TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, May 16, 2012

WADAU WA MAWASILIANO WAPEWA FAIDA YA KUTUMIA KOMPYUTA NA UMUHIMU WA MFUMO WA DIGITAL

Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano  Sayansi na Teknolojia Dr Florens Turuka akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kuelekea kilele cha siku ya sherehe ya mawasiliano duniani ambapo maadhimisho hayo yanatarajiawa kufanyika kesho Duniani kote, Dk Turuka amewaomba wafanya biashara wauze televisheni ambazo zipo katika mfumo wa Digital. Warsha hiyo imeanza leo hii katika Ukumbi wa Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Prf, John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari  leo hii jijini Dar es Salaam kwenye Semina inayoambatana na Sherehe ya  siku ya mawasiliano Duniani. ambapo amewataka watanzania kuelewa umuhimu wa mawasiliano ya mtandao.
Baadhi ya wadau mblimbali wa mawasiliano nchini waliohudhuria kwenye warsha hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi  Mapinduzi Zuwena Muddy, akitoa mafunzo ya namna ya kutumia Computer  kwa wadau waliohudhuria kwenye semina hiyo.
Mwanafunzi Jackson Joseph kutoka shule ya Msingi  Mapinduzi jijini Dar es Salaam manispaa ya Ilala, akihojiwa na waandishi wa habari juu ya faida ya matumizi  ya Computer.
Mwanafunzi Zuwena Muddy akisisitiza jambo katika mafunzo hayo kwenye warsha hiyo.

RAIS DK SHEIN AFANYA UTEUZI ZANZIBAR

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohd Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Dkt Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (4) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais amemteuwa Mdungi Makame Mdungi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar.
 
Aidha Dkt. Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 61 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amemteuwa Khamis Jabir Makame kuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 16 Mei 2012,

Lowassa kuongoza harambee kuchangia elimu Kipawa

Na Dotto Mwaibale
 
WAZIRI Mkuu aliyejiuzuru ambaye ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa anarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya mpango wa kuboresha elimu Kata ya Kipawa Ilala Dar es Salaam.
Hayo yalibainishwa na Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema ameandaa chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuboresha elimu katika Kata yake ya Kipawa.
"Hafla hiyo itafanyika juni 6 mwaka huu katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Monduli Edward Lowassa"
Alisema hatua hiyo imefikiwa kufuatia juhudi zingine alizozifanya kwa ajili ya kata hiyo ambapo machi 17,2012 aliitisha matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Katika matembezi hayo mama Salma alichangia sh.milioni 3, Clouds Media Group milioni 1, wakati viongozi wa Serikali walioongozana naye walichangia sh.milioni 10 ambapo jumla yake ilikuwa sh. milioni 15.
Alisema aliguswa na jambo hilo baada ya kubaini changamoto nyingi hasa za elimu kwenye kata hiyo yenye jumla za shule za msingi 7 mbazo zinaupungufu wa madawati 5000, matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa na kutokuwa na maji.
Alisema jumla ya sh.bilioni moja zinahitajika ili kufanikisha mpango huo ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi, mashirika ya umma, Taasisi za dini, makampuni, viongozi mbalimbali na Asasi zisizoza kiserikali Ng'os kujitokeza kwenye harambee hiyo ili kufanikisha mpango huo.
Diwani Kaluwa aliwashukuru wote waliojitokeza kufanikisha matembezi ya awali na wale  wanaendelea kufanikisha maandalizi ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko huo.

Dk Shein afanya mazungumzo na Wizara ya Viwanda.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashra,Viwanda
na Masoko,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko
Ikulu Mjini Zanzibar leo.  [ Picha  na Ramadhan Othman,IKULU.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashra,Viwanda
na Masoko,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko
Ikulu Mjini Zanzibar leo.  [ Picha  na Ramadhan Othman,IKULU.]
ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na
Sheria,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu
Mjini Zanzibar leo.  [ Picha  na Ramadhan Othman,IKULU.]

WAFUGAJI NYUKI WAKUTANA NA WAZIRI MKUU PINDA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wafugaji wa nyuki kutoka Pemba na Rufiji waliomtembelea nyumbani kwake Dodoma kwa ziara ya kujifunza ufugaji nyuki iliyodhminiwa na  Mfuko wa  Maendeleo ya Jamii (TASAF), May 15,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa  katika picha ya pamoja na wafugaji nyuki kutoka Pemba na Rufiji waliotembelea shamba lake la nyuki ili kujifunza May 15, 2012. Kushoto kwake ni  Ladislaus Mamanga ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo  ya Jamii (TASAF) ambao ulidhamini safari hiyo na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa  Kusini Pemba , Juma  Kassim Tindwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NI WIKI YA TATU SASA SERENGETI YATANGAZA WENGINE WAWILI WABORESHEWA MAISHA

Meneja wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo katikati akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Mkaguzi kutoka bodi ya taifa ya bahati nasibu, Bw. Abdallah Hemedi kulia akikagua jinsi droo hiyo inavyochezeshwa. Kushoto ni meneja wa bia ya Serengeti Bw Allan Chonjo na katikati ni mwakilishi kutoka PWC Bw.Tumainieli Malisa.

