TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, September 24, 2011

Rais Kikwete ang'ara katika ufunguzi wa mkutano wa DICOTA 2011 jijini Washington DC leo

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Watanzani nchini Marekani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Diaspora Council of Tanzania in America (DICOTA) 2011 huko Dulles, Virginia, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika (Picha na Mawasiliano Ikulu).
Wafadhili toka taasisi mbalimbali za umma na binafsi waliofanikisha DICOTA 2011 wakipozi na Rais Kikwete na Meza kuu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe akiongea kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete kuhutubi hadhira na kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011
Wageni waalikwa wakifurahia hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete wakati akifungua mkutano huo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na wageni mbalimbali katika mkutano huo.
Washiriki mbalimbali wa mkutano huo wakimsikiliza Rais Kikwete.
Rais Kikwete akiimbwa wimbo wa Taifa pamoja na meza kuu
Rais Kikwete akiwapongeza watoto kwa kuimba vyema
Sehemu ya waliohudhuria katika mkutano huo
Rais Kikwete akiwa katika banda la Mfuko wa Maendeleo wa Hassan Maajar Trust Fund
Hapa akiwa katika banda la benki ya CRDB
Ujumbe mzito toka NSSF ukiwa mkutanoni

MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA MAMA SALMA KIKWETE AKAGUA SHULE YA WAMA NAKAYAMA TARAYI KWA UZUNDUZI

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati akiongoza na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA iliopo Nyamisati Rufiji mkoa wa Pwani (kushoto) Twaha Twaha (mwenye tai) pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Suma Mensah (kulia) Sept.3.2011 kwaajili ya ukaguzi wa maandalizi kabla ya ufunguzi rasmi wa shule hiyo Sept.29.2011 utakaofanywa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Mohammed Shein . (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (mwenye miwani) pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA Mwalimu Msaidizi Suma Mensah iliopo Nyamisati Rufiji mkoa wa Pwani wakikagua mazingira ya shule Sept.23.2011 kabla ya ufunguzi rasmi wa shule hiyo Sept.24.2011 itakayofunguliwa rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt, Mohammed Shein. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Msanii mashuhuri na Mbunge wa Viti maalumu Vicky Kamata akiwa katika mazoezi ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya wasichana ya WAMA NAKAYAMA huko Nyamisati Mkoa wa Pwani kwaajili ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo Sept.24.2011 utakaofanywa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt, Mohammed Shein. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Wanafunzi na Mwalimu Mkuu Msaidizi Suma Mensah wakiwa katika kufanya usafi
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA huko Nyamisati Mkoa wa Pwani wakifanya mazoezi ya kimba wimbo maalumu Sept,23.2011 kwaajili ya uzinduzi rasmi wa Shule yao Sept.24.2011 utakaofanywa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar DDkt. Mohammed Shein. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Friday, September 23, 2011

TEITI KATIKA UKUMBI WA JB WAKIENDELEA NA MKUTANO MUDA HUU

Jengo la Benjamini Mkapa ambapo Mkutano wa TEITI unaendelea Muda huu.

Wadau katika dukuduku zao kwenye mkutano wa TEITI leo

 Mmoja wa Wadau wa TEIT akitoa ufafanuzi
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Peter Nyanje akitoa hoja

Uzinduzi wa Mpango wa Uwazi wa Uwajibikaji

Mwenyekiti wa TEITI Jaji Paul Bomani akizungumza wakati wa semina ya wadau wa Nishati na Madini, wakati akiwasilisha mchango wake kwa serikali kuitaka iunde Wizara ya Madini tofauti na Nishati, Dar es Salaam leo

 Mbaraka Igangula akichangia hoja wakati wa semina ya wadau wa Nishati na Madini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari wakimhoji Mwenyekiti wa TEITI Jaji Paul Boman Dar es Salaam leo
 Mwanyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika mapato ya madini, mafuta na gesi asilia Jaji Paul Bomani akizungumza wakati wa uzinduzi wa semina ya uwajibikaji Dar es Salaam Kushoto ni Mjumbe wa Bodi Dkt. Stephen Munga.
 Jaji Paul Bomani akisisitiza jambo kwa wakati wa semina hiyo, Dar es Salaam leo
 Jaji Paul Bomani akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu malipo madogo ya fidia kwa wananchi
Baadhi ya washiriki wa Semina wakimsikiliza kwa makini Jaji Paul Bomani wakati akizungumzia sekta ya Nishati na Madini.(Picha Zote na Shaaban Mpalule).

Jaji Bomani azindua mpango wa uhamasishaji sekta ya madini

 Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uzinduaji (TEITI), Jaji Paul Bomani akizungumza wakati akizindua semina ya siku moja, kuhusu tafiti na sheria ya madini Dar es Salaama jana.
 Mjumbe wa kamati tekelezi ya TEITI kupitia vyama vya Kijamii kwenye Upande wa Madhehebu ya Dini Askofu Dkt. Stivin Munga, akizungumza jambo kwenye Mkutano Unaoendelea kwenye Jengo la Benjamini Mkapa Posta Mpya.
Mwenyekiti wa TEITI  Jaji Paul Boman (kulia), na wajumbe wengine wa Bodi hiyo wakiendelea na Mkutano huo

TEITI YAFANYA MKUTANO BENJAMINI MKAPA.

MUDA HUU UNAENDELEA MKUTANO WA TEITI WORKSHOP ON LEGAL FRAMEWORK REVIEW FOR PREPARATION OF TANZANIA EXRACTIVE INDUSTRIES TRANSPARANCY INITIATIVE(TEITI) LEGISLATION

MKUTANO HUU UNAFANYIKA KWENYE UKUMBI WA JB BELMONT HOTEL KATIKA JENGO LA BENJAMINI MKAPA TOWER POSTA JIJINI DAR ES SALAA.

Muda mfupi nitakuletea Matukio ya Picha yanayoendelea katika mkutano huu

Wednesday, September 21, 2011

Baadhi ya Watendaji Mtaa na Kata kutoka wilaya za Kinondoni na Temeke mkoani Dar es salaam wakisikiliza kwa makini jana mjini Dar es salaam mafunzo ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi kwenye maeneo yao. Mafunzo hayo yanaendesha na Mradi wa Maboresho wa Sekta ya Sheria chini Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara(TLS).

Wakili kutoka Chama cha wanasheria Tanzania Bara(TLS) John Seka akiwafundisha watendaji wa Mitaa na Kata jana mjini Dar es salaam juu ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wenye shida mbalimbali na hawawezi kumudu gharama kuajiri wakili. Watendaji hao wanatoka wilaya za Temeke na Kinondoni.

Wakili kutoka Chama cha wanasheria Tanzania Bara(TLS) Steven Madulu akitoa somo kwa watendaji wa Mitaa na Kata jana mjini Dar es salaam juu ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wenye shida mbalimbali na hawawezi kumudu gharama kuajiri wakili. Watendaji hao wanatoka wilaya za Temeke na Kinondoni.
Mtendaji Mtaa Kiungani Kata  ya Kurasini Manispaa ya temeke Theophilda Christopher akitoa maoni yake jana jijini Dar es salaam wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo watendaji wa Mitaa na Kata juu ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi. . Mafunzo hayo yanaendesha na Mradi wa Maboresho wa Sekta ya Sheria chini Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara(TLS).(Picha Zote na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam)

UBALOZI WA MAREKANI WADHAMINI WASANII WALIOSHIRIKI TAMASHA LA MTEMI MILAMBO TABORA.

Msanii wa Muziki wa Asili Ally Mango(kulia), akifafanua jambo kuhusiana na Tamasha hilo 

Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga(Kushoto), akizungumzia Tamasha hilo.

Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.

Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango,Asha Kaombwe,Hamis Mpiga,Paulina Muhala,Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.

Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru

Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.

Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae.

Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John a.k.a Nice P.

Aksanteni kwa kunisikiliza.

Amon Mkoga
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions.
www.chiefpromotions.or.tz
0755 638 004/0655 638 004
Baadhi ya Wajumbe wa Kampuni hiyo, Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga, Mwanamuziki wa Asili Ally Mango, na wajumbe.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipiga Soga Muda mfupi Kabla ya Mkutano huo Kuanza

Hapa Wanahabari wakifuatlia kwa Makini Mazungumzo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions Amon Mkinga leo.