Kiingilio
kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya wanawake
(Twiga Stars) na Afrika Kusini (Banyana Banyana) itakayochezwa Jumalipi
(Mei 20 mwaka huu) ni sh. 1,000.
Mechi
hiyo ambayo ni sehemu ya maandalizi kwa timu hizo zinazoshiriki
mashindano ya Afrika itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 10.30 jioni. Viingilio hivyo ni kwa maeneo yote, isipokuwa VIP A
ambapo itakuwa sh. 10,000 na VIP B sh. 5,000.
Baada
ya mechi hiyo, Twiga Stars itakwenda Ethiopia kwa ajili ya mechi ya
mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
itakayochezwa Mei 27 mwaka huu jijini Addis Ababa.
Tayari
Meneja Usalama wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA), Percy
Makhanya ameshawasili nchini kuratibu ujio wa Banyana Banyana. Timu hiyo
pia iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya Fainali za Nane za
AWC ambapo katika raundi hii ya pili imepangiwa Zambia na itaanzia
mechi hiyo ugenini jijini Lusaka.
No comments:
Post a Comment