Ni katika droo ya tatu ya promosheni ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL.
Wiki mbili zilizopita zilikuwa za aina yake baada ya kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kuendelea kukonga nyoyo za wateja wake na watanzania kwa ujumla kwa kuwapa zawadi washindi wa promosheni inayoendelea inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya kizibo’ ambapo watanzania wengi wameshuhudia kampuni hiyo ikiwakabidhi washindi wa promosheni hiyo zawadi zao katika promosheni hii kubwa.
Amadeus Minja na Agness Msengi wakazi wa Dar es salaam, walijishindia jenereta (kangavuke) kubwa ambapo walikabidhiwa zawadi hizo mwisho mwa wiki iliyopita. Ibrahim Kimambo mkazi wa tabata jijini Dar es salaam alibahatika kujinyakulia pikipiki mpya na ya kisasa ambapo naye alikabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi unaovuma sana ujulikanao kama Dar LIVE pale Mbagala Zakhem.
Bw. Ibrahim ambaye hakuwa na kazi yoyote mpaka bahati iliyobebwa na promosheni hii ilipomdondokea  alikuwa na haya ya kusema, “kwa kweli nilipopata taarifa ya kushinda zawadi ya pikipiki sikuamini lakini sasa nimeamini na nawashukuru sana SBL kwa kuwa sasa naweza kujiajiri na kuendeleza maisha yangu na wale wanaonitegemea”. Kutoka jijini Mwanza Godfrey Shao ambaye alijinyakulia bajaj ya gurudumu tatu anaendelea kusubiri taratibu za usajili zikamilike ili aweze kukabidhiwa bajaj yake.
Asubuhi ya leo droo ya tatu katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini.
Droo hiyo ya tatu kama ilivyo kawaida katika droo zilizopita, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers kuhakikisha washindi wote watapatikana kihalali.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ Na kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake.
Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya SBL Bi. Teddy Mapunda, amesema kwamba “mpaka sasa tumeshawapata washindi wawili wa jenereta ambao tayari tumewakabidhi zawadi zao, wengine ni washindi wa bajaj moja na wa pikipiki moja ambao nao wameshakabidhiwa zawadi zao”
“Tunawashauri wateja wetu na watanzania wote wenye sifa za kushiriki katika promosheni hii  ya aina yake waendelee kushiriki bila kukata tamaa na hatimaye nao waweze kushinda kwani promosheni yetu ni ya kweli na ya uhakika.” alisema Mapunda na kuongeza kuwa mpaka sasa tayari watu zaidi ya 2000 wamejishindia pesa taslimu na wakafanikiwa kupata pesa hizo kwa urahisi kabisa kupitia mtandao wa kutuma na kupokea pesa wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom MPESA ndani ya masaa ishirini na nne. Pia, washindi wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika promosheni hiyo.
Washindi wetu katika droo ya tatu ni Fadhili Manzi mkazi wa Mafinga mywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager nambaye amejishindia bajaj na Raymond Denis mkazi wa Iringa ambaye  amejinyakulia jenereta kupitia bia ya Tusker Lager.
MAELEKEZO:
Nunua bia ya Serengeti lager, Tusker lager au Pilsner Lager fungua kisha angalia chini ya kizibo utapata namba zilizopo chini ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako, nakili namba zilizochanganyika na herufi  mfano AB55550, kisha tuma kwenda namba 15317 na unaweza kujishindia pesa taslimu kati ya shilingi 10,000, 50,000 au 100,000 au unaweza kujipatia bia ya bure kati ya bia zilizoainishwa katika promosheni hii . Fanya hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti.  Wanaoruhusiwa kushiriki promosheni hii ni walio  na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea.

NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MKOA WA MTWARA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali (Mst) Joseph Simbakalia akisalimiana na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo huku wakishuhudiwa na Meneja wa Mahusiano Bi. Shy-Rose Bhanji wakati wa kukabidhiwa msaada wa Madawati kwa Shule za Mkoa wa Mtwara.
(Picha zote na Beatha Hyera, Afisa Habari Mtwara)
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Joseph Simbakalia (wa kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo wakati wa kukabidhiwa msaada huo utakozinufaisha Shule za Msingi katika Wilaya za Masasi na Newala.
 Meneja wa Mahusiano Benki ya NMB Bi. Shy-Rose Bhanji akitoa maelezo kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuhusiana na msaada huo na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Benki ya NMB na wananchi kwa ujumla katika kuhakikisha maendeleo ya elimu katika nchi yetu.

WADAU KATIKA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI JIJINI BORN

Baadhi ya washiriki Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, wakiiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Kimataifa wa sayansi na taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi Mjini Bonn Ujerumani (na Evelyn Mkokoi)

Rais Kikwete atembelea Ofisi za Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alitembelea ofisi za Tume ya kukusanya na kuratibu maoni juu ya katiba zilizopo katika jengo jipya katika Wizara ya Mambo ndani jijini Dar es Salaam.Akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo Rais Kikwete alirudia ahadi yake ya kuwapatia nyenzo za kazi ikiwemo usafiri ili kuiwezesha tume hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.Pichani Rais akizungumza na wajumbe wa tume hiyo katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la tume hiyo jana.
Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu maoni juu ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba(kulia) akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipomtembelea ofisi kwake jana.Wengine katika picha ni Makamu mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mkuu Mstaafu Mhe. Agostino Ramadhani(Watatu kushoto),Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Mathias Chikawe(Wapili kushoto) na kushoto ni naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Angela Kairuki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo naProfesa Mwesiga Baregu ambaye ni mjumbe  wa Tume ya kuratibu maoni kuhusu katiba wakati Rais alipotembelea ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam jana(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Wanne kushoto Mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya kuratibu maoni  ya Katiba wakati alipotembelea ofisi za tume hiyo Jijini Dar Es Salaam jana.

President Donald Kaberuka Invited To The 38th G8 Summit And To The White House By President Obama



 
At the invitation of the President of the United States, the President of the African Development Bank will be attending the Group of Eight (G8) meeting
WASHINGTON, May 16, 2012/ -- At the invitation of the President of the United States, Barack Obama, the President of the African Development Bank, Donald Kaberuka, will be attending the Group of Eight (G8) meeting at Camp David in Frederick County, Maryland on 18 and 19 May.
The discussions will centre on the subject of food security in Africa and will also show how Africa's voice is being heard at the highest level.
Donald Kaberuka will also be attending a special luncheon at the White House during his time in the United States.

WAZIRI WA ZAMANI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII DKT. MPONDA AKABIDHI RASMI OFISI

 Waziri wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi kitabu cha sheria na mwongozo wa utendaji kazi wa wizara hiyo Waziri Mpya  Dkt. Hussein Mwinyi.Makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye ukumbi wa wizara hiyo
Mawaziri hao wakipeana mkono mara baada ya makabidhiano hayo Dkt. Mponda amemtaka waziri Dkt. Mwinyi kufuatilia na kusimamia vyema  utekelezaji wa  mikakati ya sekta ya afya ili kuweza kuimarisha huduma ya afya kwa wananchi
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi aliyekaa katikati,Kulia ni waziri wa zamani Dkt. Hadji Mponda na Naibu Waziri Mpya Dkt. Seif Rashid aliyekaa kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara hiyo mara baada ya makabidhiano ya ofisi.

Ashindwa kujiunga na Sekondari Handeni kwa kukosa ada

Mwenjuma M. Magalu (kulia) akiwa na Bibi yake nyumbani kwao Kijiji cha Msasa, wilayani Handeni
LICHA ya Serikali kuliarifu Bunge la Tanzania kuwa wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba mwaka 2011 kutoka mikoa 12 tayari wamejiunga na kidato cha kwanza, imebainika bado kuna wanafunzi wameshindwa kujiunga na shule kutokana na kipato duni cha familia zao.
Mwenjuma M. Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni ni miongoni mwa wanafunzi walioshindwa kujiunga na sekondari kutokana na mama yake kushindwa kumgharamia mahitaji ya shule.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni kijijini Msasa, wilayani Handeni, katika utafiti uliofanyika kwa ushirikiano na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), mama wa mtoto huyo Hadija Magalu aliyetelekezwa na mumewe kwa muda mrefu alisema ameshindwa kumsomesha mwanaye kutokana na kipato duni alichonacho.
Magalu alisema alipata taarifa za kufaulu kwa mwanae tangu Desemba 12, 2011 na kuanza kujikusanya taratibu lakini hadi muda wa kwenda shule ulipofika (Januari 9, 2012) alikuwa hajakamilisha baadhi ya vifaa vinavyohitajika shuleni vikiwemo fedha ya ada na michango mingine.
“Naweza kukuonesha hata baadhi ya vitu ambayo nilikuwa tayari nimenunua kama sare, kwanja na mahitaji mengine madogo madogo…aliyenikwamisha na kunivunja moyo ni babayake (baba wa mtoto), ambaye awali niliwasiliana naye kupitia kwa ndugu zake na kuahidi angenisaidia ada lakini hakufanya hivyo hadi muda wa kwenda shule ulipofika,” alisema Magalu.
Mume wa Magalu (jina tunalo) ametelekeza familia yake (watoto wanne) pamoja na mkewe kwa zaidi ya miaka minne sasa kwa kisingizio kwamba amekwenda nje ya Wilaya ya Handeni kutafuta maisha, huku mkewe akibaki akiangaikia familia hiyo.
“Tumekuwa tukisikia tu kwamba ameonekana kijiji fulani lakini ukifuatilia humpati, na mara nyingi anapowasiliana na ndugu zake ndio wanatupa taarifa zake…nami niliwasiliana naye mara ya mwisho nikimpata taarifa za mtoto kufaulu lakini hakutekeleza ahadi yoyote juu ya kunisaidia ada ya mtoto.
Michango iliyomkwamisha mwanafunzi Mwenjuma Magalu kujiunga na kidato cha kwanza ni ada ya sh. 20,000, fedha ya taaluma sh. 10,000, fedha ya madawati 15,000, fedha ya sweta sh.10,000, kitambulisho sh. 5,000, ulinzi sh. 5,000, tahadhari 5,000 pamoja na fedha kwa ajili ya nembo ya shule sh. 2,000.
Akihutubia Mkutano wa Saba wa Bunge la Tanzania lililomalizika hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kutoka mikoa 12 ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mara, Morogoro, Mwanza, Lindi, Kilimanjaro, Pwani, Ruvuma  na  Tanga, wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba wamefanikiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza.
Hata hivyo mwanafunzi Magalu kwa sasa anafanya vibarua kwa moja ya kampuni za Kichina zinazofanya ujenzi wa barabara inayopita Kijiji cha Msasa, kwa madai anatafuta fedha za ada na endapo akikamilisha atahakikisha anaendelea na elimu ya sekondari hapo baadae.
Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuzungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, Hassan Mwachibuzi alisema ofisi yake haina taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na shule, hivyo kumshauri mwandishi amueleze mtoto huyo kufika ofisi za halmashauri ili aweze kujieleza na ikiwezekana kusaidiwa.
“Kama huyo mtoto yupo mwelekeze aje pale ofisini kuna wataalamu wa utambuzi watamuhoji na kuangalia namna ya kumsaidia…sisi hatuna taarifa hizo na huenda wahusika wanatuficha,” alisema kiongozi huyo.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA

MVUA KUBWA ZILIZONYESHA MJINI BUKOBA ZASABABISHA MAJI KUJAA MITAANI

Nyumba ya mdau Bi Nesi wa Uswahili kwa mama Rujaka ikiwa imezingirwa na maji kutokana na mvua kubwa inayonyesha kwa mfurulizo mjini Bukoba mkoani Kagera kama itaendelea kunyesha huenda maafa makubwa yakatokea.
(PCHA KWA HISANI YA BUKOBAWADAU)
Nyingine ni makazi ya watu Eneo la Omukigusha na HAMUGEMBE kando kando ya mto kanoni.
hali iko hivyo maeneo ya Kashai matopeni, Kasalani, na Jamhuri  pamoja na maeneo ya Desare Pub na Hotel ya VICTORIUS.
Mwanafunzi akitoka shule akipita kwenye madimbwi ya maji yaliyotokana na mbua hiyo.
Mkazi wa mjini Bukoba akipita kwenye madibwi ya maji yaliyojaa katika mtaa mbalimbali mjini humo.
Maji yakiwa yamezingira vibanda mbalimbali vya biashara kama vinavyoonekana vikiwa vimezingirwa na maji.

NHIF na kuwaenzi wazee kwa matibabu

Na Mwandishi Wetu

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umevishauri vituo vinavyotoa huduma kwa wanachama wake ambavyo vimetenga maeneo maalum, kuhakisha vinatoa huduma hiyo kwa wazee katika maeneo hayo ili kuwaepusha na usumbufu wakati wa kupata huduma za matibabu.

Rai hiyo imekuwa ikitolewa kwa nyakati tofauti na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Emanuel Humba wakati wa kutembelea hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizosajiriwa na Mfuko huo kwa lengo la kujionea huduma zinazotolewa kwa wanachama wake.

"Lazima tuwaenzi wazee wetu, wamefanya kazi kubwa ya kuifikisha nchi hii hapa ilipo hivyo kama Mfuko tungependa kuona mahali wanapotibiwa wanachama wetu na wazee wetu nao wapate huduma mahali hapo...si vyema kuona wakitaabika wakati wa kupata matibabu," alisema Humba.

Aliwataka watoa huduma kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali zinazotolewa na NHIF kuboresha huduma za matibabu kwa kuwa na vifaa vya kisasa, dawa na kuboresha mazingira ya vituo hivyo.

"Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa fursa ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ambao unalenga moja kwa moja kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla hivyo ni vyema wazee wetu nao wakapewa heshima kubwa wakati wa kupata matibabu,"alisema Humba.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ameushauri Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ya afya kwa wananchi ili kupunguza gharama za matibabu.

Amesema elimu ya afya itasaidia wanachama na wananchi kwa ujumla kuepukana na maradhi ambayo yanagharimu fedha nyingi kwa ajili ya matibabu.

"Yapo maradhi yanayotokana na mtindo wa maisha kama kisukari, shinikizo la damu ambayo yanaweza kuepukika kwa wanachama wenu kupata elimu tu ya namna ya kula, kufanya mazoezi na mambo mengine,"alisema Manyanya.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, hivi karibuni umeendesha mikutano ya wadau wake katika mikoa mbalimbali nchini,ambayo kwa pamoja wameazimia kuifanya agenda ya Bima ya Afya kuwa ya kudumu.

JK KATIKA SEMINA YA APRM MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimwagiza jambo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wa Utawala bora, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, iliyofanyika leo May 15, 2012, kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Semina hiyo iliandaliwa na Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa vigezo vya Utawala Bora-APRM. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama. (Picha na Bashir Nkoromo)

Washindi wa Kili Talent search wafikia 12

Washindi kutoka Dodoma kutoka kushoto ni Halima Ramadhani, Juma Madaraka na Issa Dubat
Kutoka kushoto ni Proffesor Jay, Henry Mdimu, Queen Darleen na Juma Nature.
 
Na Mwandishi Wetu
Washindi wa msako wavipaji unaodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, wiki hii umefikia hatua ya nne ambapo umefanikisha kupata washindi 12 ambao wamepata nafasi ya kurekodi nyimbo zao tayari kwa kuanza safari yao ya kisanii kupitia muziki.
Kwa mujibu wa waratibu wa zoezi hilo kampuni ya Frontline Novelli, tayari usaili umeshapita katika jumla ya mikoa minne na kila mkoa walikuwa wakichukuliwa washindi watatu watatu.
Akiifafanua zaidi kuhusiana na mchakato huo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Frontline, Irene Kiwia alisema washindi hawa watatu wa kila mkoa mara wanapopatikana hupewa nafasi ya kurekodi wimbo, kila mmoja na kisha kufanya wimbo wa pamoja wakishirikiana wote watatu.
Baada ya kurekodi washindi hawa watatu wote wanashiriki katika tamasha la washindi la mkoa huo ambapo kati yao mmoja atakayefanya vema jukwaani ndio anapata nafasi ya kushiriki tamasha kubwa la washindi litakalofanyi9ka mapema mwisho wa mwezi huu jijini dar es salaam.
Mikoa ambayo imeshatembelewa mpaka sasa ni Dodoma, Mwanza, Moshi na Mbeya ambapo washindi wake tayari wamesharekodi na katika mikoa ya Dodoma, Moshi na Mwanza, washiriki wa tamasha kubwa kabisa litakalofanyika mkoani Dar es salaam wameshapatikana.

SAID BONGE WA CLOUDS APANDA MIGOMBA KATIKA BARABARA YA MWANANYAMALA BAADA YA MANISPAA YA KIONONDONI KUITELEKEZA

Mfanyakazi wa Radio Clauds FM, Said Mohamed 'Said Bonge' akipanda migomba kwenye mashimo ya barabara ya Mwananyamala Hospitali Dar es Salaam leo huku gari likipiata kando yake. Bonge alisema amechukua uwamuzi huo baada ya wahusika kushindwa kuyafukia mashimo hayo ambayo yamekuwa yakileta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Said Bonge akiendelea na shughuli ya kupanda migomba katika barabara ya Mwananyamala ambayo imeharibika vibaya huku wahusika wakiifumbia macho bila kuchukua hatua zozote za kuikarabati.

MASHINE CHACHE ZA MIONZI ZACHANGIA KUSHUKA KWA HUDUMA ZA MATIBABU YA KANSA OCEAN ROAD

NA MWANDISHI WETU
 
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Saratani Ocean Road, Twalibu Ngoma amekiri kuwa kuanguka kwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo, kumechangiwa na   uwezo mdogo wa serikali wa kununua mashine za mionzi  kwa ajili ya wagonjwa hao.
 
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi huyo aliwataka watanzania kufahamu kuwa hadi sasa hospitali hiyo ina mashine moja ambayo haiendani na idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.
 
Ngoma alisema ili huduma hizo ziweze kuwa za uhakika, hospitali hiyo inapaswa kuwa na mashine nane (8), ambapo kwa sasa ipo mashine moja ambayo haikidhi.
 
“Unajua gharama za kununua mshine moja hadi kufungwa inafikia gharama ya shil. Bilioni 2, fedha ambazo kwa sasa serikali haina uwezo wa kuzipata mara moja”alisema Ngoma.
 
Ngoma alisema kutokana na uwepo wa mashine hiyo moja kumesababisha wagonjwa zaidi ya 100 hadi 200 kulazimika kupatiwa huduma hiyo ya mionzi kitendo ambacho hakilingani na matibabu hayo.
 
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka kuna wagonjwa 40000 wanaohitaji kupatiwa matibabu lakini hata hivyo kati ya hao ni 4000 pekee ndio wanaopati huduma hiyo.
 
Aliwataka Wanzania kutambua kuwa kuanguka kwa huduma za matibabu ya saratani katika katika hospitali hiyo hakutokani na mtu bali kunasababishwa na uwezo mdogo wa kifedha wa serikali.
 
Akizungumzia matatizo ya manesi ya kutishia kuandamana kutokana na kutolipwa malipo ya saa za ziada za kazi, Mkurugenzi huyo alisema hiyo ni moja ya haki yao ya msingi ili mradi wawe na sababu za msingi.
 
Alisema kima inavyoeleweka kuwa hospitali hiyo haina kibali cha kulipa malipo ya ziada ambapo hadi sasa hakuna Nesi anayefanya baada ya masaa ya kawaida (overtime)

IDADI YA WANAWAKE WA WAFUGAJI WANAOGOMBEA NAFASI MBALIMBALI IMEONGEZEKA

NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- MONDULI

Imeelezwa kuwa kwa sasa idadi ya wanawake kutoka jamii ya wafugaji ambao
wanajitokeza kuwania nafasi za uongozi mbalimbali katika jamii
imefikia asilimia 50 tofauti na hapo awali ambapo wanawake walikuwa na
mwitikio mdogo.

Hayo yameelezwa na Katibu wa umoja wa wanawake kupitia chama cha
mapinduzi(UWT) katika kata ya Engutoto, Bi Bihulda Kisaka wakati
aliopokuwa akiongea na Waandishi wa habari wilayani Monduli

Bi Kisaka alisema kuwa kilichofanya wanawake wengi wajitokeze hasa
katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho ni pamoja na uhamasishaji
ambao unafanywa na UWT wilaya ya monduli

Alifafanua kuwa kuongezeka kwa idadi ya wanawake hasa katika kata ya
Engutoto ni Motisha kubwa sana hasa kwa kata nyingine na jambo hilo
linatakiwa kuigwa na watu wengine

“Tuna idadi kubwa sana ya wanawake wa jamii ya wafugaji ambao
wanajitokeza katika kuomba nafasi mbalimbali tofauti na hapo awali
ambapo wengi walikuwa wanaogopa sana lakini sasa wengi wanajitokeza
sana”alisema Bi Kisaka

Pia aliongeza kuwa pamoja na kuwa wanawake wengi walikuwa wanajitokeza
hasa katika kata hiyo ya Engutoto bado  wanawake wanakabiliwa na
changamoto lukuki hali ambayo inachangia hata baadhi yao kushindwa
kutumia demokrasia yao vema

Mbali na hayo alitaja changamoto nyingine ni pamoja na uhaba wa fedha
hali ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana washindwe kufikia
malengo yao mbalimbali hasa kwenye ulipaji wa ada

Awali aliwataka wanawake kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi zao vema
kwa kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
kwa kuwa wanahaki zao za msingi.

MWENYEKITI WA SARPCCO NA IGP SAID MWEMA KATIKA HAFLA YA KUAGANA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema (kulia) na Mwenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) ambaye pia ni Kamishna wa Polisi wa Nchi ya Afrika Kusini Nhlanhala Mkhwanazi wakiteta jambo wakati wa hafla fupi ya kumuaga baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Mwenyekiti wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Nhlanhala Mkhwanazi (Kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema wakitoka katika ukumbi wa Hoteli ya Kempiski baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kumuaga Mwenyekiti huyo baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.Kulia ni Kamishna wa Operesheni Paul Chagonja (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
Mwenyekiti wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Nhlanhala Mkhwanazi (Kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema wakati wa hafla fupi ya kumuaga mwenyekiti huyo baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika lilivyorindima Uturuki

Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc akifungua mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri wa Habari wa gazeti la Nipashe Jumapili, Beatrice Bandawe(wa pili kushoto) akifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita.
Mkurugenzi wa Raia Mwema aliyepata pia kuwa MhaririMtendaji wa gazeti hilo na Kampuni ya New Habari Corporation 2006, John Bwire (kushoto) na Mhariri wa Makala wa Habari Leo, Selemani Nzaro wakifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Profesa, Dk. Mohamed Bakari, raia wa Kenya anayefundisha Chuo Kikuu cha Fatih nchini Uturuki, akipokea tuzo maalumu iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Afrika ya Leo: Sera za Siasa, Uchumi na Mambo ya Nje' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia wakati Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (mbele kwenye video) akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.

Tuesday, May 15, 2012

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Linapozungumza



 
 
ASPIRE KUANZA KUSAKA VIPAJI MEI 21
Mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika kuanzia Mei 21 mwaka huu.
Vituo vitakavyohusika ambavyo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto wasiopungua 176 na tarahe ya kufanyika mchakato huo kwenye mabano chini mng’amua vipaji (scout) kutoka Hispania ni Morogoro (Mei 21 mwaka huu saa 3 asubuhi) na Bagamoyo mkoani Pwani (Mei 21 mwaka huu saa 8 mchana).
Vingine ni Kawe, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 3 asubuhi), Makongo, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 8 mchana) na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam (Mei 26 mwaka huu saa 9 mchana).
 
Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani kwa Tanzania una jumla ya vituo 14. Vituo vingine ni Kigamboni, Tandika, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni na Tabata.
 
Watoto watakaochaguliwa katika mchakato huo watakwenda katika mchakato mwingine kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Nairobi, Kenya.
 
Watakaofuzu kutoka hapo ndiyo watakaokwenda kwenye vituo vya kuendeleza vipaji (centre of excellence) vya Aspire Football Dreams. Aspire ina vituo viwili vya kuendeleza vipaji ambavyo viko Doha, Qatar na Dakar, Senegal.
 
TWIGA STARS KUJIPIMA KWA BANYANA BANYANA
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) itakayofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Happy Mothers Day - Tumsaidie Mama Yetu Mpendwa

 
Ni siku moja tu imepita tangu tusherehekee siku ya akina mama Duniani.
Lakini si kila mwanamke anapata bahati ya kushereheka sikukuu kama hii ilihali wengine tukimshukuru Mungu kwa siku hii muhimu.
Mimi na Tanzania ilimhoji Mama yetu Mpendwa Christophina ambaye amekuwa akiteseka na maumivu ya mguu kwa muda mrefu. Hadi sasa amekwishapata mchango wa shillingi 710,000/= na anahitaji jumla ya shilingi 1,200,000/= kwa ajili ya operesheni. Hivyo amepungukiwa shillingi 490,000/=. Shime watanzania!
Anahitaji msaada wa matibabu. Hebu tumsikie na tumsaidie.
Namba za simu na account zilizotolewa hapo ni za kwake mwenyewe kama kuna mtu atapenda kuwasiliana naye.
Hoyce Temu – A.k.a Mama Ruby
Mtangazaji – Mimi na Tanzania
Happy Mothers Day!

Exim Bank FC beats Stanbic FC in bankers’ soccer bonanza

Exim Bank Football Club (Exim FC) in a group photo shortly before the kickoff of their friendly match against Stanbic Bank team played yesterday at Karume grounds in Dar es Salaam. Exim beat Stanbic 3-2. Picture by our photographer.
By Staff Reporter

Exim Bank Tanzania FC beat Stanbic Bank FC 3-2 during a bankers’ soccer bonanza held at Karume Stadium in Dar es Salaam yesterday.
The Stanbic Bank FC looked superior in the first half emerging beating Exim Bank 2-1 during the first 45 minutes with Exim getting a consolation goal through Abass Digole that was scored in the 13th minute
Exim FC however made a coma back in the second half scoring an equalizer in the 64th minute through their striker Nobert Misana.
The bank’s equalizer created enthusiasm and moral for the team that consequently saw Exim bank score its third goal through Norbert Missana in the 82nd minute with Exim bank emerging winners after the final whistle.
Speaking shortly after the final whistle of the game, Norbert Missana who emerged as the game’s hero said the match was rather difficult as compared to their last match with Diamond Trust Bank.
 “Sincerely, we did not believe we would emerge victorious due to our poor performance in the first half.
“We managed to work upon our mistakes in the second half working as a team that saw us score an equalizer and a third goal (winner) in the second half. Am grateful that we managed to utilize the chances that have been generated in the second half,” he added.
The match was geared towards testing employees’ fitness in sports since sports activities play an important part in people’s lives especially after a hard day’s work.

Ufunguzi wa mkutano wa sayansi na mabadiliko ya tabia nchi mjini Bonn

Bi. Christiana Figeres, Executive Secretary wa  United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) akifungua mkutano  wa kimataifa wa sayansi na taaluma wa mabadiliko ya tabia nchi, Mjini Bonn Ujerumani. (Picha na Evelyn Mkokoi Bonn)

WATU 120 WAFANIKIWA KUJENGEWA UWEZO SPRINGS OF HOPE TANZANIA

Shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kwa jina la Springs of
Hope –Tanzania lenye makao yake makuu Mjini Arusha  limefanikiwa
kuelimisha jumla ya watu 120 waishio kwenye mazingira magumu ikiwa ni
pamoja na kuwajengea uwezo jinsi ya kuweza kuanzisha miradi
midogomidogo ili kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha  waliyo nayo.

Kutolewa kwa elimu hiyo kunafanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoani
hapa, huku wakilenga zaidi jamii iishiyo katika mazingira magumu
kutokana na kuwa  wengi wao wakishindwa kuwasomesha watoto wao
kutokana na ugumu wa maisha walio nao hivyo kuwaozesha ili kupunguza
gharama .

Akizungumza na Fullshangweblog, Kiongozi wa vikundi  hivyo kutoka  shirika
hilo ,Linus Hokororo  alisema kuwa mbali na kutoa elimu hiyo wameweza
kuwaelimisha kuunda vikundi vya watu 30 kwa lengo la kuweza
kukopeshana mikopo midogomidogo  pamoja na kuwawezesha wao kuunda
mfuko wa jamii  utakaowawezesha wao binafsi kujitatulia changamoto
mbalimbali za maisha , ikiwa ni pamoja na  kuwasaidia wao kuanzisha
saccos yao wenyewe bila kusaidiwa na mtu yeyote.

Alisema kuwa, baada ya elimu hiyo tayari jumla ya vikundi vinne vyenye
idadi ya watu 120 vimekwisha undwa huku wakiweza kuchangishana fedha
na kuanzisha miradi midogomidogo pamoja na kuweza kujiwekea akiba yao
 kwa ajili  ya kuwasomesha watoto wao ambao wengi wao wamekuwa
wakibakia majumbani tu kutokana na ukosefu wa ada.

‘Sisi tulifikia uamuzi wa kufanya hivi baada ya kuona kuwa, jamii
nyingi zimekuwa zikipata magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi kutokana
na kuwepo kwa umaskini, hali inayowapelekea kuingia kwenye vishawishi
mbalimbali, hivyo kwa kufanya hivi elimu hii imewawezesha kuwatoa
kwenye mazingira magumu na kuweza kujiinua kuichumi kwa
ujumla.’alisema  .

Aliongeza kuwa, katika kufanikisha shughuli zao wamekuwa wakiwezeshwa
na wahisani mbalimbali ikiwa ni pamoja na  East Africa Adventure
Safari company ambao waliwapatia masaada wa kiasi cha USD 360 kwa
ajili ya kutoa elimu hiyo kwa jamii itokayo kwenye mazingira magumu.

Aidha alisema kuwa , elimu hiyo imewafikia watu waishio mazingira
magumu kutoka kata ya Bwawani, Oldonyosambu, Muriet  , kata ya Suye ,
Tengeru, Kimandolu na Sanawari.

Hokororo alisema kuwa, watu hao wametokea halmashauri ya Arusha
vijijini, halmashauri ya Meru na manispaa ya Arusha huku wakiendelea
kuongeza maeneo zaidi kulingana na watakavyoendelea kufanya uchunguzi
na kubaini maeneo yenye uhitaji huo.

TANZANIA YAWA TISHIO INDABA


Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa (watatu kushoto) pamoja na Kurugenzi Mwendeshaji Biashara na viwanda wa Afrika Kusini Bibi Elizabeth Thabethe  (wa kwanza kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya waoneshaji kutoka Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki (wan ne kushoto) alipotembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya INDABA mjini Durban Afrika Kusini.
Na: Geofrey Tengeneza, Durban. 
 
Banda la Tanzania katika maonyesho ya Utalii ya Kimataifa ya INDABA yanayoendelea jijini Durban Afrika Kusini limeendelea kuvutia viongozi na watu wa kada mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini wanaotembelea maonyesho hayo.  Miongoni mwa waliotembelea banda hilo shindwa kuzuia hisia zao hususan kwa maelezo na vielelezo vinavyoonesha uzuri na upekee wa vivutio vya utalii vya Tanzania na shughuli za utalii zinavyoendeshwa nchini ni Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Viwanda na Biashara la Afrika Kusini Bibi Elizabeth Thabethe  ambao kwa pamoja walitembelea Banda la Tanzania na kujionea vielelezo mbalimbali sambamba na kupata maelezo yaliyowafurahisha sana kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk Aloyce Nzuki na waoneshaji wa Tanzania kwa ujumla Naibu huyo waziri alifurahishwa na kuvutiwa na jinsi Tanzania kupitia Bodi ya Utalii ilivyojipanga katika kuitangaza Tanzania duniani  na jinsi ambavyo Tanzania imekuwa ni mshiriki mzuri wa maonesho ya INDABA na kukiri kuwa Tanzania imekuwa ikitoa changamoto kubwa kwa nchi nyingine wanachama wa SADC katika sekta ya Utalii. “Tanzania ni nchi tishio katika sekta ya utalii miongoni mwa nchi za SADC, ni nchi inayonivutia sana “ alisema Bibi Tokozile Xasa
Jumla ya makampuni 49 kutoka sekta binafsi na taasisi sita za serikali zinashiriki katika maonesho hayo ambayo ni makubwa kuliko yote barani Afrika. Maonesho haya hufanyika kila mwaka jijini Durban Afrika Kusini. Katika maonesho kama haya mwaka jana Banda laTanzania lilitunukiwa tuzo ya kuwa Banda Bora kuliko yote katika maonesho hayo miongoni mwa nchi za SADC.

Rais Kikwete afungua semina ya APRM kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma leo asubuhi

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua semina ya Africa Peer Review Mechanism(APRM) kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya  CCM taifa katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo
Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa wakihudhuria semina maalumu ya APRM iliyofanyika katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo asubuhi(Picha na Freddy Maro)

VIJANA WATAKIWA KUZINGATIA ELIMU ILI KUZIKOMBOA NCHI ZAO KATIKA UTEGEMEZI


Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni  ubalozi wa Iran, Morteza Sabouri, akifafanua jambo.
 
NA MWANDISHI WETU
VIJANA nchini wametakiwa kutambua kuwa chanzo cha mabadiliko ya kweli katika kila nchi duniani huanzia kwao, hivyo ni vema wakazingatia elimu ili kuzikomboa nchi zao kutoka katika utegemezi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislam  ya Watu wa Iran wakati akimkaribisha Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Teheran, Kitivo cha Hadith na Sayansi, Atefeh Noor katika mkutano wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala jijini Dar es Salaam leo.
Alisema vijana ndio nguzo ya taifa, hivyo wanapo pata nafasi ya mafunzo katika Vyuo wasikubali kupoteza muda kwani kwa kufanya hivyo watakuwa hawakirudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Naye Profesa Noor, katika mkutano huo, alisema baada ya miaka zaidi  ya 30 ya Mapinduzi,Iran imfanikiwa kupiga hatua za kimandeleo kutokana na nguvu za vijana.
Alisema iwapo vijana wataitumia elimu kunauwezekanao wa kuzikomboa nchi zao katika kutegemea misaada kutoka nchi nyingine.
Prefesa Noor alisema maendeleo ya kweli kila nchi hayawezi kupatikana iwapo nchi husika itakuwa ikitegemea misaada mbalimbali ya kutoka nje hivyo ni bora wakachukuwa majukumu ya kuondoa mfumo huo.
Aidha, alisema baada ya nchi yake kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo vikwazo kutoka ilivyokuwa ikiwekewa na Mashirika ya kimataifa imejaribu mbinu za kila aina kwa kuwatumia wasomi ambao ni vijana katika kujiondolea matatizo katika nchi hiyo.
Alibainisha kuwa pamoja na changamoto mbalimbalinchi hiyo inajivunia mafanikio katika nyanja mbalimbali ikiwamo kwenye sekta ya Afya, Elimu na Sayansi.
 
Profesa Noor alisema hali ya kuwekewa vikwazo imetokana na baadhi vyombo vya habari vya nchi za Mgharibi katika kile wanachodai kuwa nchi hiyo imekuwa ikikiuka baadhi ya maazimio ya Umoja wa Mataifa.

MAZINGIRA MAGUMU KWA WANAFUNZI SHULENI NANI ALAUMIWE


HAWA NI BAADHI YA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA  KATIKA SHULE YA
MSINGI MAKUMBUSHO YA JIJINI  DAR ES SALAAM WAKIWA DARASANI, SIJUI WAPO
WANGAPI, WATOTO HAWA HULAZIMIKA KILA MWEZI KULIPA Tsh1000 YA MTIHANI
WA MWEZI,Tsh 1500 YA MTIHANI WA TERM,Tsh500 YA KILA SIKU YA UJI HAPO
BADO TUISHENI,USAFI, MLINZI,LEBO,VIDUMU,FAGIO, NA MADAFTARI PIA
HULAZIMISHWA KUNUNUA HAPOHAPO.

