Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent Shiyo (katikati) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya
kufungamanisha sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kitaifa na ile ya
kimataifa na kikanda iliyofanyika Septemba 22, 2016 katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere,
Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia
Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe na
kulia ni Bw. Maxwell Mkumba kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC).
Washiriki
wakiwa wanasikiliza hotuba ya ufunguzi kutoka kwa balozi Innocent Shiyo.
Washiriki
wakipata ufafanuzi wa malengo ya warsha hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia
Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe mara
baada ya ufunguzi.
Washiriki
wakisikiliza moja ya mada zilizotolewa katika warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment