Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Dr Florens
Turuka akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa warsha
ya siku mbili kuelekea kilele cha siku ya sherehe ya mawasiliano duniani
ambapo maadhimisho hayo yanatarajiawa kufanyika kesho Duniani kote, Dk
Turuka amewaomba wafanya biashara wauze televisheni ambazo zipo katika
mfumo wa Digital. Warsha hiyo imeanza leo hii katika Ukumbi wa
Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Prf, John Nkoma
akizungumza na waandishi wa habari leo hii jijini Dar es Salaam kwenye
Semina inayoambatana na Sherehe ya siku ya mawasiliano Duniani. ambapo
amewataka watanzania kuelewa umuhimu wa mawasiliano ya mtandao.
Baadhi ya wadau mblimbali wa mawasiliano nchini waliohudhuria kwenye
warsha hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mapinduzi Zuwena Muddy, akitoa mafunzo ya
namna ya kutumia Computer kwa wadau waliohudhuria kwenye semina hiyo.
Mwanafunzi Jackson Joseph kutoka shule ya Msingi Mapinduzi jijini Dar
es Salaam manispaa ya Ilala, akihojiwa na waandishi wa habari juu ya
faida ya matumizi ya Computer.
Mwanafunzi Zuwena Muddy akisisitiza jambo katika mafunzo hayo kwenye warsha hiyo.
RAIS DK SHEIN AFANYA UTEUZI ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohd
Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za
Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi
na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Dkt Shein
kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (4) cha katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984, Rais amemteuwa Mdungi Makame Mdungi kuwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar.
Aidha Dkt. Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha
61 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amemteuwa Khamis Jabir
Makame kuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 16 Mei 2012,
Lowassa kuongoza harambee kuchangia elimu Kipawa
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu aliyejiuzuru ambaye ni Mbunge wa Monduli, Edward
Lowassa anarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya mpango wa
kuboresha elimu Kata ya Kipawa Ilala Dar es Salaam.
Hayo yalibainishwa na Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema ameandaa chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuboresha elimu katika Kata yake ya Kipawa.
"Hafla hiyo itafanyika juni 6 mwaka huu katika hoteli ya
Kilimanjaro Kempinski na mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Monduli Edward
Lowassa"
Alisema hatua hiyo imefikiwa kufuatia juhudi zingine alizozifanya
kwa ajili ya kata hiyo ambapo machi 17,2012 aliitisha matembezi ya
hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Katika matembezi hayo mama Salma alichangia sh.milioni 3, Clouds
Media Group milioni 1, wakati viongozi wa Serikali walioongozana naye
walichangia sh.milioni 10 ambapo jumla yake ilikuwa sh. milioni 15.
Alisema aliguswa na jambo hilo baada ya kubaini changamoto nyingi
hasa za elimu kwenye kata hiyo yenye jumla za shule za msingi 7 mbazo
zinaupungufu wa madawati 5000, matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa na
kutokuwa na maji.
Alisema jumla ya sh.bilioni moja zinahitajika ili kufanikisha
mpango huo ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi, mashirika ya
umma, Taasisi za dini, makampuni, viongozi mbalimbali na Asasi zisizoza
kiserikali Ng'os kujitokeza kwenye harambee hiyo ili kufanikisha mpango
huo.
Diwani Kaluwa aliwashukuru wote waliojitokeza kufanikisha matembezi
ya awali na wale wanaendelea kufanikisha maandalizi ya chakula cha
hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko huo.
Dk Shein afanya mazungumzo na Wizara ya Viwanda.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashra,Viwanda
na Masoko,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko
Ikulu Mjini Zanzibar leo. [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]

ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na
Sheria,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu
Mjini Zanzibar leo. [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na
Sheria,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu
Mjini Zanzibar leo. [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
WAFUGAJI NYUKI WAKUTANA NA WAZIRI MKUU PINDA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wafugaji wa nyuki kutoka
Pemba na Rufiji waliomtembelea nyumbani kwake Dodoma kwa ziara ya
kujifunza ufugaji nyuki iliyodhminiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF), May 15,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wafugaji
nyuki kutoka Pemba na Rufiji waliotembelea shamba lake la nyuki ili
kujifunza May 15, 2012. Kushoto kwake ni Ladislaus Mamanga ambaye ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao ulidhamini
safari hiyo na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ,
Juma Kassim Tindwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NI WIKI YA TATU SASA SERENGETI YATANGAZA WENGINE WAWILI WABORESHEWA MAISHA
Meneja
wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo katikati akiongea na waandishi wa habari
wakati wa kutangaza washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya VUMBUA HAZINA
CHINI YA KIZIBO inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Mkaguzi kutoka bodi ya taifa ya
bahati nasibu, Bw. Abdallah Hemedi kulia akikagua jinsi droo hiyo inavyochezeshwa.
Kushoto ni meneja wa bia ya Serengeti Bw Allan Chonjo na katikati ni mwakilishi
kutoka PWC Bw.Tumainieli Malisa.
Ni katika droo ya tatu ya promosheni ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL.
Wiki mbili zilizopita zilikuwa za aina
yake baada ya kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kuendelea kukonga nyoyo
za wateja wake na watanzania kwa ujumla kwa kuwapa zawadi washindi wa
promosheni inayoendelea inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya
kizibo’ ambapo watanzania wengi wameshuhudia kampuni hiyo ikiwakabidhi
washindi wa promosheni hiyo zawadi zao katika promosheni hii kubwa.
Amadeus Minja na Agness Msengi wakazi wa
Dar es salaam, walijishindia jenereta (kangavuke) kubwa ambapo
walikabidhiwa zawadi hizo mwisho mwa wiki iliyopita. Ibrahim Kimambo
mkazi wa tabata jijini Dar es salaam alibahatika kujinyakulia pikipiki
mpya na ya kisasa ambapo naye alikabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki
iliyopita katika ukumbi unaovuma sana ujulikanao kama Dar LIVE pale
Mbagala Zakhem.
Bw.
Ibrahim ambaye hakuwa na kazi yoyote mpaka bahati iliyobebwa na
promosheni hii ilipomdondokea alikuwa na haya ya kusema, “kwa kweli
nilipopata taarifa ya kushinda zawadi ya pikipiki sikuamini lakini sasa
nimeamini na nawashukuru sana SBL kwa kuwa sasa naweza kujiajiri na
kuendeleza maisha yangu na wale wanaonitegemea”. Kutoka jijini Mwanza
Godfrey Shao ambaye alijinyakulia bajaj ya gurudumu tatu anaendelea
kusubiri taratibu za usajili zikamilike ili aweze kukabidhiwa bajaj
yake.
Asubuhi ya leo droo
ya tatu katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’
imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo
maeneo ya Oysterbay jijini.
Droo hiyo ya tatu kama ilivyo kawaida
katika droo zilizopita, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi
kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya
kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH
MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers
kuhakikisha washindi wote watapatikana kihalali.
Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium
Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima
ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ Na kuleta mabadiliko
yakinifu kwa wateja wake.
Akiongea na waandishi wa habari katika
hafla hiyo, Mkurugenzi wa mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya SBL Bi.
Teddy Mapunda, amesema kwamba “mpaka sasa tumeshawapata washindi wawili
wa jenereta ambao tayari tumewakabidhi zawadi zao, wengine ni washindi
wa bajaj moja na wa pikipiki moja ambao nao wameshakabidhiwa zawadi zao”
“Tunawashauri wateja wetu na watanzania
wote wenye sifa za kushiriki katika promosheni hii ya aina yake
waendelee kushiriki bila kukata tamaa na hatimaye nao waweze kushinda
kwani promosheni yetu ni ya kweli na ya uhakika.” alisema Mapunda na
kuongeza kuwa mpaka sasa tayari watu zaidi ya 2000 wamejishindia pesa
taslimu na wakafanikiwa kupata pesa hizo kwa urahisi kabisa kupitia
mtandao wa kutuma na kupokea pesa wa kampuni ya mawasiliano ya simu za
mkononi Vodacom MPESA ndani ya masaa ishirini na nne. Pia, washindi
wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika
promosheni hiyo.
Washindi wetu katika droo ya tatu ni
Fadhili Manzi mkazi wa Mafinga mywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager
nambaye amejishindia bajaj na Raymond Denis mkazi wa Iringa ambaye
amejinyakulia jenereta kupitia bia ya Tusker Lager.
MAELEKEZO:
Nunua bia ya Serengeti lager, Tusker
lager au Pilsner Lager fungua kisha angalia chini ya kizibo utapata
namba zilizopo chini ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi
kwenye simu yako, nakili namba zilizochanganyika na herufi mfano AB55550, kisha
tuma kwenda namba 15317 na unaweza kujishindia pesa taslimu kati ya
shilingi 10,000, 50,000 au 100,000 au unaweza kujipatia bia ya bure kati
ya bia zilizoainishwa katika promosheni hii . Fanya
hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti.
Wanaoruhusiwa kushiriki promosheni hii ni walio na umri wa miaka kumi
na nane na kuendelea.
NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MKOA WA MTWARA
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali (Mst) Joseph Simbakalia
akisalimiana na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo huku
wakishuhudiwa na Meneja wa Mahusiano Bi. Shy-Rose Bhanji wakati wa
kukabidhiwa msaada wa Madawati kwa Shule za Mkoa wa Mtwara.
(Picha zote na Beatha Hyera, Afisa Habari Mtwara)
(Picha zote na Beatha Hyera, Afisa Habari Mtwara)
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Joseph Simbakalia (wa kulia) akipokea mfano wa
hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Meneja wa NMB
Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo wakati wa kukabidhiwa msaada huo
utakozinufaisha Shule za Msingi katika Wilaya za Masasi na Newala.
Meneja
wa Mahusiano Benki ya NMB Bi. Shy-Rose Bhanji akitoa maelezo kwa Mhe.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuhusiana na msaada huo na ushirikiano mzuri
uliopo kati ya Benki ya NMB na wananchi kwa ujumla katika kuhakikisha
maendeleo ya elimu katika nchi yetu.
Rais Kikwete atembelea Ofisi za Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba jijini Dar es Salaam
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alitembelea ofisi
za Tume ya kukusanya na kuratibu maoni juu ya katiba zilizopo katika jengo
jipya katika Wizara ya Mambo ndani jijini Dar es Salaam.Akizungumza na wajumbe
wa Tume hiyo Rais Kikwete alirudia ahadi yake ya kuwapatia nyenzo za kazi
ikiwemo usafiri ili kuiwezesha tume hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.Pichani
Rais akizungumza na wajumbe wa tume hiyo katika ukumbi wa mikutano uliopo
katika jengo la tume hiyo jana.
Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu maoni juu ya Katiba
Jaji Joseph Sinde Warioba(kulia) akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
wakati Rais alipomtembelea ofisi kwake jana.Wengine katika picha ni Makamu
mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mkuu Mstaafu Mhe. Agostino Ramadhani(Watatu
kushoto),Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Mathias Chikawe(Wapili kushoto) na
kushoto ni naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Angela Kairuki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo naProfesa
Mwesiga Baregu ambaye ni mjumbe wa Tume
ya kuratibu maoni kuhusu katiba wakati Rais alipotembelea ofisi za tume hiyo
jijini Dar es Salaam jana(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Wanne kushoto Mstari
wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya kuratibu
maoni ya Katiba wakati alipotembelea
ofisi za tume hiyo Jijini Dar Es Salaam jana.
President Donald Kaberuka Invited To The 38th G8 Summit And To The White House By President Obama
At
the invitation of the President of the United States, the President of
the African Development Bank will be attending the Group of Eight (G8)
meeting
WASHINGTON, May 16, 2012/ -- At
the invitation of the President of the United States, Barack Obama, the
President of the African Development Bank, Donald Kaberuka, will be
attending the Group of Eight (G8) meeting at Camp David in Frederick
County, Maryland on 18 and 19 May.
The
discussions will centre on the subject of food security in Africa and
will also show how Africa's voice is being heard at the highest level.
Donald Kaberuka will also be attending a special luncheon at the White House during his time in the United States.
WAZIRI WA ZAMANI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII DKT. MPONDA AKABIDHI RASMI OFISI
Waziri wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji
Mponda akimkabidhi kitabu cha sheria na mwongozo wa utendaji kazi wa
wizara hiyo Waziri Mpya Dkt. Hussein Mwinyi.Makabidhiano hayo
yamefanyika leo kwenye ukumbi wa wizara hiyo
Mawaziri hao wakipeana mkono mara baada ya makabidhiano hayo Dkt. Mponda
amemtaka waziri Dkt. Mwinyi kufuatilia na kusimamia vyema utekelezaji
wa mikakati ya sekta ya afya ili kuweza kuimarisha huduma ya afya kwa
wananchi
Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi aliyekaa katikati,Kulia ni
waziri wa zamani Dkt. Hadji Mponda na Naibu Waziri Mpya Dkt. Seif Rashid
aliyekaa kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara
hiyo mara baada ya makabidhiano ya ofisi.
Ashindwa kujiunga na Sekondari Handeni kwa kukosa ada
Mwenjuma M. Magalu (kulia) akiwa na Bibi yake nyumbani kwao Kijiji cha Msasa, wilayani Handeni
LICHA ya Serikali kuliarifu Bunge la Tanzania kuwa wanafunzi
wote waliofaulu darasa la saba mwaka 2011 kutoka mikoa 12 tayari wamejiunga na
kidato cha kwanza, imebainika bado kuna wanafunzi wameshindwa kujiunga na shule
kutokana na kipato duni cha familia zao.
Mwenjuma M. Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya
Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni ni miongoni mwa wanafunzi walioshindwa
kujiunga na sekondari kutokana na mama yake kushindwa kumgharamia mahitaji ya
shule.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni
kijijini Msasa, wilayani Handeni, katika utafiti uliofanyika kwa ushirikiano na
Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), mama wa mtoto huyo Hadija Magalu
aliyetelekezwa na mumewe kwa muda mrefu alisema ameshindwa kumsomesha mwanaye
kutokana na kipato duni alichonacho.
Magalu alisema alipata taarifa za kufaulu kwa mwanae tangu
Desemba 12, 2011 na kuanza kujikusanya taratibu lakini hadi muda wa kwenda shule
ulipofika (Januari 9, 2012) alikuwa hajakamilisha baadhi ya vifaa vinavyohitajika
shuleni vikiwemo fedha ya ada na michango mingine.
“Naweza kukuonesha hata baadhi ya vitu ambayo nilikuwa
tayari nimenunua kama sare, kwanja na mahitaji
mengine madogo madogo…aliyenikwamisha na kunivunja moyo ni babayake (baba wa
mtoto), ambaye awali niliwasiliana naye kupitia kwa ndugu zake na kuahidi
angenisaidia ada lakini hakufanya hivyo hadi muda wa kwenda shule ulipofika,”
alisema Magalu.
Mume wa Magalu (jina tunalo) ametelekeza familia yake
(watoto wanne) pamoja na mkewe kwa zaidi ya miaka minne sasa kwa kisingizio
kwamba amekwenda nje ya Wilaya ya Handeni kutafuta maisha, huku mkewe akibaki
akiangaikia familia hiyo.
“Tumekuwa tukisikia tu kwamba ameonekana kijiji fulani
lakini ukifuatilia humpati, na mara nyingi anapowasiliana na ndugu zake ndio
wanatupa taarifa zake…nami niliwasiliana naye mara ya mwisho nikimpata taarifa
za mtoto kufaulu lakini hakutekeleza ahadi yoyote juu ya kunisaidia ada ya
mtoto.
Michango iliyomkwamisha mwanafunzi Mwenjuma Magalu kujiunga
na kidato cha kwanza ni ada ya sh. 20,000, fedha ya taaluma sh. 10,000, fedha
ya madawati 15,000, fedha ya sweta sh.10,000, kitambulisho sh. 5,000, ulinzi
sh. 5,000, tahadhari 5,000 pamoja na fedha kwa ajili ya nembo ya shule sh.
2,000.
Akihutubia Mkutano wa Saba wa Bunge la Tanzania
lililomalizika hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa kutoka mikoa 12 ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa,
Mara, Morogoro, Mwanza, Lindi, Kilimanjaro, Pwani, Ruvuma na
Tanga, wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba wamefanikiwa kujiunga na
Kidato cha Kwanza.
Hata hivyo mwanafunzi Magalu kwa sasa anafanya vibarua kwa
moja ya kampuni za Kichina zinazofanya ujenzi wa barabara inayopita Kijiji cha
Msasa, kwa madai anatafuta fedha za ada na endapo akikamilisha atahakikisha
anaendelea na elimu ya sekondari hapo baadae.
Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuzungumza na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, Hassan Mwachibuzi alisema ofisi yake
haina taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na shule, hivyo kumshauri mwandishi
amueleze mtoto huyo kufika ofisi za halmashauri ili aweze kujieleza na
ikiwezekana kusaidiwa.
“Kama huyo mtoto yupo
mwelekeze aje pale ofisini kuna wataalamu wa utambuzi watamuhoji na kuangalia
namna ya kumsaidia…sisi hatuna taarifa hizo na huenda wahusika wanatuficha,”
alisema kiongozi huyo.
*Habari hii
imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)
kwa kushirikiana na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA
MVUA KUBWA ZILIZONYESHA MJINI BUKOBA ZASABABISHA MAJI KUJAA MITAANI
Nyumba ya mdau Bi Nesi wa Uswahili kwa mama Rujaka ikiwa imezingirwa na
maji kutokana na mvua kubwa inayonyesha kwa mfurulizo mjini Bukoba
mkoani Kagera kama itaendelea kunyesha huenda maafa makubwa yakatokea.
(PCHA KWA HISANI YA BUKOBAWADAU)
Nyingine ni makazi ya watu Eneo la Omukigusha na HAMUGEMBE kando kando ya mto kanoni.
hali iko hivyo maeneo ya Kashai matopeni, Kasalani, na Jamhuri pamoja na maeneo ya Desare Pub na Hotel ya VICTORIUS.
hali iko hivyo maeneo ya Kashai matopeni, Kasalani, na Jamhuri pamoja na maeneo ya Desare Pub na Hotel ya VICTORIUS.
Mwanafunzi akitoka shule akipita kwenye madimbwi ya maji yaliyotokana na mbua hiyo.
Mkazi wa mjini Bukoba akipita kwenye madibwi ya maji yaliyojaa katika mtaa mbalimbali mjini humo.
Maji yakiwa yamezingira vibanda mbalimbali vya biashara kama vinavyoonekana vikiwa vimezingirwa na maji.
NHIF na kuwaenzi wazee kwa matibabu
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umevishauri vituo vinavyotoa huduma kwa wanachama wake ambavyo vimetenga maeneo maalum, kuhakisha vinatoa huduma hiyo kwa wazee katika maeneo hayo ili kuwaepusha na usumbufu wakati wa kupata huduma za matibabu.
Rai hiyo imekuwa ikitolewa kwa nyakati tofauti na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Emanuel Humba wakati wa kutembelea hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizosajiriwa na Mfuko huo kwa lengo la kujionea huduma zinazotolewa kwa wanachama wake.
"Lazima tuwaenzi wazee wetu, wamefanya kazi kubwa ya kuifikisha nchi hii hapa ilipo hivyo kama Mfuko tungependa kuona mahali wanapotibiwa wanachama wetu na wazee wetu nao wapate huduma mahali hapo...si vyema kuona wakitaabika wakati wa kupata matibabu," alisema Humba.
Aliwataka watoa huduma kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali zinazotolewa na NHIF kuboresha huduma za matibabu kwa kuwa na vifaa vya kisasa, dawa na kuboresha mazingira ya vituo hivyo.
"Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa fursa ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ambao unalenga moja kwa moja kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla hivyo ni vyema wazee wetu nao wakapewa heshima kubwa wakati wa kupata matibabu,"alisema Humba.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ameushauri Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ya afya kwa wananchi ili kupunguza gharama za matibabu.
Amesema elimu ya afya itasaidia wanachama na wananchi kwa ujumla kuepukana na maradhi ambayo yanagharimu fedha nyingi kwa ajili ya matibabu.
"Yapo maradhi yanayotokana na mtindo wa maisha kama kisukari, shinikizo la damu ambayo yanaweza kuepukika kwa wanachama wenu kupata elimu tu ya namna ya kula, kufanya mazoezi na mambo mengine,"alisema Manyanya.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, hivi karibuni umeendesha mikutano ya wadau wake katika mikoa mbalimbali nchini,ambayo kwa pamoja wameazimia kuifanya agenda ya Bima ya Afya kuwa ya kudumu.

JK KATIKA SEMINA YA APRM MJINI DODOMA
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimwagiza jambo, Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wa
Utawala bora, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM,
iliyofanyika leo May 15, 2012, kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya CCM,
mjini Dodoma. Semina hiyo iliandaliwa na Mpango wa Hiari wa Nchi za
Umoja wa Afrika kujipima kwa vigezo vya Utawala Bora-APRM. Kulia ni
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. (Picha na Bashir Nkoromo)
Washindi wa Kili Talent search wafikia 12
Washindi kutoka Dodoma kutoka kushoto ni Halima Ramadhani, Juma Madaraka na Issa Dubat
Kutoka kushoto ni Proffesor Jay, Henry Mdimu, Queen Darleen na Juma Nature.
Na Mwandishi Wetu
Washindi wa msako wavipaji unaodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, wiki hii umefikia hatua ya nne ambapo umefanikisha kupata washindi 12 ambao wamepata nafasi ya kurekodi nyimbo zao tayari kwa kuanza safari yao ya kisanii kupitia muziki.
Kwa mujibu wa waratibu wa zoezi hilo kampuni ya Frontline Novelli, tayari usaili umeshapita katika jumla ya mikoa minne na kila mkoa walikuwa wakichukuliwa washindi watatu watatu.
Akiifafanua zaidi kuhusiana na mchakato huo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Frontline, Irene Kiwia alisema washindi hawa watatu wa kila mkoa mara wanapopatikana hupewa nafasi ya kurekodi wimbo, kila mmoja na kisha kufanya wimbo wa pamoja wakishirikiana wote watatu.
Baada ya kurekodi washindi hawa watatu wote wanashiriki katika tamasha la washindi la mkoa huo ambapo kati yao mmoja atakayefanya vema jukwaani ndio anapata nafasi ya kushiriki tamasha kubwa la washindi litakalofanyi9ka mapema mwisho wa mwezi huu jijini dar es salaam.
Mikoa ambayo imeshatembelewa mpaka sasa ni Dodoma, Mwanza, Moshi na Mbeya ambapo washindi wake tayari wamesharekodi na katika mikoa ya Dodoma, Moshi na Mwanza, washiriki wa tamasha kubwa kabisa litakalofanyika mkoani Dar es salaam wameshapatikana.

SAID BONGE WA CLOUDS APANDA MIGOMBA KATIKA BARABARA YA MWANANYAMALA BAADA YA MANISPAA YA KIONONDONI KUITELEKEZA
Mfanyakazi wa Radio Clauds FM, Said Mohamed 'Said Bonge' akipanda
migomba kwenye mashimo ya barabara ya Mwananyamala Hospitali Dar es
Salaam leo huku gari likipiata kando yake. Bonge alisema amechukua uwamuzi huo baada ya wahusika
kushindwa kuyafukia mashimo hayo ambayo yamekuwa yakileta usumbufu kwa
watumiaji wa barabara hiyo.
Said Bonge
akiendelea na shughuli ya kupanda migomba katika barabara ya
Mwananyamala ambayo imeharibika vibaya huku wahusika wakiifumbia macho
bila kuchukua hatua zozote za kuikarabati.
MASHINE CHACHE ZA MIONZI ZACHANGIA KUSHUKA KWA HUDUMA ZA MATIBABU YA KANSA OCEAN ROAD
NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Saratani Ocean
Road, Twalibu Ngoma amekiri kuwa kuanguka kwa huduma za matibabu katika
hospitali hiyo, kumechangiwa na uwezo mdogo wa serikali wa kununua
mashine za mionzi kwa ajili ya
wagonjwa hao.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo Mkurugenzi huyo aliwataka watanzania kufahamu kuwa hadi sasa
hospitali hiyo ina mashine moja ambayo haiendani na idadi ya wagonjwa wanaofika
hospitalini hapo.
Ngoma alisema ili huduma hizo ziweze kuwa za
uhakika, hospitali hiyo inapaswa kuwa na mashine nane (8), ambapo kwa sasa ipo
mashine moja ambayo haikidhi.
“Unajua gharama za kununua mshine moja hadi kufungwa
inafikia gharama ya shil. Bilioni 2, fedha ambazo kwa sasa serikali haina uwezo
wa kuzipata mara moja”alisema Ngoma.
Ngoma alisema kutokana na uwepo wa mashine hiyo moja
kumesababisha wagonjwa zaidi ya 100 hadi 200 kulazimika kupatiwa huduma hiyo ya
mionzi kitendo ambacho hakilingani na matibabu hayo.
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kuna
wagonjwa 40000 wanaohitaji kupatiwa matibabu lakini hata hivyo kati ya hao ni
4000 pekee ndio wanaopati huduma hiyo.
Aliwataka Wanzania kutambua kuwa kuanguka kwa huduma
za matibabu ya saratani katika katika hospitali hiyo hakutokani na mtu bali
kunasababishwa na uwezo mdogo wa kifedha wa serikali.
Akizungumzia matatizo ya manesi ya kutishia
kuandamana kutokana na kutolipwa malipo ya saa za ziada za kazi, Mkurugenzi
huyo alisema hiyo ni moja ya haki yao ya msingi ili mradi wawe na sababu za
msingi.
Alisema kima inavyoeleweka kuwa hospitali hiyo haina
kibali cha kulipa malipo ya ziada ambapo hadi sasa hakuna Nesi anayefanya baada
ya masaa ya kawaida (overtime)
IDADI YA WANAWAKE WA WAFUGAJI WANAOGOMBEA NAFASI MBALIMBALI IMEONGEZEKA
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- MONDULI
Imeelezwa kuwa kwa sasa idadi ya wanawake kutoka jamii ya wafugaji ambao
wanajitokeza kuwania nafasi za uongozi mbalimbali katika jamii
imefikia asilimia 50 tofauti na hapo awali ambapo wanawake walikuwa na
mwitikio mdogo.
Hayo yameelezwa na Katibu wa umoja wa wanawake kupitia chama cha
mapinduzi(UWT) katika kata ya Engutoto, Bi Bihulda Kisaka wakati
aliopokuwa akiongea na Waandishi wa habari wilayani Monduli
Bi Kisaka alisema kuwa kilichofanya wanawake wengi wajitokeze hasa
katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho ni pamoja na uhamasishaji
ambao unafanywa na UWT wilaya ya monduli
Alifafanua kuwa kuongezeka kwa idadi ya wanawake hasa katika kata ya
Engutoto ni Motisha kubwa sana hasa kwa kata nyingine na jambo hilo
linatakiwa kuigwa na watu wengine
“Tuna idadi kubwa sana ya wanawake wa jamii ya wafugaji ambao
wanajitokeza katika kuomba nafasi mbalimbali tofauti na hapo awali
ambapo wengi walikuwa wanaogopa sana lakini sasa wengi wanajitokeza
sana”alisema Bi Kisaka
Pia aliongeza kuwa pamoja na kuwa wanawake wengi walikuwa wanajitokeza
hasa katika kata hiyo ya Engutoto bado wanawake wanakabiliwa na
changamoto lukuki hali ambayo inachangia hata baadhi yao kushindwa
kutumia demokrasia yao vema
Mbali na hayo alitaja changamoto nyingine ni pamoja na uhaba wa fedha
hali ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana washindwe kufikia
malengo yao mbalimbali hasa kwenye ulipaji wa ada
Awali aliwataka wanawake kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi zao vema
kwa kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
kwa kuwa wanahaki zao za msingi.

MWENYEKITI WA SARPCCO NA IGP SAID MWEMA KATIKA HAFLA YA KUAGANA
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema (kulia) na Mwenyekiti wa
Shirikisho la wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) ambaye
pia ni Kamishna wa Polisi wa Nchi ya Afrika Kusini Nhlanhala
Mkhwanazi wakiteta jambo wakati wa hafla fupi ya kumuaga baada ya
kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini. (Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi)
Mwenyekiti
wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Nhlanhala Mkhwanazi
(Kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema wakitoka
katika ukumbi wa Hoteli ya Kempiski baada ya kumalizika kwa hafla
fupi ya kumuaga Mwenyekiti huyo baada ya kumaliza ziara yake ya
kikazi ya siku mbili hapa nchini.Kulia ni Kamishna wa Operesheni
Paul Chagonja (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
Mwenyekiti
wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Nhlanhala Mkhwanazi
(Kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema
wakati wa hafla fupi ya kumuaga mwenyekiti huyo baada ya kumaliza
ziara yake ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.(Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi)
Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika lilivyorindima Uturuki
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto) akipokea
tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya
Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa
niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri
Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada
katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu
'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro
na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo
ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa
vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc akifungua mkutano wa Jukwaa la
Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na
wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri wa Habari wa gazeti la Nipashe Jumapili, Beatrice Bandawe(wa
pili kushoto) akifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika
na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita.
Mkurugenzi wa Raia Mwema aliyepata pia kuwa MhaririMtendaji wa gazeti
hilo na Kampuni ya New Habari Corporation 2006, John Bwire (kushoto) na
Mhariri wa Makala wa Habari Leo, Selemani Nzaro wakifuatilia mkutano wa
Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki,
ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka
nchi 54 za Afrika.
Profesa, Dk. Mohamed Bakari, raia wa Kenya anayefundisha Chuo Kikuu cha
Fatih nchini Uturuki, akipokea tuzo maalumu iliyotolewa kwa niaba ya
Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika
mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Afrika
ya Leo: Sera za Siasa, Uchumi na Mambo ya Nje' mjini Ankara, Uturuki
wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya
habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia wakati Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo
Leo, Willy Edward (mbele kwenye video) akiwasilisha mada katika mkutano
wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya
Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi'
mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi
ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari
na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akiwasilisha mada
katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu
'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro
na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo
ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa
vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
No comments:
Post a Comment