Katibu Mkuu wa timu ya Simba Bw. Evodius Mtawala aelezea mipango ya kuuhifadhi na kuusafirisha mwili wa
mchezaji wao marehemu Patrck Mafisango Mutesa aliyeafiki alfajiri ya
usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chang'ombe Veta jijini Dar es salaam,
wakati akirejea nyumbani kwake na kusababisha watu wengine aliokuwa nao
kupata majeraha.
Bw. Mtawala amesema hayo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na
kueleza kwamba kwa sasa wanawasiliana na Ubalozi wa Rwanda na mashirika
ya ndege ili kukamilisha utaratibu wa vibali mbalimbali tayari kwa
kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda nchini Rwanda kwa mazishi na
taarifa kamili ya lini utasafirishwa itatolewa kesho mara baada ya
kukamilika kwa taratibu zote, katika picha kushoto ni Bw. Mwakitalima
mmoja wa mashabiki wa Simba aliyefika muhimbili kushuhudia kilichotokea.
Mchezaji wa timu ya Simba Haruna Moshi Boban akilia kwa uchungu huku
akifarijiwa na jamaa na marafiki baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji
mwenzao marehemu Patrick Mafisango katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili .
Wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga kushoto na Uhuru Selemani wa Simba
wakisikitika wasijue la kufanya baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji
mwenzao marehemu Patrick Mafisango katika chumba cha kuhifadhia maiti
muhimbili leo.
Mbunge wa jimbo la Korogwe CCM Steven Ngonyani Prof Maji Marefu
akizungumza na wanahabari hospitalini hapo kuelezea masikitiko yake juu
ya kifo cha mchezaji huyo.
Haruna Moshi akitoka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti huku akilia kwa
uchungu baada ya kuhakikisha kweli mwenzao Patrick Mafisango amefariki.
Hapa Haruna Moshi akihojiwa alijaribu kuongea lakini akashindwa.
Mchezaji Uhuru Selemani akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji.
Mchezaji wa zamani wa Simba Boniface Pawasa akilia kwa uchungu huku
akifarijiwa na Mchezaji haruna Niyonzima wa Yanga, Pawasa amesema jana
walikuwa naye kwenye muziki katika klabu ya Maisha Oysterbay wakati
bendi ya Akudo Impact ikifanya onyesho klabuni hapo na marehemu alimuaga
kwamba anaenda nyumbani baadae akapigiwa simu kwa simu ya marehemu
akiambiwa mwenye simu hii amefariki dunia kwa ajali.
Boniface Pawasa kushoto, Uhuru Selemani wakilia.
Uhuru Selemani akisalimiana na wanamuziki wa bendi ya Akudo Impact
ambao pia wameelezaea masikitiko yao kwani wamesema marehemu walikuwa
naye usiku wa kuamkia leo katika klabu ya Maisha ambako walikuwa
wakifanya onyesho lao.
Aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Simba Mrundi Ramadhana Wasso
akihojiwa na waandishi wa habari kuelezea masikitiko yake kutokana na
msiba huo.
Mashabiki wa Simba wakiwa katika hospitali ya Muhimbili kwa masikitiko makubwa kwa kuondokewa na mchezaji wao kipenzi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment