TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 12, 2013

MATUKIO MBALI MBALI TANZANIA KUHUSU BARABARA NA MAZINGIRA .


Ajali za Madereva wa Pikipiki(Bodaboda)  Barabarani Zinaongezeka  kila kukicha kutokana na Madereva wengi wa pikipiki kuwa na mafunzo ya Muda Mrefu, Kijana Jumanne juma, ambaye hayupo pichani muda mfupi baada ya kunusurika na kuikimbia pikipiki katikati ya barabara kitendo ambacho pia ni chanzo cha ajali.


Barabara kuelekea Iringa


Hii ndiyo Tanzania yetu unayosikia kila siku kuwa ina rutuba na rasilimali nyingi kutokana na ardhi yetu, lakini kwa sasa unaweza kujiuliza imeisaidia vipi jamii yake ya watanzania, lakini wakati ardhi kwa tanzania ikionekana kuwa siyo tatizo, ongezeko la vijana kukimbilia mijini limezidi kuongezeka na hivyo kujaza zaidi maeneo ya Mijini kuliko Vijijini, pamoja na kwamba wanaishi katika mazingira ya kukabiliwa na tatizo la ajira kwa watu wake zaidi ikiwa Vijana.

Wakati Tanzania inapata Uhuru, Mapambano makubwa kwa ardhi yake katika kutafuta maendeleo ilikuwa ni kupata barabara zitakazounganisha katika ya mji, mkoa na mkoa, watawala waliotangulia waliweza kuipigania zaidi na kwa kutumia umoja wao katika kufanya vitu vya msingi ikiwa ni pamoja na kufanya barabara kati ya mikoa ya iringa na morogoro inapitika kwa urahisi, lakini changamoto kubwa waliyokutana nayo ilikuwa Milima Mikubwa. je Ingekuwa ni wakati huu ufanyike ujenzi kama huu Tanzania ? Toa Maoni!!

Pamoja na Kwamba kuna Taadhali kubwa zimewekwa Barabarani lakini bado Madereva Wetu wanashindwa kuzingatia, je wanachukuliwa hatua zipi na Tanzania ama Wamiliki wa Barabara(TANRODS) wamenufaika vipi na watu hao, ni kati ya matatizo ambayo yameikumba Tanzania na hivyo kuzidi kutumia barabara zenye wembamba usiostahili kupunguza ajali za barabarani.

Mkoa wa Iringa ni kati ya Mikoa ambayo imevuma na kusikika muda mrefu, hivyo ulitakiwa kuwa na maendeleo makubwa kwa kutumia ardhi na rasilimali walizonazo za nguvu kazi, Mkoa wa Iringa ni kati ya Mikoa yenye Baridi muda Mwingi, lakini je wakazi wa Mkoa huo wamenufaika vipi na Mkoa wao, ni vyanzo gani vya ajira ambavyo Mkoa umejiwekea katika kuwawezesha vijana kutokimbilia miji ya Mbeya na Dar es Salaam,

Miwa ni kati ya Mazao ambayo miaka ya nyuma ilikuwa si adimu kama wakati wa sasa, kutokana na kwamba wakazi wa zamani walikuwa wakithamini Mazao kama Kinga Muhimu kwao kwa Chakula, Tofauti na sasa watu wengi kinga imekuwa ni hela mbayo kama isipotafutwa uwezi kuwa na uhakika wa kuitunza familia kwa familia.

Mwendo kasi ni hatari kwa maana ni chanzo cha ajali za barabarani, na hata pia Matumizi Mazuri ya Barabara ni chanzo kizuri cha kuhepusha ajali, kuwa na tumia uhangalifu barabarani.

Sehemu nyingi za barabara chanzo kimojawapo cha ajali ni Kona, hivyo Madereva mnapaswa kuwa waangalifu zaidi sehemu zenye kona kali.Kona hii ni katika Milima Kitonga. Sehemu ambazo wakati wote Madereva wa Magari ya Abiria(BUS) upita wakiwa na zaidi ya spidi 70, kitendo ambacho ni hatari na ni chanzo kimojawapo cha ajali.

Gari la Mizigo likiwa limekatisha safari zake na kufunga nusu ya barabara, kitu ambacho ni hatari kwa madereva wasiyokuwa waaangalifu barabarani.

Viwanja Tatizo la Soka la Tanzania ama Soka na viwango kwa wachezaji ? ni kati ya maswali ambayo watu wengi kwa Tanzania wameendelea kujiuliza, zaidi ikiwa ni vijijini ambako sasa imekuwa kimya kusikiwa wakitokea wachezaji wenye kutumainiwa na Taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, lakini hata hivyo ikionyesha kutokuwa na mwamko kwa kizazi cha sasa katika michezo kutokana na wengi wa vijana kuwa na mawazo ya kutafuta pesa waweze kuishi, upungufu wa kufika katika viwanja vya wazi limeendea kuikumba Tanzania na hivyo kuifanya kuzidi kuwa na upungufu wa wachezaji wenye vipaji.

Moja ya taswira ya maeneo ya Mikoa ya Tanzania. nchi ambayo inasadikika kuwa na Demokrasia kubwa kuliko nchi ingine yeyote duniani, Ardhi ambayo mpaka sasa Bado imeendelea kuyanufaisha Mataifa kutoka nje, kutokana na kukosa wataalamu wa kutambua na kufanya uchunguzi wa Uwepo wa Baadhi ya Mazingira ambayo mara nyingi yamekuwa yakiibuliwa na wageni , ambao mpaka sasa wameendelea kumiminika katika kuomba kuwekeza.

Eneo hili ni Moja ya Maeneo ambayo wakandarasi , eneo hili baada ya mradi kumalizika kitakachofuata !!!

Tukumbuke kukata miti kisha kupanda miti!!


Kitakachofuata baada ya hapo unadhani ni nini, 
(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)

MASHINDANO YA MIJADALA YA SHULE ZA SEKONDARI MWANZA KUANZA SEPT. 2.

Mkurugenzi wa Stopper Entertainment,  Mukhsin Mambo, akifafanua  jambo  kuhusiana na Mashindano ya Shule za Sekondari(Interschools Debate Compatations)
 Mwalimu wa Shule ya Bwiru Boys, George George, akichangia jambo wakati wa Semina ya Walimu wa Shule za Sekondari..
 Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kitangiri ya jijini Mwanza, Luciana Ududa, akichangia jambo wakati wa Mafunzo hayo
 Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Nyabulogoya ya jijini Mwanza, Witness Mbogora, akichangia jambo wakati wa Mafunzo hayo
Baadhi ya Walimu wa Shule za Sekondari waliofanikiwa kuhudhuria Seminja hiyo katika Ukumbi wa Kimataifa wa JB. Bellemonte Hoteli jijini Mwanza leo.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
===================================================
Mashindano ya Mijadala kwa shule za sekondari mkoani Mwanza (Interschools Debate Competition), yanatarajiwa kuanza septemba 02 mwaka huu.
Akizungumza katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala kutoka katika  shule mbalimbali za sekondari mkoani Mwanza, mkurugenzi wa Stoppers Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Bwana Mukhsin Mambo, amesema jumla ya shule 32 kutoka mkoani Mwanza, zitashiriki katika shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.
Mambo, amesema shindano hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika kujieleza mbele ya jamii.
Amesema nia na madhumuni ya shjindano hilo, mbali na kuondoka na kitita cha zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.
Miongoni mwa shule zitakazoshiriki shindano hilo ni pamojana Nsumba sekondari, Nganza Sekondari, Butimba sekondari, St. Joseph Girls Sekondari, Buswelu Sekondari, New Hellen Sekondari, Hill crest Sekondari, Bismark Sekondari.

Sunday, August 11, 2013

Pepsi Mayors Cup Mwanza- yatingisha wakazi wa jiji la mwanza.

 Moja ya Mabango ya Barabarani katika kuhamasisha michuano hiyo
 Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza, Jose Mlinzi, katika pilika za maandalizi.
 Mkurugenzi wa My Way Entertainment, waandaaji wa Michuano ya Pepsi Mayors Cup, Paul Siboka, katikati, akiwa na baadhi ya Viongozi wa Pepsi katika kupanga Fainali ya Michuano hiyo katika Uwanja wa Nyamagana Mwanza.
 Mkurugenzi wa My Way Entertainment, waandaaji wa Michuano ya Pepsi Mayors Cup, Paul Siboka, na msaidizi wa Masoko wa Pepsi Taki, wakipanga mipango ya Tamasha hilo.
 Moja ya wadhamini wa Pepsi Mayors  Cup, na Wakuu wa Idara ya DUME Condom, wakiweka sawa maandalizi ya Fainali hiyo.
 Afisa Masoko wa Kampuni ya Pepsi, Taki akiwasiliana na Wakuu wa Idara Makao Makuu kuhusu ujio wa Mchezaji na Balozi wa Pepsi, Juma kaseja ambaye alitakiwa kuwasili mjini mwanza kwa ajili ya kukabidhi zawadi za washindi.
 Balozi wa Pepsi Tanzania, Juma Kaseja, akionekana mwenye furaha baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza.
 Balozi wa Pepsi Tanzania, Juma Kaseja,muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa mwanza.
 Juma kaseja na Kala Jelemia, ambao walikuwa wameharikwa katika Fainali hizo
 Hapa wakiwa katika Msafara kutoka uwanja wa ndege
Moja ya wadhamini wa Onyesho na Fainali hizo, DUME, wakiwa katika Maonyesho hayo
.(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Friday, August 9, 2013

Shamra shamra za IDD 2013 Mikumi Morogoro

 Watoto wakazi wa mji wa Mikumi Morogoro, wakifiurahia Sikukuu ya Idd  jana
Kilima Kitonga Barabara ya Iringa na maangaiko kwa Madereva, wakipishana kwa Taabu

TAMASHA LA DEMOKRASIA TANZANIA MAANDALIZI YANAENDELEA DAR,MWANZA, ARUSHA , MBEYA NA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Demokrasia Tanzania 2013- Athony Adam
Baadhi ya washiriki katika fani ya Urembo, Miss Demokrasia Tanzania-Dar es Salaam 2013, Wanafunzi wa Chuo cha DACICO TANZANIA
JENGO LA MAKAO MAKUU YA MISS DEMOKRASIA TANZANIA- DAR ES SALAAM

FAINALI YA PEPSI MAYOR'S CUP MWANZA 2013 NDANI YA NYAGANI 10/8/2013 MAANDALIZI YAMEKAMILIKA.


 ,Mwezeshaji wa TMARC ,Said Salum, akitoa maelekezo ya matumizi sahihi ya DUME  Kondom 2013 MWANZA PEPSI MAYOR'S CUP
 Muelimishaji wa TMARC Mr. Suleiman  akitoa maelekezo ya matumizi sahihi ya DUME  Kondom 2013 MWANZA PEPSI MAYOR'S CUP.
Mwezeshaji wa TMARC , Mr. Marc  Boniface akitoa maelekezo ya matumizi sahihi ya DUME  Kondom 2013 MWANZA PEPSI MAYOR'S CUP.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania),