa kundi la wasanii
wa Magu One Theatre na kuwakabidhi kadi mpya za ADC mjini Magu hivi
karibuni baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mkoani Mwanza. Picha na
David Magesa
|
Posted: 16 May 2012 11:20 PM PDT
Na Heri Shaaban Dar es Salaam
WAKUU wa Wilaya za Dar es Salaam wameagizwa kusimamie mfumuko wa bei ya vyakula katika masoko ya wilaya zao.
Agizo hilo limotolewa na Mkuu wa mkoa huo Bw.Meck Sadik mara baada kuwapisha wakuu wa wilaya zake.
Bw.Sadik
alisema kuwa kutokana na mfumuko wa bei katika bidhaa,anawagiza kutoa
kipaumbe kushughulikia suala hilo kwa kufanya ziara katika masoko na
kuangalia bei ya vyakula.
Alisema kuwa katika masoko ya mkoa
huo bei ya unga sembe kilo moja inauzwa shilingi 1200 hadi 1400 jambo
ambalo wananchi wengi wanashindwa kumudu ukali wa gharama za maisha na
kulazimika kula mlo mmoja kwa siku.
"Serikali imeshasambaza
mahindi mengi kutoka katika Ghala la Serikali kwa kuwapa
wafanyabiashara wakubwa kama Bakhresa hivyo kwa sasa unga wa sembe
utauzwa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo,"alisema Bw. Sadik.
Aliwataka wakuu wa wilaya hizo wawe na utaratibu ya kutembelea masoko na kuangalia bei za bidha zinazopanda mara kwa mara.
Alisema
wafanyabiashara wote watakaouza unga sembe kwa bei kubwa badala ya bei
ya serikali watachukuliwa hatua huku leseni zao zikikamatwa.
|
Posted: 16 May 2012 11:18 PM PDT
Mwanafunzi
akitambaa juu ya kamba wakati wa mashindano ya skauti, mafunzo haya
huwasaidia vijana kuwa wazalendo na nchi yao na wapenda amani.( Picha na
mtandao)
|
Posted: 16 May 2012 11:10 PM PDT
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MRADI wa kuzuia maji ya baharini ili yasiingie katika makaazi ya wananchi umeshindwa kutekelezeka baada ya fedha zilizoombwa kukamilisha mradi huo kutowafikia walengwa.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi jimbo la Kikwajuni Bw. Mahmoud Mohammed Mussa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa wakati alipofanya ziara kwenye maeneo ya Binguni na Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Bw. Mussa alisema kuwa kabla ya kuanzishwa mradi huo wananchi waliiomba jumla ya shilingi milioni 780 Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa lengo la kutekeleza mradi huo. Hata hivyo alisema kuwa ofisi hiyo ilituma shilingi milioni 531 lakini hazijuulikani wapi zilipofikia na kuwa zinatarajiwa kuundiwa mradi mwingine jambo ambalo wananchi hawakubaliani nalo. “Kimsingi mradi umeshindwa kutekelezeka na tunachohoji wapi fedha hizo zimekwenda,” alisema Mwakilishi huyo. Alisema kuwa kutokana na kuwepo uvumi huo kinachotakiwa kujuulikana fedha hizo zimetumwa wapi ili wananchi hao waweze kuendeleza azma yao. Tunajua fedha zimetumwa lakini wapi hatujui na kama zipo ni kwanini utafutwe mradi mwingine wakati walioomba ni wananchi wa jimbo la Kikwajuni hii kwa kweli sio sawa,” alisema.
Hata hivyo akizungumza mbele ya kamati hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Bi. Sihaba Haji Vuai alisema kwamba kiasi hicho cha fedha kinasubiriwa ili kutengeneza maeneo ya malindi ambayo kuna njia imekatika.
|
No comments:
Post a Comment