Timu
ya Taifa ya wanawake ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) inatarajia
kuwasili nchini leo (Mei 18 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ajili ya
mechi ya kirafiki dhidi ya Twiga Stars itakayofanyika Jumapili (Mei 20
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Banyana
Banyana ina msafara wa watu 26 ambapo 18 kati ya hao ni wachezaji na
itafikia kwenye hoteli ya Sapphire Court Hotel tayari kwa mechi hiyo ya
kujipima nguvu kwa Twiga Stars inayojiandaa kwa mechi ya mchujo kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya
Ethiopia. Mechi dhidi ya Ethiopia itachezwa Mei 27 mwaka huu jijini
Addis Ababa.
Nayo
Banyana Banyana iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya
Fainali za AWC ambapo katika raundi hii ya pili imepangiwa Zambia na
itaanzia mechi hiyo ugenini jijini Lusaka.
Kesho
(Mei 19 mwaka huu) saa 6 kamili mchana, makocha wa timu zote mbili,
Boniface Mkwasa wa Twiga Stars na Joseph Mkhonza wa Banyana Banyana
watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzungumzia mechi hiyo.
Twiga
Stars na Banyana Banyana zote ziko katika raundi ya mwisho ya AWC
ambapo zikifanikiwa kuwatoa wapinzani wao zitakwenda kwenye fainali hizo
zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment