“CHAGGA DAY” yaikaribisha
Krismasi Uchagani
Katika kuzikaribisha sikukuu za Krismasi na mwaka mpya, tamasha
la kihistoria la siku ya wachaga kufanyika siku ya Jumamosi Tarehe 22-12-2012
katika viwanja vya Ushirika, Moshi Mjini, Kilimanjaro kuanzia saa 4:00 asubuhi
mpaka usiku.
Tamasha hili linalenga kuhamasisha
jamii ya kabila hilo na makabila mengine kuenzi mila na tamaduni. Vilevile,
kuhamasisha jamii na falimia zao zilizopo ndani na nje ya mikoa yao kukumbuka
nyumbani na kutembelea wazee mara kwa mara.
Tuna imani kubwa kuwa zaidi ya watu 3,000 na familia zao,
watahudhuria kwa wingi tamasha hili la kihistoria huku wakipata fursa ya:
Ø Kusikia historia ya wachagga
kwa kina toka kwa wazee wanatoka kwenye familia za wafalme na machief “MANGI
MKUU” wa kichaga waishio mkoani Kilimanjaro.
Ø Kuona na kucheza ngoma zote
za asili za kichaga pamoja na vikundi tofauti tofauti vya ngoma za asili na
sanaa za makabila mengine.
Ø Kula aina zote za vyakula
vya asili vya kichagga kama kiburu, kisusio, mtori, ndafu, shiro, kiumbo, kitawa,
macharari, ngararimo, ng’ande n.k
Ø Kunywa vinywaji vyote vya
asili vya kichagga kama mbege, dadii n.k
Ø Kupata burudani kutoka bendi
ya Akudo Impact, Msanii Costa Siboka kutoka Dar es Salaam na wasanii wote
kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Tumewaalika
viongozi wa serikali yetu, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje
ya mkoa wa Kilimanjaro, viongozi wa asasi zisizo za kiserikali pamoja na asasi
za serikali yetu, wakurugenzi wa makampuni ya utalii na hoteli kubwa za mikoa
ya Kilimanjaro na Arusha.
Tumejipanga
vizuri katika kufanikisha siku za makabila yote Tanzania kila mwaka tukianza na
makabila wa kaskazini, lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuenzi mila na
tamaduni za makabila yetu na kukumbuka kuzipeleka familia zetu nyumbani tuwapo
nje ya mikoa yetu.
Imedhaminiwa na;-
Safari Lager, Pepsi, Konyagi,
Precision Air, Radio 5 FM, Toyo, Samsung, Michuzi Blog Spot, Zizou Fashion,
Mlonge Bi Makai, Egesha Trading Agency, Delina Group Enterprises and Albert
Msando Legal Consultant.
Waandaaji: MyWay Entertainment Company.
Mkurugenzi Mkuu: Paul Siboka. Mganga
No comments:
Post a Comment