WASANII WATAKIWA KUJIPANGA KUKABILI TEKNOLOJIA MPYA


Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wameshauriwa kujipanga katika kutumia fursa na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati Ulimwengu ukijiandaa kuingia kwenye mfumo wa digital kutoka ule wa nalogia ifikapo mwaka 2014.
Ushauri huo umetolewa wiki hii na Msimazi wa Vipindi vya televisheni wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mwanga Kirahi wakati akiwasilisha mada iliyohusu Teknolojia ya kisasa Katika Utengenezaji Filamu kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba.
Alisema kuwa kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali kutazalisha fursa mbalimbali za kuendeleza Sanaa nchini lakini pia ni mwanzo wa kuibuka kwa changamto nyingi ambazo kama wasanii hawatakuwa makini basi wanaweza kupotea na kushindwa kushindana ipasavyo.
  “Mfumo wa digitali utaleta ushindani katika kuandaa programu za televisheni, utazalisha fursa kwa kazi za wasaniii wetu kuonekana ulimwengu mzima lakini unaweza kuwa mwanzo wa kufa kwa ubunifu kama wasanii watategemea vifaa vya kisasa tu pasipo kuingiza ubunifu binafsi” alisisitiza.
Katika hili aliwashauri wasanii kutengeneza kazi zenye ubora na zisizo za kunakiri kutoka kwa wengine lakini pia zenye ubunifu binafsi pasipo kutegemea vifaa hivi vya kisasa pekee kwani kinyume chake ni kukataliwa kwa kazi zao na hatimaye kupwaya.
“Digital maana yake ni kazi za Wasanii wetu kuonekana Ulimwengu mzima, sasa kama zitakuwa za kunakiri kutoka kwa wengine na kutegemea vifaa hivi vya kisasa tu pasipo ubunifu binafsi hatutafanikiwa. Haya pekee yanazifanya kazi zetu zisivume muda mrefu kwani zinakuwa si original (halisi)i” alizidi kusisitiza.
Aliongeza kuwa, wasanii hawana budi kubadilika sasa na kuacha tabia ya wao kufanya kila kitu kikuanzia umeneja, utunzi, uongozaji (directing), uzalishaji (producing) na kadhalika kwani kwa kufanya hivyo kunazifanya kazi zao kuwa na radha moja pekee ambayo haiwezi kudumu muda mrefu.
Wadau wengi waliofika kupata elimu hiyo kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa waliiomba Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kupanga kukutana na wasanii ili kuwapa elimu juu ya mchakato wa kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.

Vodacom awards 10 Million to grand winner in M-Pesa promotion

Vodacom Tanzania Corporate Communications Manager, Rukia Mtingwa (left), M-PESA Expert Ms, Reenu Verma and the representative of the Gaming Board of Tanzania, Mr Abdallah Hemed follow proceedings during the draw to pick monthly winner of TShs 10 million of the M-PESA Transfer & Win promotion whereby a  Geita resident, Mr Denis Kaesha emerged the winner.
 Vodacom TZ has awarded over TShs 450 million in daily winnings to 9000 customers, and TShs 30 million in monthly prizes.
*       MPESA has endeared itself to customers, resulting into a substantial increase in the number of new adopters who have learnt not only of its reliability but also its ease of use.


Tanzania's leading mobile phone company, Vodacom has presented a cash prize of TShs 10 million to the winner of the ongoing MPESA promotion which targets users of the service during a brief ceremony at the company Headquarters at Mlimani City in Dar es Salaam.
Dennis Kaesha, an accountant from Geita was all smiles as he received news of winning the prize from Vodacom Corporate Communications Manager, Rukia Mtingwa, bringing to a close the M-Pesa Transfer and Win campaign which kicked off in March.
"I am very thrilled with this win. It's unbelievable," said a seemingly pleasantly surprised Dennis.
Dennis now joins Peter Kilalo, a traffic police officer from Dar and Revocatus Mkama, a car mechanic from Mwanza who emerged winners of the monthly grand draws in March and April, respectively.
In her remarks during the conversation with the winner, Rukia urged Vodacom customers to continue using the service, adding that the win was testament that the telecoms operators was increasingly reaching to its customers with innovative products that do not only make life pleasurable but also supports their day to day lives by addressing their unique needs.
The M-Pesa Transact and Win promotion allowed subscribers to win TShs 50,000 daily and a grand monthly prize of TShs 10 million every time they sent money.  To date, Vodacom has awarded over TShs 480 million in daily winnings to 9000 customers, and TShs 30 million in monthly prizes.
"I am pleased to tell you that you are the winner of the MPESA transact and win promotion during the month of May. We are very proud of you and will make every effort to present the money to you soon so that it can help make a difference in your life and your entire family," Rukia announced.
He said Vodacom was keen to use the MPESA platform which continues to experience exponential growth to power the lives of the Tanzanian people, irrespective of their economic standing.
The campaign is intended to not only excite users of the MPESA service and attract more but also to build the customers and general public's trust in its safety, reliability, speed and stability.
Increasingly, MPESA is becoming popular in Tanzania as more people prefer it for; payment of bills, money transfer both locally and across the borders and as a safe haven for money, especially for people on transit.
He said that while the campaign sought to increase the use of the service in the market, the company was also doing everything possible to ensure it remained strong, intact, safer, reliable and more importantly, affordable to all across the country.
The MPESA service was first introduced into the TZ market in April, 2008. Over the years, more service providers have included it in its financial management systems. These include; utility companies such as LUKU, DAWASCO, and DSTV. MPESA is also used to; pay for local flights on Precision Air, pay school fees as well as examination fees to NECTA, deposit and withdraw money through CRDB Bank, to name just a few.

NCHI MBALIMBALI ZAENDELEA KUTANGAZA WAWAKILISHI WAO MISS EAST AFRICA 2012

Miss Lula Teklehaimanot (19) kutoka Ethiopia
Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wanaendelea kupatikana kutoka katika Nchi mbalimbali zinazoshiriki mashindano hayo.
Mrembo mwingine aliyeingia fainali ni Miss Lula Teklehaimanot (19) kutoka Nchini Ethiopia ambae alipatikana mwishoni mwa wiki baada ya kuwashinda warembo wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Ethiopia katika fainali hizo.
Miss Lula Teklehaimanot ana urefu wa 1.79m na uzito wa 52kg ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha St. Merry University cha jijini Addis Ababa, Ethiopia ampapo anasomea degree ya Marketing
Pia Mrembo huyo ni miongoni mwa wanamitindo maarufu  wanaochipukia kwa kasi Nchini Ethiopia.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam

Prostate Cancer Tanzania 50plus