Picha ya pamoja
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amewataka wakulima wa zao la Tumbaku kufanya kazi kwa malengo ili kuboresha maisha yao na Watanzania ili kupata matokeo makubwa sasa(BRN).
Ameyasema hayo alipokuwa anafungua semina iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wakulima wa zao la Tumbaku katika Ukumbi wa Sapanjo unaomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ili kuleta tija kwa wakulima ambao wamekuwa na maisha duni.
Kinawiro ameitaka Benki ya NMB kutoa mikopo nafuu kwa wakulima wa Tumbaku na kukopesha Pembejeo kwa gharama nafuu ili vyama viweze kujikwamua kiuchumi kwa ajili ya kupata majawabu sahihi na Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Benki hiyo.
Aidha amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika na Benki kufanya kazi kwa uadilifu na kuacha kukwepa kutorosha Tumbaku na kupeleka mikoa mingine na nchi jirani kwa nia ya kukwepa madeni wanayodaiwa pia kufanya hivyo kunakosesha serikali mapato yake yanayotokana na ushuru.
Pia amewataka wakulima wa zao la Tumbaku kuweka pesa benki na kuhakikisha wanapanda miti ili kutunza mazingira na kupata nishati mbadala ili kuhifadhi mazingira ya Wilaya ya Chunya.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Chunya alitumia fursa hiyo kuiomba Benki ya NMB kusaidia mazao mengine kama ufuta ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa pato la wilaya hiyo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Meneja wa Kanda Sumka Mbuba amesema Benki ya NMB ina mkakati wa kuwa karibu na wakulima wa mazao mbalimbali na kuendesha semina mbalimbali zitakazowasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi kama siku za hivi karibuni walifanya semina ka hii kwa wakulima wa zao la Kahawa ilyojumuisha wilaya za Mbeya,Mbozi,Rungwe,Ileje na Mbeya.
Meneja wa NMB wilaya Chunya Musa Mumba alisema Benki yake ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wa zao la Tumbaku na kuwataka kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo kwa wakati ili iweze kusaidia wakulima wengine.
Na Mbeya yetu
Chunya
|
No comments:
Post a Comment