Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete,
Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa hotuba
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Usimamizi wa Uwekezaji wa
Miradi ya Umma Kanda ya Morogoro kwa Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na
Mipango. Waliokaa ni Bi. Anna Kimwela, Mchumi, Tume ya Mipango na Dr.
Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa
Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao
ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro
wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kikuu cha Kilimo Morogroro
(SUA).
Muwezeshaji Dr. Jehovaness Aikaeli,
Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa
elimu kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki
pamoja na wakufunzi wa mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi
ya Umma ambao ni Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Bi. Lorah
Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango
(aliyekaa wa pili kushoto) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment