NA MWANDISHI WETU
RAIS Jakaya Kikwete
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Warsha ya siku moja itakayojadili ukuwaji
wa uchumi na changamoto zake, itakayofanyika Mei 24 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Akizungmza leo na wandishi wa habari,
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii Nchini (ESRF), Dk.
Bohela Lunogelo alisema wameandaa warsha ambayo inatarajiwa kuwakutanisha wadau
ambao watachangia mada mbalimbali.
Alisema mada zitakazo
jadiliwa siku hiyo zimegawanyika katika sehemu kuu tatu ambapo zote zinahusiana
na tafiti mbalimbli zilizofanyika kwa lengo la kuimarisha ukuaji uchumi katika
jamii.
Dk. Lunogelo alisema
ukiachilia mbali Rais pia atakuwepo Profesa Benno Ndulu ambaye Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania na Dk. Huang Chengwei ambaye ni mtaalamu anashughulika na
kuondoa umasikini nchini China.
Alisema kuwepo kwa Dk.
Chengwei kutasaidia Watanzania kufahamu mambo mengi ambayo Wachina wameyapitia
hadi kupata mafanikio katika uchumi.
Adha, alisema mambo ya
takayojadiliwa na wataalamu siku hiyo yatakuwa ni pamoja na madini ukuaji wa
viwanda na utalii maswala ya usimamizi wa ardhi na ukuaji wa kilimo.
Mengine ni kuhusiana
uongozi, utawala bora na maswala ya miundombinu na uendeleza wa rasilimali na
mengineyo.
No comments:
Post a Comment